Hivi kazi ya wabunge hapa Tanzania ni nini?

Luca Paguro

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2023
Posts
476
Reaction score
1,060
Nauliza tu kazi ya wabunge Tanzania ni nini?

Sisi kwenye Civics tuliambiwa kazi kuu ya Mbunge ni kuwawakilisha wananchi, sasa mbona kero za wananchi hatuoni zikijadiliwa kwa wingi bungeni?

Wananchi wanadai Katiba Mpya, Uchaguzi Huru na wa Haki, wanataka waweze kukosoa serikali kwa uhuru bila kuhofia kutekwa, wanataka mazingira mazuri ya kuajiriwa na kujiajiri, nk. Haya yote yanahitaji watu smart wa kuyajadili na kuyafanyia ufumbuzi.

Ukisema maisha ni magumu kwa mamilioni ya Watanzania, watu wanasema serikali haiwezi kukuletea hela nyumbani kwako, ukikosoa serikali wanakuita mhaini, ukiongea kuhusu miundombinu mibovu serikali inafumba macho, kama jinsi mikoani tunavyoteseka na shida ya maji.

Maana yake matatizo ya wananchi hakuna anayeyasikiliza, na mengi wanasema sio kazi ya serikali au wanayapuuzia, ukiyataja wanasema wewe sio mzalendo!

Sasa kama wananchi wenyewe ndio sisi, na hakuna wa kutetea kero zetu bungeni, kazi ya wabunge huwa ni nini? Kwamba ubunge imekuwa tu kazi ya kukimbiliwa ili kupata posho, mishahara mikubwa, magari ya kifahari na mafuta full tank?

Wabunge wanalipwa hela kubwa, tena nchi masikini kama Tanzania inawanunulia magari ya kifahari, inawajazia na mafuta, wanapewa posho nyingi na mishahara mikubwa na sijui kama wanalipa kodi hawa. Wamekuwa wakilipwa hivi kwa miaka na miaka ila kero za wananchi kila siku zinaongezeka badala ya kupungua!

So, kazi ya wabunge ni nini?
 
BUNGE HALIPO HAPO KUBADILISHA MAISHA YAKO .

KAMA KUNA KERO MTAANI ITATUENI KWA KUSHIRIKIANA

MKISHINDWA KUJIPAMBANIA MJIANDAE KUUMIA

N.B KIJANA KATAA MAANDAMANO LINDA UHAI WAKO .
 
Nauliza tu kazi ya wabunge Tanzania ni nini

Sisi kwenye Civics tuliambiwa kazi kuu ya Mbunge ni kuwawakilisha wananchi, sasa mbona kero za wananchi hatuoni zikijadiliwa kwa wingi bungeni?

Wananchi wanadai katiba mpya, uchaguzi huru na wa haki, wanataka waweze kukosoa serikali kwa uhuru bila kuhofia kutekwa, wanataka mazingira mazuri ya kuajiriwa na kujiajiri
Haya yote yanahitaji watu smart wa kuyajadili na kuyafanyia ufumbuzi

Ukisema maisha ni magumu kwa mamilioni ya Watanzania, watu wanasema serikali haiwezi kukuletea hela nyumbani kwako, ukikosoa serikali wanakuita mhaini, ukiongea kuhusu miundombinu mibovu serikali inafumba macho, kama jinsi mikoani tunavyoteseka na shida ya maji.

Maana yake matatizo ya wananchi hakuna anayeyasikiliza, na mengi wanasema sio kazi ya serikali au wanayapuuzia, ukiyataja wanasema wewe sio mzalendo

Sasa kama wananchi wenyewe ndio sisi, na hakuna wa kutetea kero zetu bungeni, kazi ya wabunge huwa ni nini?
Kwamba ubunge imekuwa tu kazi ya kukimbiliwa ili kupata posho, mishahara mikubwa, magari ya kifahari na mafuta full tank?

Wabunge wanalipwa hela kubwa, tena nchi masikini kama Tanzania inawanunulia magari ya kifahari, inawajazia na mafuta, wanapewa posho nyingi na mishahara mikubwa na sijui kama wanalipa kodi hawa
Wamekuwa wakilipwa hivi kwa miaka na miaka ila kero za wananchi kila siku zinaongezeka badala ya kupungua

So
Kazi ya wabunge ni nini?
Pole mkuu, magufuli alijenga mfumo mzuri wa bunge,lilijaa wapinzani nusu ya wabunge wote,
Chaguzi zote kipindi cha Magufuli zilikuwa fair kabisa...sijui nani wakulaumiwa kwa hizi lawama zako au tumshtakie Yesu
 
KAMA KUNA KERO MTAANI ITATUENI

MKISHINDWA KUJIPAMBANIA MJIANDAE KUFA MASIKINI .

N.B KIJANA KATAA MAANDAMANO LINDA UHAI WAKO .
Sasa kwa nini linatumia pesa zetu kwa lazima kama halina kazi yoyote ya kuboresha maisha yetu??
 
BUNGE HALIPO HAPO KUBADILISHA MAISHA YAKO .

KAMA KUNA KERO MTAANI ITATUENI KWA KUSHIRIKIANA

MKISHINDWA KUJIPAMBANIA MJIANDAE KUUMIA

N.B KIJANA KATAA MAANDAMANO LINDA UHAI WAKO .
Soma tena kilichopostiwa na ulichokijibu... na ndio maana GenZ wanaburuta haswa ni majibu kama haya
 
Nauliza tu kazi ya wabunge Tanzania ni nini

Sisi kwenye Civics tuliambiwa kazi kuu ya Mbunge ni kuwawakilisha wananchi, sasa mbona kero za wananchi hatuoni zikijadiliwa kwa wingi bungeni?

Wananchi wanadai katiba mpya, uchaguzi huru na wa haki, wanataka waweze kukosoa serikali kwa uhuru bila kuhofia kutekwa, wanataka mazingira mazuri ya kuajiriwa na kujiajiri
Haya yote yanahitaji watu smart wa kuyajadili na kuyafanyia ufumbuzi

Ukisema maisha ni magumu kwa mamilioni ya Watanzania, watu wanasema serikali haiwezi kukuletea hela nyumbani kwako, ukikosoa serikali wanakuita mhaini, ukiongea kuhusu miundombinu mibovu serikali inafumba macho, kama jinsi mikoani tunavyoteseka na shida ya maji.

Maana yake matatizo ya wananchi hakuna anayeyasikiliza, na mengi wanasema sio kazi ya serikali au wanayapuuzia, ukiyataja wanasema wewe sio mzalendo

Sasa kama wananchi wenyewe ndio sisi, na hakuna wa kutetea kero zetu bungeni, kazi ya wabunge huwa ni nini?
Kwamba ubunge imekuwa tu kazi ya kukimbiliwa ili kupata posho, mishahara mikubwa, magari ya kifahari na mafuta full tank?

Wabunge wanalipwa hela kubwa, tena nchi masikini kama Tanzania inawanunulia magari ya kifahari, inawajazia na mafuta, wanapewa posho nyingi na mishahara mikubwa na sijui kama wanalipa kodi hawa
Wamekuwa wakilipwa hivi kwa miaka na miaka ila kero za wananchi kila siku zinaongezeka badala ya kupungua

So
Kazi ya wabunge ni nini?
Kushindana kumsifia Rais
 
BUNGE HALIPO HAPO KUBADILISHA MAISHA YAKO .

KAMA KUNA KERO MTAANI ITATUENI KWA KUSHIRIKIANA

MKISHINDWA KUJIPAMBANIA MJIANDAE KUUMIA

N.B KIJANA KATAA MAANDAMANO LINDA UHAI WAKO .
downloadfile.jpg
 
Pole mkuu, magufuli alijenga mfumo mzuri wa bunge,lilijaa wapinzani nusu ya wabunge wote,
Chaguzi zote kipindi cha Magufuli zilikuwa fair kabisa...sijui nani wakulaumiwa kwa hizi lawama zako au tumshtakie Yesu
uchaguzi Kama wa 2020 ulikuwa fair sana
 
Back
Top Bottom