Hivi kwanini wahaya na wajaluo huwa wanachanganya Kiswahili na Kiingereza katika maongezi yao

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
Katika pitapita zangu za hapa nimekutana na makabila mengi Tanzania yenye mila na desturi tofauti katika kufanya kazi zangu

Ila katika pitapita zangu kila ninapokutana na watu tokea kabila la wahaya na wajaluo kila mnapokuwa mkifanya mazungumzo hupenda kuchanganya Kiswahili na Kiingereza .......

Je ni kwanini Wajaluo na Wahaya huwa mnapenda kuchanganya kiswahili na kiingerezaaaa
 
Kwa sababu kuna maneno mengine hawayajui kwa kiswahili lakini wanayajua kwa kiingereza, pia kuna maneno hawayajui kwa kiingereza bali kwa kiswahili, na wanapochanganya sio kwamba wanaongea lugha mbili tofauti bali lugha moja.
 
Sio kwa hayo makabila tu, Kwa mtanzania yoyote aliyepita pita kwa Ras Simba...

Na ukitaka ulijue hilo angalia interview za wasanii wetu, ndio yaleyale ya because am strong woman...(hamorapa voice)
 
Wahaya na wajaluo wanafanana kwa kupenda sifa.

Pili niliwahi kuambiwa kua wahaya na wajaluo ni watani wa jadi lakini pia wana vinasaba ingawa sina uhakika maana kijaluo sio kibantu ila kihaya ni kibantu.

Kanda ya ziwa ndio inaongoza kua na watu wanaopenda sifa Tanzania nzima.

Angalia wahaya, wajaluo, wajita kina Mafuru wakwaya kina mihongo, wakurya, wakara, wakerewe, wasubi kina mukulu wa bakulu. Hawa wanasumbuliwa na ile kitu wanaita superiority complex disorders.

Kanda ya ziwa kabila pekee lisilopenda kujikweza ni wasukuma, wao kila kitu ni ntobo tabhu, ntoho shida.
 
Mbona imekuwa kawaida kwa watanzania wengi kuchanganya lugha hizi mbili. Ni makabira yote especially kama mtu amesoma hata kwa level ya form 4.
 
Hali hii inatokana na mazoea ya kufikiri kwa lugha ya kiingereza huku ukilazimika kuwasiliana kwa kiswahili. Ukiwa makini unaweza kulikwepa hili kwa kuamua kwa makusudi kufikiria kwa lugha ambayo utaitumia kuongea
 
Back
Top Bottom