Sijioni kama naweza kuvaa pete ya ndoa kila siku, eti mpaka milele - sidhani

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,935
22,915
Kuna vitu huwa najaribu vifikiria kwenye maisha najipa majibu tu kuwa sitoweza,maana kama ni kujaribu kuvaa nimeshajaribu kuvaa pete za urembo za kawaida tu muda mrefu ila nimeshindwa. Sasa nikija kufikiria pete ya NDOA ambayo nasikia ile pete ikishaingia kidoleni kuvuliwa ni kwenye special case tu, sijioni kama nitafanikisha hilo.

Huwa nanunua pete za kawaida za urembo natia kidoleni ila kiukweli huwa ile pete sifiki nayo jioni lazima ntajikuta nimeitoa nimeiweka mfukoni mana nahisi kama vidole vyangu vinakereketwa.

SWALI MLIO KWENYE NDOA:
  1. Kuna shida yeyote kama nimeoa na nikatoka kwenda kazini au popote bila pete ya ndoa kidoleni?
  2. Sitofikiriwa vibaya na jamii?
  3. Hili swala ni la uamuzi binafsi au inapasa nipate kibali cha kutovaa pete kutoka kwa mke wangu?
  4. Naombeni kujua nyie mlio kwenye ndoa kuanzia mwaka wa pili na kuendelea hizo pete hapo. Vipi kwa upande wenu?

wedding-rings-for-women-amazing-wedding-rings-for-women-registaz-800-x-800.jpg
 
Hakuna shida ni makubaliano yenu nyie wawili tu

SWALI MLIO KWENYE NDOA :

Kuna shida yeyote kama nimeoa na nikatoka kwenda kazini au popote bila pete ya ndoa kidoleni?


Jamii ni nini

Wanahusika vipi na ndoa yenu na maisha yenu?

Jamii ni jua kwamba lisipowaka Giza litatawala?

Wakikufikiria vibaya au vizuri inakuongezea au kukupunguzia nini

SWALI MLIO KWENYE NDOA :

sitofikiriwa vibaya na jamiii?

Zungumza na ubavu wako. Yeye ndio inamhusu sio wengine

SWALI MLIO KWENYE NDOA :


hili swala ni la uamuzi binafsi au inapasa nipate kibali cha kutovaa pete kutoka kwa mke wangu?

Naombeni kujua nyie mlio kwenye ndoa kuanzia mwaka wa pili na kuendelea hizo pete hapo Vipi kwa upande wenu.

View attachment 1361505



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachungaji waangalie namna ya kuboresha hili swala waweke pia na Saa za ndoa

watu tujichagulie tuvae saa za ndoa au pete za ndoa, kuvaa saa kwangu itakua option

bora zaidi kuliko hicho ki ring kisichosogea kidoleni,kwangu n mtihani haswa
 
Kiimani (kwa baadhi ya wakristu), Pete ni ishara ya pendo lako kwa mwenzio. Pia ni ishara kwa jamii kwamba umekwishaoa/olewa.

Kuvaa/kutovaa pete wakati wote nadhani kimsingi inahitaji maelewano tu kati yako na mwenzi wako wa ndoa - na hasa kwa vile baadhi ya watu hutafsiri kutovaa pete hiyo kama dalili ya ukware.
 
Sioni shida yeyote kuivaaa. Huwa naivua nikitaka kuoga na kulala. Ikitokea nimesahau kuivaa huwa naona kidole kimepooza sana.
 
Kuna vitu vingi sijawahi kuvaa na pete ni mojawapo
Pete naziogopa sana nikiona watu mpaka wanakatwa vidole kwa kuvimba
Ila sijawahi kupendelea pia kuvaa tu na sio lazima kwangu



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kuna vitu vingi sijawahi kuvaa na pete ni mojawapo
Pete naziogopa sana nikiona watu mpaka wanakatwa vidole kwa kuvimba
Ila sijawahi kupendelea pia kuvaa tu na sio lazima kwangu



Sent from my iPhone using Tapatalk
Pete mi nadhani ivaliwe kama pambo tu

uvae kwenye event flani mkitoka inavuliwa

ila hii ya kuamka na pete kushinda nayo mpk

kuja kulala nayo usiku,hapa ndio panachangamoto.
 
Back
Top Bottom