Hivi kwanini Africa isiungane tuwe moja? Mbona litakuwa jambo zuri mno!

Hilo swala la kuungana hakuna alieliweza ktk marais wote wa afrika kasoro MUAMAR GADDAFI
Aliweza kwa asilimia 60 kuhamasisha marais wa Africa kuungana pamoja
Hapo hapo ndio wazungu wakajua huyu anataka kuwa KING OF AFRICA
Wakaanzisha fitna kwa wananchi wa LIBYA ili wampidue tu GADAFI hadi walifanikisha
Leo LIBYA wanalia machozi ya damu kwa majuto ya kumuua Gaddafi Kutokana na mateso,njaa na shida zinazowakabili wananchi wa LIBYA
 
Hili hata Nyerere mwenyewe alilikiri, akiwa Ghana na hata kwenye makala zake. Kwamba Wazo la Kwame japo lilikuwa na changamoto nyingi lakini lilifaa zaidi.
SINA UHAKIKA KAMA AMEWAHI KUKIRI.... hapana.
 
Leo hii mbali na kwamba Tanzania tuna shida katika mfumo tawala ila bado kuna ahueni, huyu mtanzania ambaye amezoea kuamka asubuhi akaenda kuuza dagaa wake akatoka jioni akapitia kijiweni akapata story mbili tatu akaingia ndani akakusanyika na familia yake akala akalala bila bughudha , umuunganishe na msomalia, mnaijeria mkongo, methiopia, mrundi, mlibya, mtu wa afrika ya kati nk ambao wengi kukicha haujui kama giza litaingia akiwa salama, akitoka nje hajui kama atarejea ndani tena, kwakweli jaribu kuwatafakari viongizi kama akina Museveni, Nkurunziza, Mugabe,,Salvakiir, Omary Bashir, Riekmachar, Kagame, Kabila, uwaweke meza moja na akina Kikwete, Shein , Kenyata, Magufuli na akina Mwinyi? Kwakweli kwa upande wa Afrika kuungana ni kuleta dhahama tupu kwa Waafrika tulio wengi, wacha tubaki hivyo tu labda vizazi vijavyo kama vitakuwa vimejitambua itafaa sana ila si kwa kizazi hiki.
 
Hebu nielezee kidogo kuhusu hiyo ibada asilia ya kiafrika, mm nachojua ibada ya waafrika ilikua kuabudu milima, miti, matambiko na kafara mbalimbali, miiko ya kijinga kama kuua mapacha, arubino, Etc.
Hebu nielezee kuhusu hiyo dini asilia mama..
Dini ni misingi, mengine yote hubadilika kutokana na mazingira na nyakati. Sijawahi kumuona Mmasai albino, ila siwabezi kwa hilo, najua huwa wanawatoa kafara. Sio dhambi kwa jinsi mifumo yao ya kimaisha ilivyokuwa. Sawa na Bible na Tourati ya kale ilivyo wafanya waliokuwa na maradhi ya ukoma.

Nimesema, dini ni misingi, viambata vinginevyo hubadilika kulingana na nyakati. Unadhani utumwa ulikuwa ukionekana kuwa ni kinyume na Mungu? Basi itafute misingi ya kiafrika ktk Ubuntu, utu, dogons, na kwenye tamaduni mbalimbali, Ukwele, Uzaramo nk. Kuna kanuni nzuri kuzipitita hata za hizi dini mpya.
 
Hilo swala la kuungana hakuna alieliweza ktk marais wote wa afrika kasoro MUAMAR GADDAFI
Aliweza kwa asilimia 60 kuhamasisha marais wa Africa kuungana pamoja
Hapo hapo ndio wazungu wakajua huyu anataka kuwa KING OF AFRICA
Wakaanzisha fitna kwa wananchi wa LIBYA ili wampidue tu GADAFI hadi walifanikisha
Leo LIBYA wanalia machozi ya damu kwa majuto ya kumuua Gaddafi Kutokana na mateso,njaa na shida zinazowakabili wananchi wa LIBYA
Gadaff siye mwafrika pekee, hata sisi ni wana wa Afrika. Tuanze sisi hili vuguvugu, tena lianze kwa Uzi huu na lienee kote Afrika. Umajinuni wa kiafrika urejee.
 
Kwani nikiendelea na dini yangu hii tatizo lipo wapiii..
Dini ni misingi, mengine yote hubadilika kutokana na mazingira na nyakati. Sijawahi kumuona Mmasai albino, ila siwabezi kwa hilo, najua huwa wanawatoa kafara. Sio dhambi kwa jinsi mifumo yao ya kimaisha ilivyokuwa. Sawa na Bible na Tourati ya kale ilivyo wafanya waliokuwa na maradhi ya ukoma.

Nimesema, dini ni misingi, viambata vinginevyo hubadilika kulingana na nyakati. Unadhani utumwa ulikuwa ukionekana kuwa ni kinyume na Mungu? Basi itafute misingi ya kiafrika ktk Ubuntu, utu, dogons, na kwenye tamaduni mbalimbali, Ukwele, Uzaramo nk. Kuna kanuni nzuri kuzipitita hata za hizi dini mpya.
 
Nshakupa like yako.

1.Tatizo wazungu hawataki tuungane.

2.uchu wa madaraka/ubinafsi

3. Utegemezi/

4. Ujinga

5. Mavita wenyewe kwa wenyewe
Hasa kwenye vita, ndio huwa nauona umbumbumbu wetu. Naamini sote tunajua kwamba, hivi vita vinavyoendelea Afrika, si kwa manufaa ya wana Afrika bali mataifa makubwa ya nje. Sasa Kwanini tusijifunue tukaviacha kwa haraka?

Hainiingii akilini UN kuleta walinda amani, wakati silaha zinatengenezwa, zinaingizwa kupitia mipaka yetu, kuniambia hazijulikani zinakotoka na namna zinavyoingizwa Hainiingii kabisa.
 
Niliwahi sikia wakina Kwame Nkurumah na J.K.Nyerere walikuwa na hii idea wakapotea bila ya kutimiza ndoto zao..
 
Leo hii mbali na kwamba Tanzania tuna shida katika mfumo tawala ila bado kuna ahueni, huyu mtanzania ambaye amezoea kuamka asubuhi akaenda kuuza dagaa wake akatoka jioni akapitia kijiweni akapata story mbili tatu akaingia ndani akakusanyika na familia yake akala akalala bila bughudha , umuunganishe na msomalia, mnaijeria mkongo, methiopia, mrundi, mlibya, mtu wa afrika ya kati nk ambao wengi kukicha haujui kama giza litaingia akiwa salama, akitoka nje hajui kama atarejea ndani tena, kwakweli jaribu kuwatafakari viongizi kama akina Museveni, Nkurunziza, Mugabe,,Salvakiir, Omary Bashir, Riekmachar, Kagame, Kabila, uwaweke meza moja na akina Kikwete, Shein , Kenyata, Magufuli na akina Mwinyi? Kwakweli kwa upande wa Afrika kuungana ni kuleta dhahama tupu kwa Waafrika tulio wengi, wacha tubaki hivyo tu labda vizazi vijavyo kama vitakuwa vimejitambua itafaa sana ila si kwa kizazi hiki.
Sio lazima lije lifanikiwe leo au kesho, na inawezekana lisifanyike hata kwa miaka mia ijayo, au lisije kufanikiwa kabisa hadi kiama, kama kitakuwepo, lakini la msingi ni kulianzisha,tena si kesho bali sasa. Si vyema kushindwa kabla ya kuanza.
 
Kwani nikiendelea na dini yangu hii tatizo lipo wapiii..
Tatizo dini yako hiyo haituunganishi bali inatutenganisha. Lakini lililo kuu, inatufanya tuwe watumwa wa kifkra zaidi. Unyonge wa mwafrika umejengwa na silaha kuu mbili za kikoloni, elimu na dini. Tumeshindwa kuzitumia kujiendeleza nazo.
 
Back
Top Bottom