Bondpost
JF-Expert Member
- Oct 16, 2011
- 6,602
- 9,343
Tokea utotoni hadi sasa sijawahi kuvaa hata saa ya mkononi, ukiachilia cheni za shingoni, naona kama tabu, sasa tabu imekuja kuwa hii pete ya ndoa, nataka kuitoa kwa kuwa nahisi ni kama foreign body kwenye mwili wangu (irritant object) na mke wangu hataki niivue, je kuna ulazima wowote wa kuivaa muda wote?
nawasilisha..
Nilipata hayo matatizo pindi nimeoa maana sikuwa na tabia ya kuvaa accessories za kiume maishani mwangu, nilikuwa najikuta wakati wa kulala lazima nitoe pete kama navyoitoa saa ya mkononi, nikajizoesha mpaka ikawa habit yangu yani nisipoivaa nahisi kama something is missing na pia my waifu wangu alikuwa anajisikia raha akiona nimevaa pete maana alikuwa anajua sikuvaa pete yeyote ujanani mwangu ilikuwa inampa faraja sana, so ni vizuri ujitahidi kuivaa, pia inakupatia heshima mbele za watu at least unaonekana mwenye majukumu people can trust you, believe it or not, vaa pete yako hata kwa nyumba ndodo ivae ajue kabisa wewe una mkeo hapo upo kwa muda tu! So achague moja!