Hivi kwanini kila ninachokifanya mke wangu haridhiki?

Hivi kwanini kila ninachokifanya mke wangu haridhiki?

Joined
Oct 2, 2015
Posts
5
Reaction score
10
Mwaka 2012 nilipata matatizo kazini, tangu hapo nimehangaika sana kutafuta kazi nyingine bila mafanikio, katika kipindi chote hiki familia yangu haijawahi kulala na njaa hata siku moja, hii ni kwa sababu nimekua mhangaikaji sana hata kama ni kazi za hovyo nitafanya ili mradi nyumbani mambo yaende

Lakini mke wangu ambae ni mwajiriwa amekua hana shukrani kwa yote nayoyafanya, hatoi mchango wowote katika familia pamoja na kuwa na kazi, pesa zake ni kujipamba, kuhudumia Gari lake, nguo Mpya kila siku na kadhalika, pamoja na ukweli kuwa mimi ndie kichwa lakini nahitaji kusaidiwa kwa kuwa sina kazi, nachofanya nikiamka asubuhi na kwenda town yote yatajulikana huko, kwa msaada wa washikaji napata dili ndogo ndogo nimeweza kumudu mahitaji yote ya familia, chakula, electricity bill, water bill, ada za watoto na mengine mengi for the past three years,

Kuna siku Rafiki wa wife aliniomba maongezi, akaniuliza umefikia wapi katika kutafuta kazi, nikajibu naendelea kutafuta, lakini hata hivyo home hakuna kinachokosekana, natimiza mahitaji yote yanayotakiwa kwa shughuli nazopata, akashangaa sana, akasema mbona mkeo anakuzungumza vibaya kwenye ma group yetu ya marafiki! Anasema hufanyi chochote umekua ni kama gunia hadi ubebwe.

Niliumia sana, yule Dada aliniambia kejeli nyingi sana anazozungumza wife ambazo pia nimeshazisikia Mara kadhaa kwa ndugu Wa karibu

Nimesikitika kwa sababu yote hayo si ya kweli, juzi nimefungua Duka Mtaani kwetu baada ya kudunduliza sana, cha kushangaza wife hakupenda kabisa idea hiyo, akidai namdhalilisha yeye na familia kwa kuuza kibandani, anakiita kibanda, kwamba watu walizoea kuniona natoka ndani ya Gari na tai na Gari sasa nauza kibanda, eti bora ningetafuta sehemu ya mbali
Ukweli ni kuwa nataka nijue mapato ya siku na biashara inavyokua ndipo nimuache mtu

Siku hiyo nilimpa kipigo kizito sana, kwa majibizano hayo baada ya kauli za kuudhi, tangu kuondoka kazini 2012 nimejiepusha kuwa mzigo kwa mwenzangu kwa kuondoka alfajiri na kurudi usiku, kama ningekua nimemuachia majukum ya kifamilia yy hapo angeweza kulalamika, kama huduma hazifanani na wakati ule nipo kazini hilo ni suala lingine na ziada sio basic need

Sijawahi kumsumbua wife hata nilipokua kazini, sijawahi kuwa na mchepuko wala nini, sasa iweje yeye ashindwe kuwa na utu

Inafikia pahala watoto wanakula mezani anawaambia kuwa kuleni tu hayo majani siku baba yenu akiwa tajiri mtakula kuku, wakati Jana yake watoto wamekula kuku au nyama, anawajengea nini hawa watoto dhidi yangu? Halaf yy hata kubeba nusu kilo ya nyama hamna

Kumbe wanawake wanaweza kubadilika kiasi hiki kama Mume umepatwa na matatizo!

Siku wakija wageni wake kutoka kutoka ndipo atanunua mazagazaga kibao waweze kula vizuri, wakija wa kwangu hajishugulishi na chochote, hadi mgeni anashtuka kuna tatizo ndani ya familia

Sasa basi nimechoka na hali hii, nimeghafilika sana, natamani sana Rafiki wa wife ndio angekua mke wangu, ana Upendo na mimi, kwa kujua hali yangu amekua akinitumia hadi fedha kwa simu hata bila kuhitaji, nikimwambia sikua nahitaji fedha anasema chukua tu shemeji najua hali yako,

Ni bahati mbaya tu alifiwa na mumewe lakini ni mtu mwenye kunijali sana,
Mama yangu mzazi alikuja hapa kwa operation huyu shemeji yangu alizunguka na na mama muhimbili wiki nzima na alitumia pesa zake hadi mwisho, yy anafanya kazi hapo hospitalini, wakati huo wife hakujishugulisha kabisa alikua akisema Rafiki yake atafanya kila kitu hapo hospital

Nimefikia mwisho, nitafanya maamuzi magumu sana

Sijawahi kuwa na gubu wala kinyongo, maana mm ni mchakarikaji, sijawahi kuomba mtu hela natafuta mwenyewe, huku naendelea kushughulikia suala la kazi, lakini hata kama sikupata nitakomaa huku kwa business hadi nitoke, masikitiko yangu ni kwa huyu mke wangu ambae hanipi support.

Kumbe ndio maana watu waliopata matatizo kazini na kusota sana siku wakifanikiwa maisha tena wanawaacha wake zao na jamii inaanza kuwalaumu kwamba wamekimbia familia zao baada ya kupata mafanikio tena, kumbe hawaelewi kuwa mtu unaamua kumuacha mke ukikumbuka matendo, manyanyaso, Maneno, kejeli, masimango na dharau wakati ukiwa juu ya mawe

Najua nitafanya nini, naomba nisilaumiwe.
 
daaah!!!
pole sana ila em tujuze huyo mkeo umemtoa kwenye hali gani ya maisha ya kwao...!!!!
namaanisha kiuchumi kwao kupoje....!!!!!
 
Pole, ila naendelea kuamini ndoa sio harusi, kama ni ndoa ya kikristo kua makini, ni mke mmoja mume mmoja hadi kifo!
 
Pole sana ndugu,yaani inaumiza vibaya sana lakini wewe komaa wala usijali na wala tabia hizo hazina kabila kusema wapare! Shit happens in life na Mungu lazima akujaribu komaa ila yakianza kuwa poa wanaanza kujileta aiseeee mi kaa mbali kabisa!
 
Umenifunza kitu bro, itabidi nioe mhaya sasa.
 
Mwaka 2012 nilipata matatizo kazini, tangu hapo nimehangaika sana kutafuta kazi nyingine bila mafanikio, katika kipindi chote hiki familia yangu haijawahi kulala na njaa hata siku moja, hii ni kwa sababu nimekua mhangaikaji sana hata kama ni kazi za hovyo nitafanya ili mradi nyumbani mambo yaende

Lakini mke wangu ambae ni mwajiriwa amekua hana shukrani kwa yote nayoyafanya, hatoi mchango wowote katika familia pamoja na kuwa na kazi, pesa zake ni kujipamba, kuhudumia Gari lake, nguo Mpya kila siku na kadhalika, pamoja na ukweli kuwa mm ndie kichwa lakini nahitaji kusaidiwa kwa kuwa sina kazi, nachofanya nikuamka asubuhi na kwenda town yote yatajulikana huko, kwa msaada Wa washikaji napata dili ndogo ndogo nimeweza kumudu mahitaji yote ya familia, chakula, electricity bill, water bill, ada za watoto na mengine mengi for the past three years,

Kuna siku Rafiki Wa wife aliniomba maongezi, akaniuliza umefikia wapi ktk kutafuta kazi, nikajibu naendelea kutafuta, lakini hata hivyo home hakuna kinachokosekana, natimiza mahitaji yote yanayotakiwa kwa shughuli nazopata, akashangaa sana, akasema mbona mkeo anakuzungumza vibaya kwenye ma group yetu ya marafiki!!! Anasema hufanyi chochote umekua ni kama gunia hadi ubebwe
Niliumia sana, yule Dada aliniambia kejeli nyingi sana anazozungumza wife ambazo pia nimeshazisikia Mara kadhaa kwa ndugu Wa karibu

Nimesikitika kwa sababu yote hayo si ya kweli, juzi nimefungua Duka Mtaani kwetu baada ya kudunduliza sana, cha kushangaza wife hakupenda kabisa idea hiyo, akidai namdhalilisha yeye na familia kwa kuuza kibandani, anakiita kibanda, kwamba watu walizoea kuniona natoka ndani ya Gari na tai na Gari sasa nauza kibanda, eti bora ningetafuta sehemu ya mbali
Ukweli ni kuwa nataka nijue mapato ya siku na biashara inavyokua ndipo nimuache mtu

Siku hiyo nilimpa kipigo kizito sana, kwa majibizano hayo baada ya kauli za kuudhi, tangu kuondoka kazini 2012 nimejiepusha kuwa mzigo kwa mwenzangu kwa kuondoka alfajiri na kurudi usiku, kama ningekua nimemuachia majukum ya kifamilia yy hapo angeweza kulalamika, kama huduma hazifanani na wakati ule nipo kazini hilo ni suala lingine na ziada sio basic need

Sijawahi kumsumbua wife hata nilipokua kazini, sijawahi kuwa na mchepuko wala nini, sasa iweje yeye ashindwe kuwa na utu
Inafikia pahala watoto wanakula mezani anawaambia kuwa kuleni tu hayo majani siku baba yenu akiwa tajiri mtakula kuku, wakati Jana yake watoto wamekula kuku au nyama, anawajengea nini hawa watoto dhidi yangu? Halaf yy hata kubeba nusu kilo ya nyama hamna

Kumbe wanawake wanaweza kubadilika kiasi hiki kama Mume umepatwa na matatizo!!!!

Siku wakija wageni wake kutoka kutoka upareni ndipo atanunua mazagazaga kibao waweze kula vizuri, wakija Wa kwangu hajishugulishi na chochote, hadi mgeni anashtuka kuna tatizo ndani ya familia

Sasa Basi nimechoka na hali hii, nimeghafilika sana, natamani sana Rafiki Wa wife ndio angekua mke wangu, ana Upendo na Mimi, kwa kujua hali yangu amekua akinitumia hadi fedha kwa simu hata bila kuhitaji, nikimwambia sikua nahitaji fedha anasema chukua tu shemeji najua hali yako,
Ni bahati mbaya tu alifiwa na mumewe lakini ni mtu mwenye kunijali sana,
Mama yangu mzazi alikuja hapa kwa operation huyu shemeji yangu alizunguka na na mama muhimbili wiki nzima na alitumia pesa zake hadi mwisho, yy anafanya kazi hapo hospitalini, wakati huo wife hakujishugulisha kabisa alikua akisema Rafiki yake atafanya kila kitu hapo hospital

Nimefikia mwisho, nitafanya maamuzi magumu sana

Sijawahi kuwa na gubu wala kinyongo, maana mm ni mchakarikaji, sijawahi kuomba mtu hela natafuta mwenyewe, huku naendelea kushughulikia suala la kazi, lakini hata kama sikupata nitakomaa huku kwa business hadi nitoke, masikitiko yangu ni kwa huyu mke wangu ambae hanipi support

Kumbe ndio maana watu waliopata matatizo kazini na kusota sana siku wakifanikiwa maisha tena wanawaacha wake zao na jamii inaanza kuwalaumu kwamba wamekimbia familia zao baada ya kupata mafanikio tena, kumbe hawaelewi kuwa mtu unaamua kumuacha mke ukikumbuka matendo, manyanyaso, Maneno, kejeli, masimango na dharau wakati ukiwa juu ya mawe

Najua nitafanya nini, naomba nisilaumiwe



mtoa mada pole sana kwa yanayokukuta. hiyo ndio ndoa sasa inaanza kukomaa.

kuna mdau ameweka comment ya ukabila hapo juu mpuuzee tabia ni tabia tu.

Kuwa makini sana na maneno ya watu hasa wanawake wanapokueleza jambo kuhusu mkeo, wanawake asili yetu tuna kijiba cha roho tena haswaa hatupendi kwenye group mmoja wetu awe na familia yenye furaha kuzidi wenzie kuna kitu kinawaumaga wengi nakuanza kuwagombanisha ( note hii)

huyo mkeo ishi naye kwa akili,endelea kupigana na maisha yako na kibanda chako, akiongea maneno ya kejeli jifanye huoni wala husikii mwache ale hela zake aoteshe tumbo.

iko siku hyo biashara yako itakua kubwa na kazi utapata hiyo ndo itakuwa adhabu yake maana, hebu kuwa busy na mambo yakulea familia yako jifanye unaishi na chizi utakuja kuleta mrejesho humu dawa ya mwanamke mwenye kiburi mbona ndogo nyamaza kama umeweka maji mdomono.

habari yakuchepuka acha kabisaaa hyo ndo itakupoteza makukuchizisha kabisa maana siku umeishiwa mchepuko utakuchana makavi utajuta
 
Duuuhh, pole sana Kaka. Wakati mwingine mwamuzi sahihi huhitaji ndani ya Muda muafaka. Kwa kuwa kuna uamuzi tayari umeufanya basi fanya ndani ya Muda muafaka.
 
mtoa mada pole sana kwa yanayokukuta. hiyo ndio ndoa sasa inaanza kukomaa.

kuna mdau ameweka comment ya ukabila hapo juu mpuuzee tabia ni tabia tu.

Kuwa makini sana na maneno ya watu hasa wanawake wanapokueleza jambo kuhusu mkeo, wanawake asili yetu tuna kijiba cha roho tena haswaa hatupendi kwenye group mmoja wetu awe na familia yenye furaha kuzidi wenzie kuna kitu kinawaumaga wengi nakuanza kuwagombanisha ( note hii)

huyo mkeo ishi naye kwa akili,endelea kupigana na maisha yako na kibanda chako, akiongea maneno ya kejeli jifanye huoni wala husikii mwache ale hela zake aoteshe tumbo.

iko siku hyo biashara yako itakua kubwa na kazi utapata hiyo ndo itakuwa adhabu yake maana, hebu kuwa busy na mambo yakulea familia yako jifanye unaishi na chizi utakuja kuleta mrejesho humu dawa ya mwanamke mwenye kiburi mbona ndogo nyamaza kama umeweka maji mdomono.

habari yakuchepuka acha kabisaaa hyo ndo itakupoteza makukuchizisha kabisa maana siku umeishiwa mchepuko utakuchana makavi utajuta

Mkuu kuna maumivu na maumivu,kuhusu kuwa na mtu hiyo sijui but nyongo ikishapasuka ogopa sana! Halafu jua kavumilia kiasi since 2012?! Mi naona afanye maamuzi yenye tija ila asiwe na huyo mwanamke anayempoza people always take things for granted!
 
wanawake ndo walivo... kama umemuoa ukiwa tajiri halafu ukaja kuporomoka ni tatizo kubwa sana. Ndo mana nasapoti ile classical idea ya kuoa angali unaanza maisha ukiwa chini kabisa ili mke akuzoe katika hali ya chini kabisa.
 
Back
Top Bottom