Hivi kwanini kila ninachokifanya mke wangu haridhiki?

Pole sana ndugu...lakini ukweli ni kuwa 'hakuna mke hapo'!
 
Hio ndoa yako ni kama mkataba wa kazi serikalini,watu full kuzembea tu na hawaguswi...
Ushauri wangu ni hivi,just man up na kuhusu kuvumilia upuuzi wa mwanamke sio jambo rahisi,sometimes kumu ignore huwa inasaidiaga and if i were me ningezungumza nae juu ya itikadi zake za kishamba na kumueleza consequences zinazoweza kutokea kama akiendelea kunipuuza.Mwanaume heshima bhana na isitoshe una watoto nae kabisa,Yeye kama anadhani hilo la kukuheshimu bila shuruti litakuwa mtihani basi naye ajiandae kutoheshimiwa kwa we kupiga pini tu mpaka atapojirekebisha.Mchepuko huwa sio kitu kizuri ila kwa hali ulionayo sasa hakika unauhitaji sana uwe kama anti-depressant yako ili uendele kupambana na life,mind you asiwe yule shemeji yako anaekusaidia maana ukishamgonya utatengeneza deni na uhasama mkubwa nikimaanisha misaada hutaipata tena bila kumgusa mara kwa mara na pia mkeo akijua ndio itakuwa tiketi ya kuvunjia ndoa!
umeanza vizuuuri ukamalizia vibaya. Huyu keshasema toka ameoa hajawahi kuchepuka. Kwa nini unamshauri aanze sasa? Hakuna siku mchepuko umewahi kuwa suluhisho. Kama ni anti-depressant si aende muhimbili akapewe? Unadhani kuna mchepuko unapenda mwanaume mwenye kipato cha kubahatisha? Labda kama huo mchepuko una hela na ukishamtumia jamaa utammwaga bila huruma halafu atarudi kwa mkewe ambaye atakuwa hajabadilika tabia yake ya dharau au akajikuta anaimba "ahera hakuendeki, dunia haikaliki, nimepatwa na mfadhaikooo....".
 
Wanawake wengi huficha tabia zao. Akikuchoka ndo huonyesha vizuri rangi zake. Fanya maamuzi magumu ila waambie watoto sababu ya hayo maamuzi hata kwa lugha rahisi. Ili hata wakijazwa ujinga na mama yao wawe wanajua nini kinaendelea. Simama kama mwanamme fanya maamuzi yatakayo kufanya uishi kwa furaha sio kunung'unika na moyo uliopondeka.
 
aisee pole sana mkuu tena sana... wengi wameishakushauri mi ntakukumbuka tu kwenye maombi...
pia nawe usisahau kumuombea huyo mke... ni nguvu za shetani tu hizo..

Mungu aniepushe mbali na wanawake wa tabia kama hizi..

Aamiin.
 
Mkuu we piga kimya tu kama humuoni huyo mkeo,
ila nakushauri fungua account bank ambayo itakuwa "freezed"
kisha anza kuwa wekea hao wanao pesa kwajili ya mahitaji yao
ya hapo baadae na hata ada zao ....kwani yeye anadhani anakukomoa
wewe kwa sababu ya watoto mlionao.
Ila zidisha juhudi na maarifa katika kazi, dedication " maisha ni mapambano" by less wanyika.
 
Jamani pole kakaangu ila nakuomba xanaxana utafte sala ya mtakatifu Antoni ufunge na uombe ili upate kazi ndani ya mwezi mungu atajibu maombi yako
 
umeanza vizuuuri ukamalizia vibaya. Huyu keshasema toka ameoa hajawahi kuchepuka. Kwa nini unamshauri aanze sasa? Hakuna siku mchepuko umewahi kuwa suluhisho. Kama ni anti-depressant si aende muhimbili akapewe? Unadhani kuna mchepuko unapenda mwanaume mwenye kipato cha kubahatisha? Labda kama huo mchepuko una hela na ukishamtumia jamaa utammwaga bila huruma halafu atarudi kwa mkewe ambaye atakuwa hajabadilika tabia yake ya dharau au akajikuta anaimba "ahera hakuendeki, dunia haikaliki, nimepatwa na mfadhaikooo....".

Ni kweli mchepuko hausaidii bali ataongeza stress na pengine kupanua family huku na uchumi nao ni wa kubabaisha.

Ushauri wa FaizaFoxy kuhusu kumridhisha kitandani nao hauna maana kwa sababu tayari mama keshadharau kila afanyalo mume. Dawa ni huyo jamaa kujijenga kiuchumi na kwa sasa ni kum ignore.( NI MATESO MAKUBWA MNO ZAIDI YA JELA)
 
Pole sana ndugu yangu. Majaribu tumeumbiwa wanadamu. Ziba masiko endeleza hicho kinachohitwa kibanda kuna siku Mungu atakuwezesha nawe maisha yatanyooka. Husiache kumuomba Mungu azidi kukupigania katika kutafuta kwako.
 
Wenye matatizo wapo na wema wapo pia. Ingawa siku zote wema hauvumi sana kama ubaya unavyovuma. It's too much kwa jinsi wanawake tunavyochukuliwa, as is hatuna jema hata moja. Mbona wanaume wengi na nyie mkipataga hela kidogo tu akili zinachanganyikiwa hadi kuona wake zenu takataka? Ila akifanya mwanamke basi inakuwa wanawake wote ni wapumbavu. Not Rait kwa kweli, hata Mungu hapendi looh

Jina na maandishi yako yanaonesha ni Kati ya wanawake wachache wenye maono but wanawake wengi ni changamoto dadangu, unatamani kuwa naye ila ukifikiria kuwa unaenda kuishi naye for the rest of your life unashindwa hata kumtambulisha Kwa wazazi wetu, be blessed dada, i believe your man is proud of you.
 
Duh! kweli mama aliniambia mwanangu kuwa uyaonee...
Kumbe sio maghorofa na magarii ni nikuwe niyaone mambo ya duniaaa...

UKIITWA BABA LAZIMA UBABAIKE
jitume kwaajili ya wanao na huyo rfk wa mkeo naye mmmh mi sisemi ila sijuui!
 
mwenyezi mungu alipowaalaani Adam na Hawa (Eve) alisema, adam utakula kwa jasho na Hawa, utazaa kwa uchungu. Hakuna mahali alisema Adam ule kwa jasho na Hawa ule kwa jasho na kuzaa kwa uchungu. Ni nature. Mwanamme atamlisha na kumvisha mke wake miaka yote kama hana income na wala usisikie vibaya, you feel ni jukumu lako, lakini inapokua kinyume kua sasa mwanamme huna income unataka msaada wa mke, ni vigumu kuupata kama unavyotarajia maana si jukumu la mwanamke kufanya hivyo. ukibahatika kupata mwenye moyo wa pekee atasaidia lakini kwa kiwango Fulani, then atachoka. ukipata mwenye roho ya mkeo hatatoa msaada wowote maana si jukumu lake. Pole sana kwa hii hali, naomba tu ulijue hili kua wanawake hawakuumbwa kutunza familia hasa kama kuna mtu mwenye jukumu hilo. nageuka kwa mjane. kua mwangalifu nae. umeshasema ni mjane, kumbuka kua ana take advantage ya matatizo yako kupata faraja. anaweza pia asiwe hivyo unavyodhania endapo utaamua kua nae, hivyo jihadhari usijiongezee frustration nyingine.
 
Mkuu usipime kumreplace mkeo na rafiki wa mkeo. Mvumilivu hula mbivu vile umeanza biashara Mungu atakupigania. Dharau zake zisikutishe kuwa na hekima muhimu ni watoto. Watoto wataona ukweli mbele ya safari. Huyu shemeji sijui rafiki wa mkeo usijidanganye ni informer atakuharibia ndoa hakuna ndoa takatifu vumilia bana!
 
Ni kweli mchepuko hausaidii bali ataongeza stress na pengine kupanua family huku na uchumi nao ni wa kubabaisha.

Ushauri wa FaizaFoxy kuhusu kumridhisha kitandani nao hauna maana kwa sababu tayari mama keshadharau kila afanyalo mume. Dawa ni huyo jamaa kujijenga kiuchumi na kwa sasa ni kum ignore.( NI MATESO MAKUBWA MNO ZAIDI YA JELA)


Wacha Kufananisha hayo Mateso na Jela aafiru.....
 
Kuna vitu umeficha, mwanamke wa hivyo hata unyumba hakupi kwa sababu anaona wewe sio wa level yake, hana hamu na wewe, huna mvuto, anaona unamsumbua etc. Tatizo ni moja, bado huna ground za kumwacha. Kikubwa mambo yako yakiwa safi na wewe mpuuze. Tafuta nyumba ndogo nzuri mahali awe anakutoa stress. Basi

Nakubaliana na wewe
 

Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom