Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Nakupongeza kwa huu uzi, maana umemuibua mentor wangu Kiranga cha Ngeda Sakala Kandubwa!

Yuko bize na watoto wa 'kitasha' mwenyewe anaita, huko NewYork marekani, haonekani kabisa JF.
Mada zinapwaya, suruali na vibwaya
Ibada za ubaya, kwa wakali wa ulaya
Ghani za Marekani, kukupeni burudani
Gani korodani ndani ya fani fanani, bara na pwani?
 
Kiranga mbona Kama umeamka na hasira?relax mkuu.hayo maneno ya umbeya wanatupa wenzenu wanaorudi na kutupiga virungu sisi na kutumia vizungu vigumuuu ili tuwaamini 🤣🤣🤣
Mimi hata nikipiga chafya ya ki New York, wabongo wataona nimeamka na hasira.

Kwa sababu hawajazoea chafya ya ki New York.

Inapigwa ki agggressive aggressive mpaka anayepiga chafya anaonekana ana hasira.

Ndiyo maana mara nyingine nasoma tu.
 
Sio kweli kwamba kila anaye kwenda ulaya hafanikiwi, inategemea ulienda kwa malengo gani.

Mfano mzuri ni mimi mwenyewe kabla sijaenda US nilikuwa nimeajiriwa Bongo kipato changu kilikuwa cha kawaida sana, mara baada ya kwenda huko na kukaa kwa muda usiozidi hata miaka minne maisha yangu niliyabadilisha kwa kiasi kikubwa… hivi tunavyoongea nimeweza kujenga nyumba mbili za kisasa na viwanja kadhaa mjini, nasomesha wadogo zangu shule za private nina usafiri mzuri ambao vijana wengi wa mjini wanautolea macho. Kitu nilichojifunza wengi wakifika nje hubweteka na kuiga maisha ya watu wa ulaya na kusahau walipotoka.
Kitu kingine wabongo wengi wanapokwenda nje huwa hawaendi kwa kufuata utaratibu wa nchi husika wao huwa wanajiripua mara baada ya kufika huko huwachukua muda mrefu kutafuta makaratasi ya kuwawezesha kuishi kihalali, kwa muda wote ambao wanafight kupata hayo makaratasi huishia kufanya kazi za kawaida ambazo kipato chake ni kidogo hivyo wanashindwa kufanya saving.


👏👏👏

Wale jamaa waliokua wanasema usije kiwanja wakati wao hawajafika hata Chalinze sijui wanajisikiaje sasa 🤣 🤣

Rudi mapambano yaendelee.
 
Kwani wanaijaaa wametushinda nini wao wengi wao wametoboa maana tusiseme tu eti kisa issues zao nyeusi ? Sisi majungu na unaaa wa bongo tunaupeleka majuuu.
 
Naunga mkono hoja! Ukiwa na profession ulaya rahisi kutoboa sana hasa hizo za afya malipo mazuri! Unaingiza hela nyingi kwa muda mfupi halafu hata uki convert kibongo ukiwa na. Pound 5000 tu ni hela ndefu huku na wala kwao kuipata sio kazi kama unajishughulisha!
Sasa mkuu Nyani Ngabu miaka aliyokaa huko si angekuwa ana flats za kutosha Masaki na Mikocheni
 
Mimi hata nikipiga chafya ya ki New York, wabongo wataona nimeamka na hasira.

Kwa sababu hawajazoea chafya ya ki New York.

Inapigwa ki agggressive aggressive mpaka anayepiga chafya anaonekana ana hasira.

Ndiyo maana mara nyingine nasoma tu.
Nyani ngabu
 
Mada zinapwaya, suruali na vibwaya
Ibada za ubaya, kwa wakali wa ulaya
Ghani za Marekani, kukupeni burudani
Gani korodani ndani ya fani fanani, bara na pwani?
Yoooo! Mzee baba. Going poetic like never before.

Fleva kama hizi tunazikosa siku hizi, JF imepoteza ladha.
 
Ndo maana wanatetea nonsense kwa kushindwa kufikiri sawa.

Mtu aliye illogical kiasi hiki hawezi kuwa na kasi ya maisha inayohitajika kuishi na kufanikiwa ughaibuni acha abaki Chitipa tu.
Huyu dada msameheni bure tu, ni mwanamke aliyejiruhusu kuwa na limited options, anachowaza yeye ni kujiuza, soma komenti yake...
Hahahahahaaaaaa. Hujui kitu ndio maana unaongea tu. Hujajibu swali langu hata moja kazi yako kudeflect. Eti viwanda. Unafikiri tupo kwenye 1960s?Utaenda kwenye hizo nchi upewe work permit ya kuwa kibarua kiwandani? Au ni ujuzi gani uliospesho sana ulionao wewe kwenye sekta ya viwanda ambayo hana mtu kwenye hio nchi au nchi za jirani?
Ndugu utaishia kujiuza.
 
Hivi inakuaje walioenda uarabuni wanakua tofauti na walioenda ulaya,asilimia kubwa walioenda uarabuni wanawekeza sana bongo,kujenga nyumba zao n.k Hata kama alienda kufanya kazi tu za ndani akirud anakua vizur tofaut na waulaya sio wote but asilimia kubwa
 
Hivi inakuaje walioenda uarabuni wanakua tofauti na walioenda ulaya,asilimia kubwa walioenda uarabuni wanawekeza sana bongo,kujenga nyumba zao n.k Hata kama alienda kufanya kazi tu za ndani akirud anakua vizur tofaut na waulaya sio wote but asilimia kubwa
Hizo kazi za ndani utapata wapi muda wa kula bata?

Halafu hizo kazi za ndani ni za mikataba unajua kabisa mwaka flani ninarudi TANZANIA
 
Back
Top Bottom