Hivi kwanini kila ninachokifanya mke wangu haridhiki?

Upendo, heshima, uvumilivu na tabia ya kweli ya mke/mchumba hujulikana pale mchumba/mume anapostruggle kufanikiwa au pale mume anapotetereka kiuchumi.

Sasa hivi ndo unaona tabia halisi ya mkeo. But all in all don't let her bitterness weakens you/your life. Muache hivyo hivyo na dharau zake, ipo siku atakuheshimu tena kwa magoti.

Concentrate na duka lako, tena Jitahidi usiwe unakaa naye sana manake utasikia kebehi zake. Endelea kumjali na kuwajali watoto wako, uzuri watoto wana macho na wanaona kinachoendelea, so siku zote heshima na upendo wao kwako utabaki pale pale. Heshima ya mwanaume ni kazi, so Piga kazi, Mungu atakuinua tena

Huyo rafiki wa mkeo hata usiwaze kabisa kuwa nae. Sasa hivi upo so down, hivyo mtu yeyote ayakayeonesha kukutia nguvu ( anaboost confidence yako) unaweza ukahisi unampendaaa, kumbe sio upendo maybe ni huo upweke ulionao as mkeo ni kama anakutenga. Mungu akusaidie na akuinue, huyo mkeo Mungu atadeal naye sawasawa na atakavyoona. Mmh kweli watu hatujui thamani ya kitu hadi kiondoke, huyo mwanamke sijui anataka Mungu ampe nini khaaa

Nakubaliana na wewe 100%
 
Muoneshe mapenzi ya kiwango cha juu kadiri uwezavyo huku ukitafuta gheto hapo hapo mtaani hakikisha siyo mbali na nyumbani then panga but usiache kuwahudumia wanao.mwanamke hapigwi mangumi na mateke braza ulikosea sana unampigaje mwanamke physically bwana?
 
Wakati mwingine Mungu anapokupa mitihani si kama hakupendi bali anataka akuonyeshe taswira halisi za watu wanaokuzunguka.

Kabla ya hapo ulihadaika ukajua umepata bonge la mke.
Sina cha kukushauri kwa sababu umesema unajua cha kufanya na umesema usilaumiwe. Ok go on.
 
pole sana. uko sahihi kila kitu isipokuwa hapo kwa mjane mwenye "huruma"! anaweza akawa anakuonea huruma kweli kama wengine tulivyokuonea huruma hapa lakini iko kama anavuka mipaka. si ajabu keshaanza kukufananisha na marehemu mumewe. we haya! Yesu alijaribiwa ile ile siku aliyosikia njaa shetani akamwambia amsujudie ampe mkate. Na jaribu lilikuja siku ya mwisho kabisa. sasa we sasa hivi una njaa ya upendo, huruma na usalama wa kihisia. umekomaa kiume toka 2012, sasa unapoona unaanza kuyumba ujue unakaribia ushindi. usikubali mjane akuharibie ushindi wako. Kama una imani huu ndo wakati wa kukomaa na Mungu wako akushindie na hawa wanawake wawili. endelea kufanya kama ulivyokuwa ukifanya zamani - lea familia, tafuta hela, sahau kuchepuka. Mahaba yakikuingia utafakamia, utavimbiwa na spidi ya kutafuta hela na kuwaza watoto wako itapungua. Kanuni ya tatizo kama lako ni kuwa ukivumilia mpaka mwisho mkeo atakuja kufulia ili ajifunze kuthamini utu wako. Na wewe kuna kitu utakuwa umejifunza.

dah! We dada cjui umeshikwa ufahamu na malaika il umsaidie huyu jamaa,umeongea kwa busara sana am much impressed with your comment,kama jamaa kaisoma hi itamsaidia sana,ubarikiwe
 
Pole, ila naendelea kuamini ndoa sio harusi, kama ni ndoa ya kikristo kua makini, ni mke mmoja mume mmoja hadi kifo!

Hiki ndicho kinachowapa kiburi wanawake,ukishajua ni ndoa ya kikiristo unaamini huwezi kuachika hadi kifo hata ufanye upumbavu kama huo.

Ndio maana mimi nimeamua kuachana na mambo ya dini ili niwe huru nisifungwe na masharti yoyote.
 
Kuna vitu umeficha, mwanamke wa hivyo hata unyumba hakupi kwa sababu anaona wewe sio wa level yake, hana hamu na wewe, huna mvuto, anaona unamsumbua etc. Tatizo ni moja, bado huna ground za kumwacha. Kikubwa mambo yako yakiwa safi na wewe mpuuze. Tafuta nyumba ndogo nzuri mahali awe anakutoa stress. Basi
 
Hio ndoa yako ni kama mkataba wa kazi serikalini,watu full kuzembea tu na hawaguswi...
Ushauri wangu ni hivi,just man up na kuhusu kuvumilia upuuzi wa mwanamke sio jambo rahisi,sometimes kumu ignore huwa inasaidiaga and if i were me ningezungumza nae juu ya itikadi zake za kishamba na kumueleza consequences zinazoweza kutokea kama akiendelea kunipuuza.Mwanaume heshima bhana na isitoshe una watoto nae kabisa,Yeye kama anadhani hilo la kukuheshimu bila shuruti litakuwa mtihani basi naye ajiandae kutoheshimiwa kwa we kupiga pini tu mpaka atapojirekebisha.Mchepuko huwa sio kitu kizuri ila kwa hali ulionayo sasa hakika unauhitaji sana uwe kama anti-depressant yako ili uendele kupambana na life,mind you asiwe yule shemeji yako anaekusaidia maana ukishamgonya utatengeneza deni na uhasama mkubwa nikimaanisha misaada hutaipata tena bila kumgusa mara kwa mara na pia mkeo akijua ndio itakuwa tiketi ya kuvunjia ndoa!
 
Poleni mliooa..
malizia bana: "poleni mliooa pasua vichwa". ndoa ni nzuri ila kwa kuwa wanadamu ni dhaifu haikosi shida za hapa na pale. Swala ni kuwa wote wawili mko committed kiasi gani kuhakikisha ndoa haimezwi na matatizo. Ukijikuta peke yako ndo unapigana isife lazima upewe pole maana ni mateso.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom