Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Hili jambo sasa limetamalaki mno kwa Viongozi, pamoja na Graphic Designer wa Yanga, kutoheshimu logo maalum za timu nyingine, jambo ambalo si sahihi kwakweli tukiweka ushabiki pembeni.
Wenye mamlaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, BMT, TFF mko wapi katika hili mbona kimya? Kulikoni.
Mbona kampuni ya simu Vodacom na GSM ambao ni wadhamini wenu wamewaheshimu na kukubali kubadili rangi zao nyekundu na kuweka rangi zenu, kwanini Yanga haiheshimu logo ya timu zingine?
Logo ni sehemu muhimu sana ya utambulisho wa brand yoyote ikiwa ni klabu, Kampuni au Taasisi, ambayo inakuwa na rangi maalum tofauti tofauti ambayo inapaswa kuitambua na kuiheshimu, lakini kwa Yanga hili jambo wameshindwa kabisa na kulitambua kulifanyia kazi.
Kama wapinzani wao wa jadi Simba wanatumia rangi nyekundu ambayo kwa mila za Yanga hawawezi kuiweka hiyo haina shida, lakini je timu nyingine za Azam FC, Ruvu Shooting, Mbeya City? Kwanini mnaharibu logo za timu zao?
Huu ni ushamba uliopitiliza ambao hausaidii chochote katika maendeleo ya soka la Tanzania, haiwezekani timu takriban 20 kwenye VPL hawafanyi huu ujinga halafu Yanga pekee ijione iko sawa katika hili, kwingineko hii ni kesi kubwa sana ambayo inaweza kuigharimu klabu, lakini hapa wahusika wanachukulia kawaida tu.
Nawasilisha