Hivi kwanini cheo cha DC na DED vimeshuka thamani?

Hivi kwanini cheo cha DC na DED vimeshuka thamani?

Tatizo ni wanaopewa hizo nafasi baadhi kukosa
1. Ubunifu
2. Kuwa watumishi wa mishahara kama kada zingine
3. Kutokuwa wawajibikaji wa umma/watu, kuna viongoz wanajitenga sana na wananchi, hawaonekani kabisa.
4. Uwoga wa kuthubutu, we DED anaogopa kuanzisha mradi wa kugusa umma wa hata milion 10 tu anaziona nyingi na hana tija ya kufanya, tija ya mradi mpaka itoke serikali kuu au kwenye kichwa chake.
5. Kusahau kuwa uhuru una majukumu.
6. Kuwa na genge la wajinga.
Unajua kwenye siasa wajinga wanasikilizwa kuliko welevu, toka na wazo lako nenda kwa baadh ya mwanasiasa, we unampa wazo lipo kwenye karatasi ataona kama uchafu tu, ila kapige kikumbo mtu utaonekana ni bora.
7. Hawana watu wa kuwasemea. DED na DC hajui media hata afanye nini hawez kuonekana, atakuwa gizani.
8. Hawana uwezo wa kushawishi watu kwa hoja. Kuna vikao unakuta havina watu kabisa, wanadharau kuwa hawana jipya, hili ni tusi.
9. Daraja baya la kiongozi wa kijiji na wilaya. Ushirikishwaji maeneo mengine ni changamoto, uhusiano bora wa kiongoz wa juu na chini ni hafifu.
Kwa haya huwezi kuona nguvu ya hivyo vyeo ni kama "ceremonies title".
Kuna DC na DED wanaheshimika sana na kila mtu anamtambua tena kwa jina lake, yote ni uwajibikaji na kuwa karibu na matatizo ya umma.
 
cheo cha Ded kiliharibiwa pale chama kilipoamua kuwageuza hawa kuwa makatibu wenezi wa chama.Unajua DED siyo mtu mdogo,anasimamia maendeleo ya wilaya kitalaamu.Ila hawa madeni sorry ma-DED wote walipata teuzi baada ya kugombea nafasi za ubunge na kura kutotosha.hawana uzoefu ni system za halmashauri.zamani Maded walilikuwa wanapandishwa kutoka nafasi labda za maafisa mipango wa halamashauri walio iva kabisa.wanaojua kuoperate system za halmashauri. sasa wamejikuta wengi wao wakipata udedi wanaendelea na azma yao kutaka kugombea msimu ujao
Ndio utaratibu unavyotakiwa kuwa DED lazima atokane na Mkuu wa Idara sio kutolewa mtaani.
Kitendo Cha kuwatoa mitaani au junior officers kimefanya Halmashauri nyingi kushindwa kuendesheka maana mteule anakuwa anahisi kudharauriwa na Wakuu wa Idara.
 
Matatizo yote haya yalianza na Kikwete bafaye Magufuli ndio akaharibu kabisa,sasa Mtumishi gani wa Serikali mwenye akili timamu asome for 12 years afu aje aongozwe na MTU kama Jokate-slay Queen.

U-DED na DC ulikuwa imara kipindi cha Mkapa na Kikwete kidogo.
Imewakatisha tamaa sana watumishi
 
Zamani viongozi hao wote walikuwa wanafanyiwa vetting hata kama alipewa kama zawadi. Ilipotokea kiongozi huyo ameboronga system inaumiza akili kabisa kuwa nini kimetokea! Vyeo hivyo vilikuwa vya heshima sana kwamba vinatoa taswira ya Rais. Mtu ameshajitambulisha na kukutwa na kitambulisho kuwa anatokea kitengo, ananyanyasa watu baa, analala hotelini halipii huduma, kesho anateuliwa kuwa DC!
 
Hivyo vyeo vimegeuka fadhila za kisiasa baada ya uchaguzi mkuu...
maDC na maDED, wakati wa uchaguzi wanashindana kwa uovu wa kuiva kura au kulazimisha kutangazwa mbunge mwanaCCM aliyeshindwa uchaguzi.

Na wao wanaamini kuwa jukumu lao kuu na la kwanza ni wajati wa uchaguzi kuhakikisha mgombea wa CCM anatangazwa mshindi.

Wanazingatia sana maelekezo ya marehemu, 'gari nikuoe mimi, mafuta nikuoe mimi, posho ya kwenda kusimamia uchaguzi nikuoe mimi, halafu unaebda kumtangaza mpinzani ameshinda, una akili wewe!'

Ukizingatia wengi wateuliwa kwenye nafasi hizi ni watu ambao ni jobless, wanatenda chochote alimradi kitendo hicho kitawafanya wabakie kwenye hizo nafasi.

Kwa ujumla, kwa sasa hivi, hawa watu mchango wao kwa maendeleo ya nchi, ni negligible. DED mmoja nilienda ofisini kwake, baada ya kumaliza kujadili kilichonipeleka jwake, mwishoni akaanza kuniomba mchango wa ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa CCM. Nilimwambia tu kuwa mwongozo wa Serikali kwa wawekezaji wote ni kuwa wasishiriki kwenye shughuli za vyama vya siasa. Akasema, unachosema ni kweli, lakini tunafanya kazi katika mazingira magumu, viongozi hawa CCM wanayajua hayo lakini wanatubebesha mzigo watendaji.
 
uteuzi umejaa kujuana na vimemo hakuna vetting wala weledi wa kutosha kwenye teuzi ukiwa kada tu wa CCM possibility ya kupata U DC /DED ni 100% ukiwa na watu wazuri wa kulipigania jina lako yani HOVYO KABISA
 
Hivi vyeo n bora vifutwe kabisa kwani hawa watu hawana msaada wowote kwa Taifa badala yake ni mizigo kwa walipa kodi!
Tz bila katiba mpya hakuna lolote la maana!
 
habari za mchana,

Kichwa cha habari cha jieleza hapo juu, hivi kwanini vyeo hivi vimekuwa vya kawaida sanaa tofauti na zamani?

Zamani watu wenye vyao hivi walikuwa watu wanaoheshimika sanaa katika jamii, yaani DC akitoa order si kwa watumishi au wananchi lazima ifuatwe mara moja lakini siku hizi ni kinyume chake.

Leo nilikuwa nafuatilia kikao cha Waziri Mkuu huku Tandahamba, yanii DC anatoa maelekezo hakuna anaejali; si DED wala watumishi wa chini yake hadi Waziri Mkuu akalikeme hilo.

Pia kuna mahala nimeona wananchi kwenye mkutano wanampa maneno ya kashfa DED kiongozi hadi RC wake akaamua kuingilia kati ndo wananchi wakatulia, tatizo nini? Matukio ni mengi sanaa hiyo ni michache tu.

Mifumo imechoka au haifanyi kazi kabisa.

NJOO TUJADILI.
Per Diem allowance ndo muhimu
 
Back
Top Bottom