Hivi kuna umuhimu gani wa kuvaa pete ya ndoa kidoleni muda wote? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna umuhimu gani wa kuvaa pete ya ndoa kidoleni muda wote?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mshawa, Jun 24, 2012.

 1. Mshawa

  Mshawa JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 711
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Tokea utotoni hadi sasa sijawahi kuvaa hata saa ya mkononi, ukiachilia cheni za shingoni, naona kama tabu, sasa tabu imekuja kuwa hii pete ya ndoa, nataka kuitoa kwa kuwa nahisi ni kama foreign body kwenye mwili wangu (irritant object) na mke wangu hataki niivue, je kuna ulazima wowote wa kuivaa muda wote?
  nawasilisha..
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,368
  Likes Received: 22,231
  Trophy Points: 280
  mi nisipovaa pete ya ndoa jongoo hapandi mtungi, sijui ndio limbwata lenyewe au ndio nimewekewa tego?
   
 3. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  heheeeeeee...
   
 4. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,298
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Nkem Owoh, you have to go to kafanchami to see papa. Your isupandege does not fu what? function??? that ring is wrong ha hahaa
   
 5. Mshawa

  Mshawa JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 711
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Kaaazi kwelikweli
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Unajua kuna dhana moja wanayoiamini kuwa usipovaa pete ya ndoa unataka kumcheat mkeo
  Wengine ni kuonyesha kwa wengine kuwa ni mtu ambaye ana mtu wake kashafunga ndoa
  Ila nadhani ni uamuzi wako tuu. Kuvaa au kutovaa pete hakumaanishi kuwa wewe humpendi au huithamini ndoa yako. Ndoa iko ndani ya moyo wako. Na ukiamua hata ukiwa na pete kidoleni unaweza kumcheat mkeo. So mkuu ni uamuzi wako kuamua kuvaa au kutovaa na hata usipovaa haimaniishi kuwa humpendi mkeo au unaisaliti ndoa yako
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hilo swali ni zuri sana kwa padri, mchungaji au shehe aliyekufungia ndoa yako mfuate muulize atakujibu ipasavyo pia hata mkeo atakuwa ana imani na wewe pindi utakapokua huivai atadhani teyeri ushaanza mambo ya vidum
   
 8. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hakuna kwa kweli, hii ni kwa wote wanandoa pia sidhani kama itakuwa rahisi hasa kwa wale wanaooa more than 1 sidhani kama inawezekana.
   
 9. N

  Nehondo JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pete ni ishara ya upendo kwa mwenzio
   
 10. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  WEWE KICHECHE, WAJUA PETE INAFANYA UOGOPWE NA TOTOs?? MWAMBIE NA SHEMEJI AIVUE ILI TUMUAPPROACH
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  kwa nini huukuikataa wakati anakuvalisha mbele za watu ukamwambia ni 'foreign/irritant object'?

  Mapozi mengine hayana hata maana unapanda bangi unataka uote mchicha, khah!
   
 12. k

  kisukari JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,762
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  wanaume wanaoishi pwani sio wote wanaovaa pete za ndoa.na kwa wake zao sio issue kabisa.mimi nikiwa na mume wangu,avae asivae nitaona sawa tu, ndugu zangu wengi wenye ndoa zao sioni pete kwenye vidole vyao.muhimu upendo uwepo basi
   
 13. kimweri Jr

  kimweri Jr Senior Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 131
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  PETE ni sawa na psycotherapy kwa wanandoa hasa kwa ulimwengu wa sasa japo ni kautaratibu ka tangu zamani. Unapovaa pete wengi wanajiaminisha kuwa ni ishara ya upendo, kinga ya ndoa na alama ya ukumbusho na utambulisho popote ulipo lakini huo siyo ukweli bali tiba ya kisaikolojia. Hayo yote niliyosema hayatekelezwi na uwepo wa pete bali utayari wa nafsi ya mtu. Mind ina ID, EGO NA SUPER EGO. Huko kuna memory, identity and emotion. Hakuna zaidi ya hayo kwenye pete.
   
 14. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Akah! kumbe usipovaa inamaana nyengine? mie naona sawa tuu.....
   
 15. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Haya mambo ni ya wazungu bana, na hii hapa ndo historia yake kwa ufupi tu: iko kwa kikoloni so nimeona itanichukua muda kutafsiri; ukiona ngumu iteme

  A wedding ring or wedding band is a metal ring indicating the wearer is married. Depending on the local culture, it is worn on the base of the right or the left ring finger. The custom of wearing such a ring has spread widely beyond its origin in Europe. Originally worn by wives only, wedding rings became customary for both husbands and wives during the 20th century.[SUP]
  [/SUP]
  Wedding ceremonies that reference rings
  • Church of England (1662 Book of Common Prayer) - "With this ring I thee wed, with my body I thee worship, and with all my worldly goods I thee endow: In the Name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost. Amen."[SUP][5][/SUP]
  • Jewish - "You are consecrated to me with this ring according to the law of Moses and Israel." - Said in Hebrew by the groom at an Orthodox Jewish wedding and by both the bride and groom at a Reform Jewish wedding[SUP][citation needed][/SUP]
  • Roman Catholic - "N., take this ring as a sign of my love and fidelity. In the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit."[SUP][6][/SUP]
  • Eastern Orthodox - "The servant of God (N.) is betrothed to the handmaid of God (N.), in the Name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen." - from the Eastern Orthodox Service of Betrothal, part of the Mysterion of Holy Matrimony ("crowning"), said three times while the Priest makes the Sign of the Cross with the bride's ring over the bridegroom's head, he then places the bride's ring on the groom's hand. The same words are said three times over the bride, reversing the names of the bride and groom, placing the groom's ring on the bride's hand. The rings are then exchanged three times (either by the priest or by the best man), so that the bride and the groom end up with their own rings.[SUP][citation needed][/SUP] In Eastern Orthodox tradition the wedding ring is worn on the right hand rather than the left.[SUP][7][/SUP]
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  bhikola, hata kama ni ya wazungu, alilivaa la nini mbele za watu tena kwa mbwembwe afu saa hivi ajidai halitaki?

  Kwa nini hakusema hataki from day 1?

  Ukishaingingia kwenye 'cult' yeyete ukakubali katiba inayoongoza cult hiyo then vifungu vyote vya katiba hiyo vinakuhusu.
  Huwezi kusema eti kifungu 2.1.a ni cha kihindi mie myunani, ndoa za sasa wizi mtupu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Pete ni ishara ya upendo na uaminifu.
  Yani nimeona heading ya hii thread nimefungua haraka nione kulikoni; kwani juzi kati kuna dada (wadogo zangu wa skuli) Mkenya aliniuliza NK kwa nini unavaa pete yako muda wote. Kwa kweli nilimwelewa vibaya kwa kuwa na yeye ni mke wa mtu na wote tuko ughaibuni. Nivue ili iweje. Nimeivaa kwa karibu miaka tisa na wala sijaona inaleta usumbufu wowote imeshakuwa part ya kidole changu.

  Pete kwa sisi wanawake inasaidia kufukuza wasumbufu na mashetani watu hasa kama sie wenye maumbo madogo kiasi mtu anaweza asijue kuwa ni mke wa mtu. Hata mie siwezi kumuelewa mtu aliye kwenye ndoa na anaona pete yake kuwa ni karaha; are you still available????
  Yule dada wa kikenya kwa kweli alinifanya ni conclude kuwa ni cheater maana baada ya kuniuliza hayo niligundua yeye havai pete yake na mumewe yuko Kenya; maana yake anajifanya yuko single.

  Mimi hata kuoga naoga nayo; haijawahi kutoka kwenye kidole toka nivalishwe kanisani. (niliwahi ivua kwa masaa lol. nilipogombana na hubby ili kumpa pressure; ila sikutoka ndani ilikuwa kwa masaa)

  Kuna kaka aliangusha pete yake akiwa ananawa mikono kazini alihangaika akasema wife wake hataamini kuwa hakuivua atende maovu. Ila ilikuwa loose na mambo ya sabuni ikateleza bila yeye kujua.

  Haya mambo ya kuzini na waume au wake za watu kwa excuse kuwa sikujua kama kaoa/ kaolewa yanachangiwa na wavua pete.

  Mume wangu hataki hata niongeze pete nyingine mkononi ili watu waone kabisa kuwa mimi ni mke wa mtu; maana yakijazana ni ngumu mtu ku notice.
   
 18. N

  Neylu JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ni vema ukavaa pete yako ili hata ukiamua kumuapproach mwanamke, aamue mwenyewe kukubali huku akijua wewe umeoa tayari.. Kuna wanaume wengine wanavua pete zao na kudanganya dada za watu kwamba hawajaoa.. Sasa kwa wale wenzangu na mie tunaoangalia pete inakula kwetu...
   
 19. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Na ikumbukwe kuwa pete ina maana kwa wakristu tu (correct me if am wrong) sasa ukisema watu wa pwani hawavai pete ni kwa sababu wengi ni waislamu. Kwa mwislamu ukiona amevaa pete eti ni ya ndoa jua anafanya kuiga tu; wao hawana kitu kama hicho.

  Tena kuna mtu alinambia mwanamme wa kiislamu hapaswi kuvaa mi gold? Sijuhi alikwa sahihi.

  Mimi nawashangaa wakristu ambao leo hii wanaona pete kero; wakatae toka kanisani kuwa mimi ndoa yangu haiitaji pete.

  Mfano mi nikikutana na ndugu/rafiki yangu akiwa hana pete yake ya harusi; nta conclude kuwa amesha divorce, sina haja hata ya kumuuliza.
   
 20. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,860
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  me naweza sema uaminifu na upendo upo moyoni mwa mtu binafsi. mara ngapi tunawaona watu wanacheat ilhali wana pete zao za ndoa vidoleni? nijuavyo pete ni ishara ya kuonesha umeshaoa / kuolewa na co ishara ya uaminifu na upendo. nawashangaa sana watu waliooa na kuolewa tena wakaapa mbele ya padri/mchungaji altaren kuwa watakuwa waaminifu lakn wao ndo wa kwanza kuvunja viapo vyao. ME NAFIKIRI IFIKE WAKATI HIVI VIAPO VIFUTWE MAKE HAVINA MAANA. ni mtazamo wangu charminglady
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...