Hivi kuna haja ya fungate jamani??

Na mimi naongelea fungate.Kama ambavyo wazungu waliianzisha kwa maana yao ndivyo ambavyo na sisi tunaweza kubadili maana kuendana na mazingira yetu.Oh alafu nna njaa...sijala kabisa leo!

...fungate muhimu bana, hata mkiwa kwenye ndoa si vibaya mara moja kwa mwaka kujipa fungate!
Mnahitaji muda nyie wawili faragha mbali na majukumu yenu ya kila siku ku 'refresh!'
Kwa hao wana ndoa, acha nao wapumzike baada ya heka heka za kuandaa harusi.
waheshimiwa Mbu na Lizzy labda mtupe maana ya fungate kwanza. halaf tutauliza masuali ya nyongeza.
 
waheshimiwa Mbu na Lizzy labda mtupe maana ya fungate kwanza. halaf tutauliza masuali ya nyongeza.

Hivi babu na bibi zetu walikuaga na fungate?Sio lazima kuiga kila kitu kama kilivyo kwahiyo maana tuliyoletea sio muhimu hapa!Wanaoenda wanatumia kama muda wa kupumzika..kuconnect au kureconnect kitu ambacho nadhani ndo muhimu kwa wanandoa wote..hata kama walishazeeka!
 
waheshimiwa Mbu na Lizzy labda mtupe maana ya fungate kwanza. halaf tutauliza masuali ya nyongeza.

...pheewww, umeni quote kabla sija edit bana.
Fungate ni kwa wanandoa changa (Newly Weds)

Najaribu kutafuta neno muafaka kwa Veterans kama mimi,
nikienda ku renew vows, siwezi kwenda/kuita 'fungate?'
 
Hivi babu na bibi zetu walikuaga na fungate?Sio lazima kuiga kila kitu kama kilivyo kwahiyo maana tuliyoletea sio muhimu hapa!Wanaoenda wanatumia kama muda wa kupumzika..kuconnect au kureconnect kitu ambacho nadhani ndo muhimu kwa wanandoa wote..hata kama walishazeeka!
kwa hili la fungate nadhani wazungu ndio waliiga afrika. hivi unajua fungate lilianzia afrika, naomba usibishe nina data kamili.
 
...pheewww, umeni quote kabla sija edit bana.
Fungate ni kwa wanandoa changa (Newly Weds)

Najaribu kutafuta neno muafaka kwa Veterans kama mimi,
nikienda ku renew vows, siwezi kwenda/kuita 'fungate?'

ukilipata utatusaidia wengi, hata mimi nalihitajia.
 
Nabisha mpaka ntakapoona hizo data!
nitarejea, acha niwasiliane na ofisi flani hivi. hakikisha unanisubiri na karatasi na kalam. nilipojiunga na JF nilijua kwamba nahitajika. sikujiunga kuongeza idadi ya member tu.
 
nitarejea, acha niwasiliane na ofisi flani hivi. hakikisha unanisubiri na karatasi na kalam. nilipojiunga na JF nilijua kwamba nahitajika. sikujiunga kuongeza idadi ya member tu.

Nani tena anakuhitaji??
 
Hivi babu na bibi zetu walikuaga na fungate?Sio lazima kuiga kila kitu kama kilivyo kwahiyo maana tuliyoletea sio muhimu hapa!Wanaoenda wanatumia kama muda wa kupumzika..kuconnect au kureconnect kitu ambacho nadhani ndo muhimu kwa wanandoa wote..hata kama walishazeeka!
Jamii nyingi za kiafrika walikuwa na honeymoon ya aina ingine,baada ya harusi kwa wiki moja hawatoki ndani na wanahudumiwa kila kitu na ndugu,idadi ya siku ilitofautiana kati ya jamii.
 
Jamii nyingi za kiafrika walikuwa na honeymoon ya aina ingine,baada ya harusi kwa wiki moja hawatoki ndani na wanahudumiwa kila kitu na ndugu,idadi ya siku ilitofautiana kati ya jamii.
kamanda asavali umenijibia. huyu Lizzy naona ameanza kusahau afrika tangu apate ka viza ka kwenda romania.
 
Hahaha visa ya Romania tena ? lol! kamanda unauaaa hivi ulirudi lini kutoka Chekoslovakia ? lol!
ina maana hakukushtua Lizzy, mbona aliaga sana tu hapa. Mkuu bado nipo huku shekoslovakia, wazembe wanakula mikate balaa, kila hatua nane kuna bakery.
 
ina maana hakukushtua Lizzy, mbona aliaga sana tu hapa. Mkuu bado nipo huku shekoslovakia, wazembe wanakula mikate balaa, kila hatua nane kuna bakery.
Hawawashindi wazambia mtu anamaliza mkate mzima na soda moja lol!
 
Jamii nyingi za kiafrika walikuwa na honeymoon ya aina ingine,baada ya harusi kwa wiki moja hawatoki ndani na wanahudumiwa kila kitu na ndugu,idadi ya siku ilitofautiana kati ya jamii.
Mhuu!Sasa Kloro embu sema kuna ubaya gani hata wakongwe kama mimi na mwenzangu tukiamua kujifungia ndani wiki moja?
 
kamanda asavali umenijibia. huyu Lizzy naona ameanza kusahau afrika tangu apate ka viza ka kwenda romania.
Kama kawaida yako..yani kuficha siri kunakushinda kabisa?Ndo maana huitajiki magharibi wala mashariki..achilia mbali kusini na kaskazini.
 
by definition Honeymoon ni vacation taken by a newly married couple.

Mimi ni mmoja wapo ambaye nilioa wakati tumeshazaa mtoto mmoja na lovely wife wangu. Lakini nili-enjoy sana honeymoon nadhani ktk siku chache ambazo nilifurahia mama yangu kunileta ktk dunia ni siku hiyo.

Kwanza zile pilika za harusi na mahangaiko yote ambayo yanatokea na ule wasiwasi kama je shughuli itafana (kwa ufupi stress zote za harusi) ndio zinaenda kuisha kule kwa kweli ni siku nzuri sana maishani na waliyobuni walishaona hayo ni vacation ya mapumziko na kumshukuru Muumba kwa kuwawezesha kufunga ndoa.

I remember the day baada ya harusi j/pili yake tulikaa ufukweni mwa bahari na kulikuwa na watu wengi sana walikuja kwenye ile hoteli na kufanya ufukwe upendeze sana na j/pili jioni kulikuwa na live bendi yaani kila nyimbo iliyopigwa tuliona kama tunaimbiwa sisi, pia pale hotelini walituwekea mauaridi mpk kitandani na kutuandikia kadi yenye ujumbe wa maisha mema ya ndoa na walisaini wafanyakazi karibu wote wa hoteli yaani tulifurahia mpk tukawapa keki moja kati ya mbili tulizopewa harusini wafanyakazi wa ile hoteli (naomba nisiitaje)

Mwaka juzi tulienda tena kutembelea ile hoteli na kulala the same room tuliyolala siku ya honeymoon

Ni siku nzuri sana nawashauri vijana wote ambao hawajaoa waende honeymoon ni muhimu sana tena mkifika huko mzime simu kabisa muwe free peke yenu wawili tu mfurahi na kupanga mipango ya maisha yenu

Husipoenda honey moon ina maana ukitoka tu siku ya harusi unaanza kukutana na matatizo mara zawadi zimebaki ukumbini unatakiwa kuzifuata, mara shangazi katoka Ntwara hana nauli ya kurudi kisha unajikuta unakosa muda wa kupumzisha akili na mkeo

Honey moon ni muhimu sana tena kupita maelezo hata kama umechoka kiuchumi jipange uende honey moon sehemu ya bei ya chini mkapumzike na mwenzi wako. Mnataka kuchakachua mpk mambo ya msingi mmmmh
 
Umaana upo kwa wahusika.

Hakuna cha wahusika. Maana ni maana tu, na huwa ni standard. Haiwezekani kila mtu awe na maana yake katika jambo moja. Maana lazima iwe common. Kama katika lugha ya kiswahili mzazi wa kiume anaitwa baba, basi itabaki kuwa hivyo siku zote. Hakuna kuwa na maana tofauti hapo.
 
Back
Top Bottom