MLAU
JF-Expert Member
- Aug 23, 2007
- 4,726
- 3,354
Pamoja na Maelezo mengi kuhusu issue hiyo ya kiwanja na kusema mwishoni kuwa mama hana hatia.Nimefuatilia maelezo ya mama na mwenyekiti Wa mtaa aliyewekwa ndani na mkuu Wa mkoa Wa Dar es salaam nimebaini vitu kadhaa ambavyo vinasikitisha hasa katika mstikabari Wa uongozi na viongozi Wa serikali
1. maelezo yaliyokuwa yanatolewa na mama yanajitosheleza hivyo mpaka mkuu Wa mkoa anafikia hatua ya kutoa amri kwa mama Huyo awekwenp ndani sikuona sababu ya kumtia hatiani.
2. mama amekubali kuwa kiwanja kimeuzwa lakini kwa makubaliano na wananchi pamoja na wajumbe na ametaja na tarehe ambapo kulifanyika vikao vilivyobariki uuzwaji Wa ardhi hiyo.
3 mama anajaribu kumuelewesha mkuu Wa mkoa kwa umaridadi kabisa kuwa eneo limeuzwa na pesa IPO, na diwani analijuwa hill na diwani huyo alishiriki katika vikao vyote.
4. Baadhi ya wajumbe ambao wanaonekana kuwa wanachama Wa chama cha mapinduzi ( mmoja kavaa tisheti ya chagua magufuli) wanajaribu kubisha kwa hoja za kuungaunga eti wao huwa hawashirikishwi eti wanaoshiriki ni wajumbe watatu. hoja dhaifu.
polisi wanaamuriwa wamkamate. mpaka hapo sikuona sababu ya kumkamata maana ardhi imeuzwa kwa makubariano ya wananchi na uongozi husika Wa mtaa na mama ana ushahidi wote.
Hizi ni siasa za kipuuzi, umefanya mauzo mbele ya watu ili kupata umaarufu lakini Nina uhakika huyo mama hata mngempeleka mahakama ya Lumumba atawagaragaza. lakini najuwa lengo lako ulitaka uonekane unatumbua ila ukweli unaujuwa huyu mama kwa maelezo pamoja na maelezo ya kuunga unga ya watu wanaomtuhumu, hana hatia
nawasilisha.
Kumbuka kuwa wanainchi wanapolalamikia jambo jua kuwa kuna tatizo mahali aidha kwa Viongozi,mnunuzi au hata huyo mama mwenyewe.
Na ni moja ya majukumu ya viongozi kuhakikisha wanainchi wanakaa kwa amani,kutatua matatizo ya jumla ya jamii husika na pia kuwawekea mazingira mazuri kujijenga kiuchumi.
Huwezi jua labda kawekwa ndani kwa usalama wake baada ya tuhuma kutolewa hadharani mass unaweza kutoka na hasira ikadestroy Mali zako kama utatoka unajigamba 'hamniwezi' ukaamsha hasira kwa jamii yanatokea hayo.
Let's wait and see what next