Hivi kama siyo siasa za kijinga, huyu mama alikuwa na kosa gani la kuwekwa ndani?

Kwa mwendo wako huu huyu RC yatamshinda kabisa maana mama alisema hata ukitaka ushahidi nipo tayari kukupeleka eneo ambako tumeanza ujenzi wa shule na maelezo ya gharama za matumizi yote yapo,heee ghafla OCD kamata weka ndani huyu mama
 
Hivi kuna watu wanafuatilia hayo maigizo!? Bora niangalie Isidingo kuliko hayo maonyesho.
cc; Watu wa Lumumba mnamuona huyu mwenzenu ameanza kujitambua? Amkeni na nyie maana mnadharauliwa!
Nyerere alisema, mtu mwerevu akikuambia mambo ya kipuuzi nawe ukamkubalia na kumshangilia ATAKUDHARAU. Hivyo Magu na Makonda wanawadharau
 
HAMY-D leo umeona kuwa ni maigizo kumbuka UKAWA tuliwaeleza mapema sana kuwa viongozi wote wa ccm hufikiria kwa kutumia masaburi.



swissme
 
Kwa kuwa serikali imeshindwa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji, malalamiko ya wananchi ni mengi kupindukia, kwa muktadha wa posti yako waziri mwenye dhamana amepaswa kuswekwa korokoroni?
Pamoja na Maelezo mengi kuhusu issue hiyo ya kiwanja na kusema mwishoni kuwa mama hana hatia.

Kumbuka kuwa wanainchi wanapolalamikia jambo jua kuwa kuna tatizo mahali aidha kwa Viongozi,mnunuzi au hata huyo mama mwenyewe.

Na ni moja ya majukumu ya viongozi kuhakikisha wanainchi wanakaa kwa amani,kutatua matatizo ya jumla ya jamii husika na pia kuwawekea mazingira mazuri kujijenga kiuchumi.

Huwezi jua labda kawekwa ndani kwa usalama wake baada ya tuhuma kutolewa hadharani mass unaweza kutoka na hasira ikadestroy Mali zako kama utatoka unajigamba 'hamniwezi' ukaamsha hasira kwa jamii yanatokea hayo.

Let's wait and see what next
 
Kiukweli hata Mimi namefuatilia Yale maohojiano nilijifunza ni kwamba hii ziara imekaa kimikakati ya kisiasa. Yule mama hana kosa na amejibu maswali yote kwa usahihi na kujiamini kabisa

Makonda anafanya UONEVU na UDHALILISHAJI kwa Watumishi wa umma!Juzi Waziri Mkuu Majaliwa amekemea huu upumbavu lakini Muk*nd* anajifanya kidume.
Ushauri wangu kwa huyu Mama AENDE AKAMWONE WAZIRI MKUU kwa hatua zaidi.
 
hivi mahakama na viongozi nani anatoa amri ya mtu kuwekwa ndani..? au katiba imewapa viongozi mamlaka hayo..?

KENZY,
Kwa sasa Tanzania hasa hii A5 Utawala wa SHERIA au Katiba umewekwa kapuni! Nchi inaendeshwa kwa Maagizo,Maelekezo na Mihemko ya JPM na Vikaragosi wake! Poor Tanzania.
 
hivi mahakama na viongozi nani anatoa amri ya mtu kuwekwa ndani..? au katiba imewapa viongozi mamlaka hayo..?
Kama umefanya jinai polisi wanakukamata tu then unapelekwa mahakamani. so yes, mkuu wa mkoa anayo mamlaka ya kukusweka ndani whether kwa kukuonea au laa
 
Serikali ya jpm haitaki ubabaishaji sasa hivi imefikia ,wakati kila jambo liwekwe wazi hakuna siri ,mnacho kitetea hapa hakipo ,mwacheni makonda awanyoshe wezi
 
Nimefuatilia maelezo ya mama na mwenyekiti Wa mtaa aliyewekwa ndani na mkuu Wa mkoa Wa Dar es salaam nimebaini vitu kadhaa ambavyo vinasikitisha hasa katika mstikabari Wa uongozi na viongozi Wa serikali

1. maelezo yaliyokuwa yanatolewa na mama yanajitosheleza hivyo mpaka mkuu Wa mkoa anafikia hatua ya kutoa amri kwa mama Huyo awekwenp ndani sikuona sababu ya kumtia hatiani.

2. mama amekubali kuwa kiwanja kimeuzwa lakini kwa makubaliano na wananchi pamoja na wajumbe na ametaja na tarehe ambapo kulifanyika vikao vilivyobariki uuzwaji Wa ardhi hiyo.

3 mama anajaribu kumuelewesha mkuu Wa mkoa kwa umaridadi kabisa kuwa eneo limeuzwa na pesa IPO, na diwani analijuwa hill na diwani huyo alishiriki katika vikao vyote.

4. Baadhi ya wajumbe ambao wanaonekana kuwa wanachama Wa chama cha mapinduzi ( mmoja kavaa tisheti ya chagua magufuli) wanajaribu kubisha kwa hoja za kuungaunga eti wao huwa hawashirikishwi eti wanaoshiriki ni wajumbe watatu. hoja dhaifu.

polisi wanaamuriwa wamkamate. mpaka hapo sikuona sababu ya kumkamata maana ardhi imeuzwa kwa makubariano ya wananchi na uongozi husika Wa mtaa na mama ana ushahidi wote.

Hizi ni siasa za kipuuzi, umefanya mauzo mbele ya watu ili kupata umaarufu lakini Nina uhakika huyo mama hata mngempeleka mahakama ya Lumumba atawagaragaza. lakini najuwa lengo lako ulitaka uonekane unatumbua ila ukweli unaujuwa huyu mama kwa maelezo pamoja na maelezo ya kuunga unga ya watu wanaomtuhumu, hana hatia

nawasilisha.
Halafu tukumbuke masuala ya mtaani watu wengi huwa hawafuatilii kwa karibu hivyo. Sasa inapofikia hatua viongozi tunatoa maamuzi kwa zomeazomea na kuwadharirisha viongozi wa Chini mimi naona sio sawa. Japo sikatai Kwamba huko mitaani kuna tatizo.
 
Back
Top Bottom