Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 5,557
- 8,195
Watanzania tulio wengi tumeshindwa kabisa kufanya biashara ya pamoja kama wanafamilia au watu wa ukoo mmoja kwanini?
Tofauti na jamii za kiarabu, kihindi na hata familia nyingi za kizungu hudumisha tamaduni hii ya biashara za kifamilia. Yani kutoka kwa muasisi (hasa alieleta mageuzi ya kiuchumi) familia huendeleza biashara hizo na kurithishana kizazi hadi kizazi bila kuuza wala kugawanywa kwa warithi. Hii husaidia familia hizi kutoanza kutoka mavumbini kama tulivyo wengi wetu hapa tz,
Familia nyingi za kitanzania baada ya kufa muasisi awe Baba au mama wa familia watoto huanza kugombania Mali na kugawana assets au kuziuza kabisa na kugawana hela. Yani hawawezi kuthubutu kutunza na kuendeleza alipoishia muasisi na kufanya biashara hizo au uwekezaji kuwa mkubwa kwa ajili ya kunufaisha kizazi kilichopo na kuandaa warithi kwa ajili ya vizazi vingine
Wengi wa walioacha uwekezaji mkubwa mali zao huishia kuuzwa au kugawanywa au tena kama kaacha wosia mali zisiuzwe basi watoto hawawezi kuendeleza kutoka moja kwenda mbili na tatu bali watabweteka na macho yote yatakuwa kwenye mirathi hiyo iwafanyie kila kitu wala hawatashughulika kuitunza wala kuiendeleza na kuwekeza zaidi mwisho wa siku wanaishia kugombana na kesi zisizoisha mahakamani
Je, elimu ndio tatizo?
Je wewe kama mwanafamilia unaona nini kikwazo?
Je ni kweli biashara za kifamilia hazina tija kwa familia za kitanzania?
Kama ipo tija nini kifanyike?
Umeweka mikakati gani kuhakikisha kizazi chako kinaendeleza unachokifanya?
Karibu tujadili.