Hivi kuna tofauti kati ya biashara ya Forex, kubet na ununuzi wa hisa?

Biashara unajua kabisa nachukua mahindi Mbeya kwa 6000 debe naenda kuuza dar 10000 debe. Unapiga gharama ya usafiri unajua na faida yako. Kwenye Hisa unabet kuwa labda jinsi uchumi unavyoenda basi hisa za FB zitapanda. Unanunua ili uuze kwa faida, ila huna hakika. Kwenye Fx unaangalia uchumi wa nchi na matukio kucheki kupanda na kushuka kwa pesa unaenda na hizo taarifa kufanya business ila huna hakika itapanda kiasi gani au itakuwaje na inaweza isiwe hivyo kabisa.
Hata kwenye kubet mpira watu wanacheki vikosi, nani yuko nyumbani, majeruhi, umuhimu wa game, nani anajua kujilinda, nani anafunga sana nk. kisha anatumia hizo taarifa kuweka mkeka. hizi mambo zinafanana sana. Tofauti na mtu anayenunua mashati China na kuja kuuza Bongo. Anajua kabisa ataauza kiasi gani na atapata faida kiasi gani. Ukienda na hela ndogo anakwambia hailipi.
Mbona hii nayo ni betting pia...ukikuta watu wengi wameleta mahindi kama wewe utayauza kwa 10000 hivyo hiyo?
 
Well mi naona betting is betting kama ilivyo na forex ni betting lakini yenyewe risk yake ndogo ukilinganisha na betting yenyewe.

Lakini inapokuja ishu ya hisa, inategemeana na wewe unavyoucheza mchezo, kama unanunua na kusubiri baada ya muda zipande ili uuze then unakuwa speculator, kwa sababu sehemu kubwa ya sababu zinazosababisha kupanda na kushuka kwa bei za hisa mara nyingi ziko nje ya uwezo wa market players na hakuna anaeweza kuzipredict (the market is full of suprises).

Ila kama unanunua na kuzihold kwa mda mrefu, say 10 years or more, basi unakuwa investor kwa sababu thamani ya hisa inatarajiwa kupanda (in a long run) plus unakuwa unaendelea kuenjoy devidends along the way.

Kuspecurate kunafaida kubwa zaidi ukiringanisha na kuinvest (watu huwa wawin big huko lakini wengine wanalose kila kitu pia). Kama kawaida "big return comes with big risks and vice versa".

Binafisi nadhani watu tunatakiwa kulitazama soko la hisa kama moja ya options of our way up to financial freedom na sio kama biashara yeneywe or au labda uwe na funds mbili, one to finance your future and the other for play.
 
Back
Top Bottom