Hivi kuna umuhimu gani wa kuvaa pete ya ndoa kidoleni muda wote?

pete ina umuhimu wake, kama umeoa au kuolewa kwa bila shinikizo huwezi kuogopa kuivaa hata mara moja. ila kam umeolewa/oa kwa push ya watu wengine then u will feel ashamed kuwa nayo mkononi.
 
Unajua watu wanasahau kuwa binadamu ni kiumbe dahifu na udhaifu unazidiana viwango. Lakini bado kuna wengi sana wanaoheshimu ndoa ZA WATU na hawapendi kubeba dhambi ya kuwa chanzo cha kuvunja ndoa. Ndio maana nasema mimi NK ningekuwa sivai pete ningekuwa natongozwa na wanaume wengi sana; lakini pete yangu imesaidia kuepuka hivi vishawishi kwani wengi sana wanaogopa wake za watu. Na si rahisi mtu kukuuliza umeolewa au la ila akiona pete anapata jibu. Sawa uaminifu uko rohoni mwa mtu; lakini mazingira yanachangia watu kukosa uaminifu. Pete inafukuza vishawishi na anayekufata huku anaona pete jua hilo ni bazazi sugu.
 
hata kama ni ya wazungu, alilivaa la nini mbele za watu tena kwa mbwembwe afu saa hivi ajidai halitaki?

Kwa nini hakusema hataki from day 1?

Ukishaingingia kwenye 'cult' yeyete ukakubali katiba inayoongoza cult hiyo then vifungu vyote vya katiba hiyo vinakuhusu.
Huwezi kusema eti kifungu 2.1.a ni cha kihindi mie myunani, ndoa za sasa wizi mtupu

Tofautisha mila, desturi, tamaduni na mazoea wewe then usiongee kama unaongea na mwanao, naweza kukuliza weyee!!
 
ukiwa ndani ya nyumba then usipovaa sio mbaya bt ukitoka nje ya nyumba ni vizuri uwe nayo
 
ukiivua na mkeo akaamua kuivua yake usilalamike.....

Uliinunua ya nini kama huoensi kuivaa?
 
Pete yako ikizoea kidoleni hutaona shida maana itakuwa sehemu ya kidole na siku ukiivua utasikia tofauti. Ni vizuri kuivaa muda wote maana inakutambulisha kuwa tayari una mtu wako na umefunga nae ndoa. Kuna rafiki yangu anapenda sana totozi lakini ananiambia kwa jinsi anavyoheshimu wake za watu hapendi kabisa kutembea na mwanamke ambaye dhahiri ni mke wa mtu na ana pete ya ndoa hivyo pia wapo wadada ambao wanaheshimu waume za watu na watakutambua kwa pete kidoleni.
 
mh! Mimi nilikuwa nampenda mke wangu kizamani (kwa matendo.) kumbe siku hizi upendo huonyeshwa kwa ishara? Aksante kwa kuni-up date.

kwenye imani ya kikristo ndo wanavosemaga wakifungishwa ndoa....pokea pete hii..... ishara ya mapenzi yangu kwako....
 
Kasome vitabu vya mwenyezi MUNGU ili ujue kuvaa pete ni ishara ya upendo kwenye ndoa yako au upo ktk giza la kushikilia miungu ya shetani ktk ndoa yako? Soma Mwnzo 35:1-4, Isaya 3:16-20,Wafalme wa pili 9:30,Petro wa kwanza 3:3-4. Ukimaliza kusoma ukielewa vzuri wambie na wenzako mnaovaa pete mkiashiria upendo wa ndoa zenu, kuwa mungu hana shida na hizo pete, pete ya ndoa yako ni kushika amri kumi za MUNGU mioyoni mwenu. Kasome kitabu cha kutoka 20:1-21. Hiyo ndo pete imara ya ndoa yako.
 
pete inaonyesha kuwa tayari hupatikani, ukiwa hujavaa inamaanisha u are availabo, so kama ww ni mke wa mtu hujavaa nikikupiga sound utalalamika mie sina adabu?

wanawake na wanaume wenye ndoa vaeni pete zenu, ili mtupunguzie maswali "eti dada umeolewa?"
 
Jamaa yangu mmoja (mnyarwanda) aliwahi kunihadithia yeye ya kwake huwa anaivua kila anapocheza mechi za ugenini. Jamaa ni kiwembe ile mbaya na mke wake ni bomba sana. Nikamwambia kwanini usiivue kabisa akadai mke wake hakubali kabisa atoke nyumbani kwao bila kuvaa pete.

 
Last edited by a moderator:
Pete ina maana kama wachangiaji walivyosema aihitaji kurudia ila pete insaidia mtu kujiona anawajibu kwa familia yake, pia hata kama mtu anafanya kitu kibaya mbele za watu kwa kiasi ataona aibu hivyo kufanya ajifiche anapotaka kufanya mabaya.
 
Back
Top Bottom