Hivi kama siyo siasa za kijinga, huyu mama alikuwa na kosa gani la kuwekwa ndani?

hivi mahakama na viongozi nani anatoa amri ya mtu kuwekwa ndani..? au katiba imewapa viongozi mamlaka hayo..?
Mkuu awamu hii ni ya ajabu sana, eti hata wabunge wa ccm nao wanamamlaka ya kutumbua na kuwashusha vyeo watumishi wa uma
 
uyo mama walimuonea sn....na sisi tulijua tu kua watamkamata maana kuna baadhi ya wananchi wasiokua na fikra ndefu watakuepo kwny mkutano.....waliomchongea uyo mama ni wananchi wa kawaida ambao sio wanachama na ambao walikua wanadhn iko kiwanja ni cha serikali kumbe sio cha serikali ni cha taasisi
 
Hivi kuepusha shari usipoenda kwenye hiyo mikutano ya ccm kisheria watakufanya nini?
 
Nisiwe mnafiki nachukia utendaj kaz wa makonda wa kutaka kujifanya yy ndio mwenye maamuz ya kila kitu kwa dar sitoshangaa siku akimsimamisha kaz kiongoz mwenzake aliyepo kwnye kamat ya ulinzi na usalama kwa maana dogo ni mtu wa kujipendekeza sana.
 
Kuna thread humu ilikuwa inauliza ANACHOKIFANYA MAKONDA NI SAHIHI?"

Hatukatai makonda kufanya ziara kujua kero za wananchi wake...

Tunachukia yanayotokea kule kwenye mikutano! Tunachukia hizi siasa za chuki!

Makonda anafanya vitu with popularity image...media kibao! Drones za nini sasa? Majukwaaa makubwa kama kuna fiesta....

Hiyo hela yote ya kuleta media na majukwaa kila mahali anatoa wapi na watu wanatabu dsm?

Mara apigie Magufuli simu amuweke loud speaker! Huu ni uhuni tuu...

Mimi naangalia haya maigizo ! Kila lenye mwanzo lina mwisho...

Kila la kheri makonda na wana Dsm
 
Nimefuatilia maelezo ya mama na mwenyekiti Wa mtaa aliyewekwa ndani na mkuu Wa mkoa Wa Dar es salaam nimebaini vitu kadhaa ambavyo vinasikitisha hasa katika mstikabari Wa uongozi na viongozi Wa serikali

1. maelezo yaliyokuwa yanatolewa na mama yanajitosheleza hivyo mpaka mkuu Wa mkoa anafikia hatua ya kutoa amri kwa mama Huyo awekwenp ndani sikuona sababu ya kumtia hatiani.

2. mama amekubali kuwa kiwanja kimeuzwa lakini kwa makubaliano na wananchi pamoja na wajumbe na ametaja na tarehe ambapo kulifanyika vikao vilivyobariki uuzwaji Wa ardhi hiyo.

3 mama anajaribu kumuelewesha mkuu Wa mkoa kwa umaridadi kabisa kuwa eneo limeuzwa na pesa IPO, na diwani analijuwa hill na diwani huyo alishiriki katika vikao vyote.

4. Baadhi ya wajumbe ambao wanaonekana kuwa wanachama Wa chama cha mapinduzi ( mmoja kavaa tisheti ya chagua magufuli) wanajaribu kubisha kwa hoja za kuungaunga eti wao huwa hawashirikishwi eti wanaoshiriki ni wajumbe watatu. hoja dhaifu.

polisi wanaamuriwa wamkamate. mpaka hapo sikuona sababu ya kumkamata maana ardhi imeuzwa kwa makubariano ya wananchi na uongozi husika Wa mtaa na mama ana ushahidi wote.

Hizi ni siasa za kipuuzi, umefanya mauzo mbele ya watu ili kupata umaarufu lakini Nina uhakika huyo mama hata mngempeleka mahakama ya Lumumba atawagaragaza. lakini najuwa lengo lako ulitaka uonekane unatumbua ila ukweli unaujuwa huyu mama kwa maelezo pamoja na maelezo ya kuunga unga ya watu wanaomtuhumu, hana hatia

nawasilisha.
kumfurahisha mkuu kila siku lazima uwe na full mizuka ,mihemko,kujipendekeze ikibidi hata kuonea waliochini ili tu mkuu akusikie
 
Ila Natoa Ombi kwa mkuu wa kaya!

Natoa ombi kwa mhe. Rais John J P magufuli...

Mwakani wakati wa kufanya RC relocation !please tunaomba umlete RC makonda Arusha.

Sisi Arusha tunamtaka Makonda ! Please JPM ! Tuletee makonda Arusha..

Huku Arusha tunapenda wachapakazi kama Makonda
 
Mihemuko na kutaka sifa za kijinga ndo zinawaandamana viongozi HAWA
Wamama watatu wajane walovunjiwa nyumba zao kimakosa bila makonda jana wasingepata haki yao, shida yenu mnaangalia upande mmoja tu, wananchi tunateseka na viongozi wa mitaa, waache washikishwe adabu
 
Kuna thread humu ilikuwa inauliza ANACHOKIFANYA MAKONDA NI SAHIHI?"

Hatukatai makonda kufanya ziara kujua kero za wananchi wake...

Tunachukia yanayotokea kule kwenye mikutano! Tunachukia hizi siasa za chuki!

Makonda anafanya vitu with popularity image...media kibao! Drones za nini sasa? Majukwaaa makubwa kama kuna fiesta....

Hiyo hela yote ya kuleta media na majukwaa kila mahali anatoa wapi na watu wanatabu dsm?

Mara apigie Magufuli simu amuweke loud speaker! Huu ni uhuni tuu...

Mimi naangalia haya maigizo ! Kila lenye mwanzo lina mwisho...

Kila la kheri makonda na wana Dsm
Hayo maswali makonda kayajibu jana alipokua mburahati barafu, hamjui shida za wananchi shida mnazozijua za kwenye social network tu ndo mana kazi yenu kuropoka tu
 
Wamama watatu wajane walovunjiwa nyumba zao kimakosa bila makonda jana wasingepata haki yao, shida yenu mnaangalia upande mmoja tu, wananchi tunateseka na viongozi wa mitaa, waache washikishwe adabu
Mkuu hatukatai na hatupingi harakati hizo lkn ni lazma kuwe na uchunguzi zaid baada ya hapo maana inaweza ikawa ni visasi na majungu hali ambayo italeta uhasama kati ya viongoz na wananchi
 
Hayo maswali makonda kayajibu jana alipokua mburahati barafu, hamjui shida za wananchi shida mnazozijua za kwenye social network tu ndo mana kazi yenu kuropoka tu
Mkuu mimi naropoka tuu ! Nimeropoka kweli mkuu! Ila mwambie makonda aache siasa za chuki ! Aache siasa za kutafuta popularity....

Mwacheeni aendelee kutoa matamko tuu bila utekelezaji...with media around mnaona anafanya kazi...

Baada ya miezi 2 pita huko alikotoa matamko kama kuna kilichoendelea..
 
Nimefuatilia maelezo ya mama na mwenyekiti Wa mtaa aliyewekwa ndani na mkuu Wa mkoa Wa Dar es salaam nimebaini vitu kadhaa ambavyo vinasikitisha hasa katika mstikabari Wa uongozi na viongozi Wa serikali

1. maelezo yaliyokuwa yanatolewa na mama yanajitosheleza hivyo mpaka mkuu Wa mkoa anafikia hatua ya kutoa amri kwa mama Huyo awekwenp ndani sikuona sababu ya kumtia hatiani.

2. mama amekubali kuwa kiwanja kimeuzwa lakini kwa makubaliano na wananchi pamoja na wajumbe na ametaja na tarehe ambapo kulifanyika vikao vilivyobariki uuzwaji Wa ardhi hiyo.

3 mama anajaribu kumuelewesha mkuu Wa mkoa kwa umaridadi kabisa kuwa eneo limeuzwa na pesa IPO, na diwani analijuwa hill na diwani huyo alishiriki katika vikao vyote.

4. Baadhi ya wajumbe ambao wanaonekana kuwa wanachama Wa chama cha mapinduzi ( mmoja kavaa tisheti ya chagua magufuli) wanajaribu kubisha kwa hoja za kuungaunga eti wao huwa hawashirikishwi eti wanaoshiriki ni wajumbe watatu. hoja dhaifu.

polisi wanaamuriwa wamkamate. mpaka hapo sikuona sababu ya kumkamata maana ardhi imeuzwa kwa makubariano ya wananchi na uongozi husika Wa mtaa na mama ana ushahidi wote.

Hizi ni siasa za kipuuzi, umefanya mauzo mbele ya watu ili kupata umaarufu lakini Nina uhakika huyo mama hata mngempeleka mahakama ya Lumumba atawagaragaza. lakini najuwa lengo lako ulitaka uonekane unatumbua ila ukweli unaujuwa huyu mama kwa maelezo pamoja na maelezo ya kuunga unga ya watu wanaomtuhumu, hana hatia

nawasilisha.

Umeeleza vizuri ingawa kuna baadhi ya maelezo hujayaweka bayani ambayo yangeweza kusaidia kujibu maelezo yako.
1-tunaomba maelezo aliyoyatoa Afisa wa mipango miji ILALA Juu ya hulalali wa m/mtaa kujihusisha na uuzaji wa ardhi.

2-tueleze RC alisisitiza nini baada ya kuamuru m/kiti achukuliwe na police.

Tuache kutafuta point dhaifu kwasababu tu hupendezewi na mtu.
 
Back
Top Bottom