Ikoko
JF-Expert Member
- Jul 15, 2022
- 2,101
- 3,036
Wadau tumetoka Dar na Bus la HAPPY NATION saa 12 asubuhi na tumefika hapa Sikonge, Tabora Bus limezuiwa kuendelea na safari eti mpaka saa 12 asubuhi, eti kwa sababu njiani kuna mapori makubwa.
Kwa maoni yangu hii si sawa kabisa, yaani pamoja na jitihada kubwa za serikali kukamilisha barabara hii na sasa ni lami kutoka Dar mpaka Mpanda, bado tunawapotezea muda watanzania kukaa hapa masaa 8 kisa hatuwezi kuimarisha usalama?
Hivi tutajikwamua vipi na umasikini ikiwa tunapoteza muda kiasi hiki? Halafu sehemu yenyewe hakuna hata stend yenye facilities za kuhudumia hata abiria wa Bus mbili. Kingine cha kushangaza kwenye maamuzi yetu ni kwamba hivi unawezaje kuacha bus ilale Tabora mjini kwenye huduma nyingi halafu uje kuzuia ma Bus Sikonge?
Kwa staili hii ya kupotezeana muda kiasi hiki uchumi wa kati tutausikia tuu kwa wenzetu. Nimesikitika sana kwa kweli.