Hivi kweli kuna Vijana Watanzania bado wanataka CCM iendelee kushika dola 2015?

vijana waliobaki wanaichagua ccm ni wale mambulula wanaokula kwa shemeji zao mwenye timamu hawezi kuangaika na ccm
 
niko vijijini nafanya utafiti , ccm imekwisha , kilichobaki ni madaraka tu ! Na mkijiloga mkaboresha daftari la wapiga kura ( kitu ambacho ni lazima , mtake msitake ) ndiyo kaburi lenu .
inategemea utafiti wako unaufanyia wapi na ni vijiji vingapi.kama ni baa hao walevi wanakupa moyo tu ili uedelee kuwapa ofa.ulevi ukiisha huwapati tena
 
Japo mimi siyo kijana najisikia kuchangia mada hii sababu ni mwananchi na nina watoto vijana. Kwa maoni yangu vijana na hasa wa elimu ya juu wanao pigania CCM ni kwasababu au hawajawa huru kifikra au wanamtazamo wa maslahi binafsi au maslahi kikundi au kupenda shortcuts tajirishi hata kama zina athari za kimaangamizi. Katika baadhii ya mazungumzo vijana wasomi wanakuambia ukitaka fursa kuwa CCM. Hoja zao zinazua maswali kama elimu yao ni ya kiuchambuzi zaidi au ni kifuata mkumbo zaidi? Wana msaada gani kwa wasioenda shule? Kuweka madarakani kwa kura halali chama W au X badala ya chama Z na hasa ikiwa kimekaa zaidi ya miaka 50 ni jambo la manufaa kuliko balaa hata kwa chama chenyewe. Chama W au X kikikamata dola hakiwezi kujisahau au kupuuza wananchi sababu kinajua wapiga kura wameshajua nguvu yao. Vijana wachache waliofunguka wasikate tamaa ufunguaji vijana waliofungwa ufahamu uendelee. Tusidanganyane eti vyama zaidi ya CCM havina rasilimali watu hao, tuchague vingine vyama kisha tuone makada wapo!
 
japo mimi siyo kijana najisikia kuchangia mada hii sababu ni mwananchi na nina watoto vijana. Kwa maoni yangu vijana na hasa wa elimu ya juu wanao pigania ccm ni kwasababu au hawajawa huru kifikra au wanamtazamo wa maslahi binafsi au maslahi kikundi au kupenda shortcuts tajirishi hata kama zina athari za kimaangamizi. Katika baadhii ya mazungumzo vijana wasomi wanakuambia ukitaka fursa kuwa ccm. Hoja zao zinazua maswali kama elimu yao ni ya kiuchambuzi zaidi au ni kifuata mkumbo zaidi? Wana msaada gani kwa wasioenda shule? Kuweka madarakani kwa kura halali chama w au x badala ya chama z na hasa ikiwa kimekaa zaidi ya miaka 50 ni jambo la manufaa kuliko balaa hata kwa chama chenyewe. Chama w au x kikikamata dola hakiwezi kujisahau au kupuuza wananchi sababu kinajua wapiga kura wameshajua nguvu yao. Vijana wachache waliofunguka wasikate tamaa ufunguaji vijana waliofungwa ufahamu uendelee. Tusidanganyane eti vyama zaidi ya ccm havina rasilimali watu hao, tuchague vingine vyama kisha tuone makada wapo!

shikamoo mzee .
 
Vijana wanaoitaka ccm ni wale watoto wa mafisadi,majangili,wauza sembe na punda wa mizigo,wengine tumeshavua gamba zamani na kuachana na ukoo wa mapanya.
 
Vijana wengi bado wanaikubali CCM mfano mdogo mmeona jimbo la Kalenga na Chalinze.
 
Nimefuatilia comments za vijana wengi kwenye mitandao yakijamii na kwingineko nimesikitishwa kuona vijana wengi hawajui wanachokitaka. Hawajitambui, hawajui future yao na wala hawana msimamo kamili. Vijana hawa wanalalamikia ajira na serlikali inawaambia wajiajiri. Sawa kujiajiri ni jambo jema lakini je Serikali imeandaa mazingira rafiki ya vijana kujiajiri? Serikali hiyohiyo ya ccm licha yakuwataka vijana kujiajiri lakini haijawahi kufafanua ni mazingira gani vijana wanajiajiri. Wala hakuna ndoto za ccm kuondoa tatizo la ajira. CCM insert kujisifu tu kwamba ni nambari one kakini je imejjipima na nani? Hivi ccm inavyong'ang'ania kuendelea kushika dola itafanya nini au inanini cha tofauti chakuwashawishi vijana kuichagua? Na wewe kijana yaani na akili zako zooote unazani ccm wanajipya gani zaidi ya huu umasikini waliotusababishia kwa makusudi na kwakushindwa kutumia rasilimali zetu vizuri?

Sasa kwakijina ambae ndo kwanza unataka kuanza maisha na hujui unaanzia wapi, hivi bado unawaza CCM iendelee kushika dola? Hivi unatumia kigezo gani kuichagua CCM chama ambacho hakina nia mzuri ya future yakijana mTanzania? Kwanini vijana sasa tusichague upinzani ambao vyama vya upinzani vimeonesha makusudi mzuri yakuinua vijana kifikra, Kiuchumi na kielimu. Hivi kama ccm imeshindwa kabisa kutatua tatizo la ajira kwa zaidi yamiaka 50 bado kuna kijana anaota ndoto kwamba ccm inaweza kutatua tatizo la ajira?

Naomba vijana wenzangu tutumie akili yetu na kura zetu kuiangusha ccm katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015? Tusikubali kushikiliwa akili zetu na ccm.

Ewe kijana Mtanzania tafakari chukua hatua.

Unasikitisha sana kwa kuwa na dhanna ya kungoja kufanyiwa kila kitu.

Jiulize, vijana walioweza walifanyiwa na nani?

Wewe kama wakukosa wakukosa tu hata ufanyiwe nini hutobadilika. Anza kwa kujifanyia na kuifanyia serikali na nchi yako.

Kijana mzima unangoja kufanyiwa? utangoja sana, labda ufanyiziwe.

Punguani wahed.
 
Ninauwezo wakukuajiri wewe na ukoo wako wote nakuwalipa mishahara kwa miaka 100 bila kuyumba. Turudi kwenye mada mkuu. CCM hakuna ilichofanya chakunishawishi kuichagua. Haina mtazamo wowote kwavijana. Imewekeza kwenye siasa za mazoea yusitarajie jipya huo undo ukweli kama hutaki haulazimishwi lakini ccm haina jipya.
 
Vijana wengi bado wanaikubali CCM mfano mdogo mmeona jimbo la Kalenga na Chalinze.

Wanaoichagua ccm ni wale wazee ambao hawajui kusoma wala kuandika na hao sio kwamba wanapenda kuchagua ccm bali wanachakachuliwa na wasimamizi ambao wanawaomba kuwasaidia. Hakuna kijana anayejitambua ataichagua ccm hata siku moja. Unapotaja majimbo yavijana usisahau Ubungo, Kawe, Kigoma kusini&Kaskazini, Mbeya mjini, Arumeru, Arusha, alafu kokotoa utatia akili. CCM nikama maiti isiyo na ndugu, itazikwa tu kwa msaada wa jiji.
 
Naomba tafsiri ya kuanza Maisha

Kuanza maisha kwa tafsri yangu binafsi isiyo rasmi ningesema ni kuanza kujitegemea, yaani kijana kuanzia +18 anaachana na utegemezi wa wazazi katika mahitaji yake yakila siku nakuanza kujitafutia yeye mwenyewe. Hiki ni kipindi kigumgu ambacho vijana wengi wanapotea kabisa na wachache ndo wanafanikiwa. Wanaopotea ni wale ambao walikosa msaada wakimaandalizi na wanaofanikiwa ni wale ambao waliandaliwa. Mfano ushindi wa Riziwani Chalinze na Mgimwa Kalenga umatokana na msaada wakimaandalizi na wala sio juhudi zao ingawa hapa JF watu wanawasifia kinafikinafiki.
 
ccm inapendwa na vijana wazembe wanaofikiria kupata short cut ya maisha kwa kubebwa,watoto wa mafisadi na wauza unga,watoto wa majangili na wale vijana punda wabeba mizigo.Hakuna kijana anayejitambua anayeweza kushabikia hilo genge la wahujumu uchumi wa taifa lake.
 
Ninauwezo wakukuajiri wewe na ukoo wako wote nakuwalipa mishahara kwa miaka 100 bila kuyumba. Turudi kwenye mada mkuu. CCM hakuna ilichofanya chakunishawishi kuichagua. Haina mtazamo wowote kwavijana. Imewekeza kwenye siasa za mazoea yusitarajie jipya huo undo ukweli kama hutaki haulazimishwi lakini ccm haina jipya.

Ungekuwa na uwezo ungelalamika kutaka kufanyiwa?

Chopa tatu kata tatu.
 
Nimefuatilia comments za vijana wengi kwenye mitandao yakijamii na kwingineko nimesikitishwa kuona vijana wengi hawajui wanachokitaka. Hawajitambui, hawajui future yao na wala hawana msimamo kamili. Vijana hawa wanalalamikia ajira na serlikali inawaambia wajiajiri. Sawa kujiajiri ni jambo jema lakini je Serikali imeandaa mazingira rafiki ya vijana kujiajiri? Serikali hiyohiyo ya ccm licha yakuwataka vijana kujiajiri lakini haijawahi kufafanua ni mazingira gani vijana wanajiajiri. Wala hakuna ndoto za ccm kuondoa tatizo la ajira. CCM insert kujisifu tu kwamba ni nambari one kakini je imejjipima na nani? Hivi ccm inavyong'ang'ania kuendelea kushika dola itafanya nini au inanini cha tofauti chakuwashawishi vijana kuichagua? Na wewe kijana yaani na akili zako zooote unazani ccm wanajipya gani zaidi ya huu umasikini waliotusababishia kwa makusudi na kwakushindwa kutumia rasilimali zetu vizuri?

Sasa kwakijina ambae ndo kwanza unataka kuanza maisha na hujui unaanzia wapi, hivi bado unawaza CCM iendelee kushika dola? Hivi unatumia kigezo gani kuichagua CCM chama ambacho hakina nia mzuri ya future yakijana mTanzania? Kwanini vijana sasa tusichague upinzani ambao vyama vya upinzani vimeonesha makusudi mzuri yakuinua vijana kifikra, Kiuchumi na kielimu. Hivi kama ccm imeshindwa kabisa kutatua tatizo la ajira kwa zaidi yamiaka 50 bado kuna kijana anaota ndoto kwamba ccm inaweza kutatua tatizo la ajira?

Naomba vijana wenzangu tutumie akili yetu na kura zetu kuiangusha ccm katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015? Tusikubali kushikiliwa akili zetu na ccm.

Ewe kijana Mtanzania tafakari chukua hatua.
NANI KAKUDANGANYA KUWA ETI""""vijana wengi wanaipenda ccm???""". ukweli ni kwamba vijana wengi wa tanzania wamechoshwa na ccm lakini hawaoni kimbilio. hata wewe hapo unajua fika kwamba HAKUNA MBADALA WA CCM na hivyo basi hicho kinachokufanya ukipende hicho chama ukipendacho ni UPOFU NA UJINGA ULIOKUGUBIKA.
jichunguzeni, je mnastahili kupewa uongozi wa hata mkoa mmoja kwa siku 100?? kila siku ninasema na ninaamini kuwa TATIZO KUBWA LINALOIKABILI HII NCHI SIO CCM bali ni vyama vya upinzani kukosa watu wanaweza kuaminika kuchukua nafasi ya ccm. hili ndio tatizo linalotukabili kuliko uwepo wa ccm yenyewe. kama unajaribu kuukwepa ukweli na kuzielekeza lawama kwa vijana wa tanzania!! hiyo ndiyo hulka yenu( ya kujivua majukumu na lawama na kutafuta wa kuwatwisha).
kwa jinsi ninavyoona,2015 ndio litakuwa anguko kuu la upinzani wa tanzania kwani zaidi ya 3/4 ya majimbo mliyoshinda 2010 yatawaponyoka na idadi ya kura za uraisi itakuwa ndoooooogo kiasi cha kuathiri ruzuku za chama chenu. na kwa sababu ruzuku ni moja kati ya mfupa katika koo la chama chenu, basi upungufu wa ruzuku ndio utakaokuwa msumari wa mwisho katika jeneza lenu
HUU NI UKWELI AMBAO MNAUUA MIOYONI MWENU JAPO MKIJA MAJUKWAANI MNAHUBIRI TOFAUTI.
JICHUNGUZENI NA MCHUKUE HATUA KABLA HAMJAFUTIKA KATIKA SIASA ZA NCHI HII
 
ccm inapendwa na vijana wazembe wanaofikiria kupata short cut ya maisha kwa kubebwa,watoto wa mafisadi na wauza unga,watoto wa majangili na wale vijana punda wabeba mizigo.Hakuna kijana anayejitambua anayeweza kushabikia hilo genge la wahujumu uchumi wa taifa lake.[/QUOTE
KAMA JINSI AMBAVYO CHADEMA KINASHABIKIWA NA WANYWA MBEGE NA WEZI WA MAGARI NA MITANDAO YA UJAMBAZI.
 
Back
Top Bottom