Hivi kumbe kubadilisha badilisha majina shuleni inaweza leta shida mbeleni hivi?

excel

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
21,293
14,764
Dah, wakuu nimejikuta namsikitia sana Makonda P.J kwenye huu msala wa majina yake mengine ya Daudi Bashite, bila kujali alinunua au alibadilisha!

Itampa wakati mgumu sana kutuonesha vyeti vyake ni kuondoa sintofahamu hii kwa watanzania wanaofuatilia hili sakata.

Je, vipi kuhusu mheshimiwa John Heche? wadakuzi waliosoma nae Musoma Technical wanasema sio jina lake halisi? kwamba walimjua kwa jina la Wegesa Charles?

Je, yeye ni John Heche au Wegesa Charles?

Tuna haki ya kuhoji uhalisi wa Taaluma za viongozi wetu na wao watupatie ufafanuzi.

Hili la Heche sina uhakika nalo sana, lipo mezani kwa mjadala
karibuni
 
Endelea kufikiria kwa sanaaaaa tu

Mnajua kudonoa donoa kila dakika

Mnampenda sana ndio maana hamuachi kumfikiria

Makonda oyeeeeee
 
Aisee haya mambo yalikuwepo sana zamani, kuna watu walikua wanaazimana vyeti kuombea ajira hapo nazungumzia miaka ya 90 kurudi nyuma! Ngoja tuendelee kufukua tu, tunaweza jua mambo mengi sana.

[HASHTAG]#gwajimahunaphdachausanii[/HASHTAG]
 
uadilifu haupo unaponunua jina la mtu mwenye uwezo, hata kama na wewe utaendana na wezo wake;

hakuna uadilifu pia katika kutumia cv za mtu kujipatia chochote, licha ya kuwa kosa kughushi, lakini pia utakuwa mwizi wa kuaminiwa
 
Acha maneno.

Tatizo la RC ni kutumia cheti cha mtu mwingine ili kuendelea na masomo baada ya kupata Zero (F hadi kiswahili na Civics.....!!!!!).

Ni wengi hawatumii majina yao au wanatumia ya ubatizo ila kwa makonda shida sio jina lake wala elimu yake tatizo ni CHEO ALICHONACHO WENGI WANATAKA CREDIT YA KUWA WAMEMTEMESHA ULAJI ALIONAO.
 
Failure ila ndio kiongozi wenu(ujanja kuwahi). Kama ni mburura asingeweza kufika hapo kwa cheo alichonacho. Mbona mwenyekiti wa wema nae ni bashite tu ila anakuzidi kiuongozi na pesa.
Acha maneno.

Tatizo la RC ni kutumia cheti cha mtu mwingine ili kuendelea na masomo baada ya kupata Zero (F hadi kiswahili na Civics.....!!!!!).
 
Failure ila ndio kiongozi wenu(ujanja kuwahi). Kama ni mburura asingeweza kufika hapo kwa cheo alichonacho. Mbona mwenyekiti wa wema nae ni bashite tu ila anakuzidi kiuongozi na pesa.
Kiiichomfikisha hapo ni u homeboy.

Bashite a.k.a Mr F (ZERO).

Yaani mbwembwe zote zile kumbe alishindwa kupata walau D ya Kiswahili inamaana jamaa hajui hata aina za Vitenzi.
 
Sizani kama kutumia jina la mtu afu ukafanya mtihani mwenyewe ni shida sana. Bali kununua cheti ambacho mwingine ndio alifanya mtihani.
Yote ni makosa, tena wanasema ya jinai. Kununua jina ili ulitumie kufanyia mtihani ni kosa, kununua vyeti ni kosa, kulipa mtu akufanyie mtihani ni kosa...yote ni makosa na ikibainika hivyo inabidi uhukumiwe accordingly.

Watu wanahaso kusoma ili wapate vyeti na hatimaye kuajiriwa/kujiajiri, wengine wananunua majina, vyeti na kufanyiwa mitihani...they must be punished!!
 
Li-ulimi limejaa mno mdomoni! Akili itatoka wapi? Ngoja niende nisake maswali ya mitihani ya mwaka 2000 tuone ilikuwa migumu kiasi gani mpaka mungu wa Dar akashindwa hata kupata D moja!!
 
Tatizo Sio kubadili jina unaweza kubadili jina kisheria hamna tatizo. Tatizo ametumia cheti cha mtu mwingine na hili ni kosa linalokupa miaka saba jela!!
 
Maskin yaan unavyojitapa kwenye keyboard huku maisha halisi umepigika aisee.

Niwekee vyeti vyake nivione basi au namba yake ya mitihani nikaangalie necta
Kiiichomfikisha hapo ni u homeboy.

Bashite a.k.a Mr F (ZERO).

Yaani mbwembwe zote zile kumbe alishindwa kupata walau D ya Kiswahili inamaana jamaa hajui hata aina za Vitenzi.
 
Aisee haya mambo yalikuwepo sana zamani, kuna watu walikua wanaazimana vyeti kuombea ajira hapo nazungumzia miaka ya 90 kurudi nyuma! Ngoja tuendelee kufukua tu, tunaweza jua mambo mengi sana.

[HASHTAG]#gwajimahunaphdachausanii[/HASHTAG]
Daud Bashite kaiba cheti cha Paulo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom