Hivi kwanini wanawake hawapishani kwenye siti wakiona mwenzao mjamzito kasimama?

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Leo nikiwa kwenye daladala nilikaa kwenye siti, row ya 3 hivi kutoka mlangoni, siti za mbele yangu walikuwa wamekaa wanawake watupu, maeneo fulani hivi akaingia mdada mjamzito tena tumbo kubwa kachoka.

Kilichonishangaza wanawake wote mbele yangu wakajikausha kama hawajamuoni vile mwenzao kasimama na tumbo lake, wengine wanazuga wako bize na smart phone zao, nikamuonea huruma ikabidi nimpishe siti akae.

Swali la kujiuliza hivi kwanini wanawake hawapendi kupishana siti tena wakiona mwenzao mjamzito mpaka asimame mwanaume?
 
Hakuna kitu kama hicho tunapishana sana. Mbona nyie mkiona mwaume mwenye busha hammpishi. Kwendraaaaaa. Kila mwanamke anajua kwamba nikitu kizur kumpisha mwenzie akiwa katika hali hiyo, tutolee upuuuzi wako hapa. Hata awe hajaza lazima awe nahuruma maana wote tunjua hiyo hali ni delicate sana
 
Wanawake wanajua wenyewe hisia zao kuna mmoja nilimuuliza akajibu" Wengine wanakera magari yapo kibao na anajua ana mimba au yupo na mtoto anapanda lililojaa ana uhakika atapishwa,Mimi kama kuna shida ya usafir nampisha ila kama kuna magari mengi ila anajifanya ana haraka najifanya sijamuona"mwisho wa kunukuu
 
Ila kuna saa wengine wanafanya makusudi kabisaaa. Mfano huku kanda ya ziwa hakuna tatizo la usafiri daladala nyingi zinakuwa na seat hasa mida ya mchana unakuta mwanamke mjamzito au mwenye mtoto anaona kabisa gari imejaa,makusudi anapanda akitegemea huruma ya kupishwa siti,heee kila mtu ana uchovu wake,mtu umechooka gari imejaa ukimpisha mtu inakula kwako unasimama vituo karibu saba bila kupata siti aah kama ni roho au tabia mbaya basi iwe hivyo tu.
 
Hakuna kitu kama hicho tunapishana sana. Mbona nyie mkiona mwaume mwenye busha hammpishi. Kwendraaaaaa. Kila mwanamke anajua kwamba nikitu kizur kumpisha mwenzie akiwa katika hali hiyo, tutolee upuuuzi wako hapa. Hata awe hajaza lazima awe nahuruma maana wote tunjua hiyo hali ni delicate sana

Hahahahahahaha ulivyosema uko pande za Temeke sibishi.
 
Hakuna kitu kama hicho tunapishana sana. Mbona nyie mkiona mwaume mwenye busha hammpishi. Kwendraaaaaa. Kila mwanamke anajua kwamba nikitu kizur kumpisha mwenzie akiwa katika hali hiyo, tutolee upuuuzi wako hapa. Hata awe hajaza lazima awe nahuruma maana wote tunjua hiyo hali ni delicate sana
Povu lote hili la nini? Ukweli ni kwamba hawakumpisha mwenzao
Unachofanya wewe ni kutaka kutetea kosa kwa kosa lingine.
 
Hapana si wote kabisa... Me huwa nawapisha sana maana naelewa jinsi anavokua anajisikia.
 
Wanawake wana roho mbaya sana na si wa kuaminika kabisa. Wee fikiria % kubwa ya wanawake wakiona mwanamke mwenzao kapendeza tuu , shida watageuza geuza mimacho na kumchambua mpaka basi, awasifiana viumbe hivi , pili mwanamke roho ngumu na mbaya sana . Ukitaka uhudumiwe vibaya kwenye sehemu za starehe wee nenda na mwanamke uone kazi ,hila siku ukienda mwenyewe aahaha muhudumu wa kike atakunyenyekea mpaka utafurahi mwenyewe.Hawa ni mama zetu dada zetu na mashangazi zetu , lakini ni wa kuwaangalia sana kwa kweli
 
Leo nikiwa kwenye daladala nilikaa kwenye siti, row ya 3 hivi kutoka mlangoni, siti za mbele yangu walikuwa wamekaa wanawake watupu, maeneo fulani hivi akaingia mdada mjamzito tena tumbo kubwa kachoka.

Kilichonishangaza wanawake wote mbele yangu wakajikausha kama hawajamuoni vile mwenzao kasimama na tumbo lake, wengine wanazuga wako bize na smart phone zao, nikamuonea huruma ikabidi nimpishe siti akae.

Swali la kujiuliza hivi kwanini wanawake hawapendi kupishana siti tena wakiona mwenzao mjamzito mpaka asimame mwanaume?
Kama amezaa au anatarajia kuzaa anaweza kumwonea huruma ila nasikia warembo wa dar wengi hawataki kuzaa watapoteza uzuri, kuna shida sana kumbe hawajui uzuri haudumu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom