Hivi jamii ya sasa ya Tanzania kuna watu wana maadili, malezi bora, Imani na lugha za staha?

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
5,557
Reaction score
8,193
Maadili ni neno pana ila linaloeleweka kiasi kwamba ukizungumza kuhusu maadili kikawaida mtu atafikiria moja kwa moja matendo mema

Katika jamii ya sasa ya kitanzania sijui kama kuna watu wema wenye matendo mema, lugha za staha, malezi bora na mavazi ya heshima kama wapo ni asilimia chache sana. Kumejaa watu wazima wasio na utofauti na watoto au vijana wao, ni kawaida kumuona kijana mdogo akiongea matusi na mtu mzima wenyewe wakiona ni moja ya utani

Familia zimekuwa mbovu kiasi kwamba mkubwa na mdogo hawajulikani, hakuna heshima wala aibu katika maongezi yao. Maneno yaliyojaa matusi na lugha mbovu baina ya wakubwa na wadogo ndio lugha zao za kutaniana

Japo nimezaliwa miaka ya 90's lakini katika umri wangu wa utoto sijawahi kuyashuhudia ninayo yashuhudia sasa, kipindi napata akili kulikuwa na utofauti wa marika na kulikuwa na gap baina ya Marika haya ni ngumu kukuta kijana akitukanana na mtu mzima kama sehemu ya utani

Binafsi natamani nikaanzishe kanchi kangu mimi na familia yangu tukaishi huko huenda tukaishi kwa amani, maadili na tabia njema hii jamii ya sasa haiendani kabisa na malezi niliolelewa

Nawasilisha hili kwa jamii ahsanteni
 
Kauli za Kitanzania, oops sorry I meant kauli za Kizanzibari zilizopokelewa kwa mikono miwili nchini Tanganyika na kukubalika haraka kupitia agents(chawa) ni kama vile mkipatwa na msiba mnaambiwa "kifo ni kifo tu" au mkiwa na malalamiko mkadai haki mnaitwa "kenge".
Ndiyo Tanganyika yetu iliposhikishwa kwenye hizo kauli zisizo na staha.
 
Rais wa nchi mwenyewe anatukana wananchi wake..wht do u expect?
 
Hao wa zamani walikuwa na maadili gani zaidi ya kuiba mali za umma na kutuachia umasikini? Bora tuendelee kutukana.
 
Hao wa zamani walikuwa na maadili gani zaidi ya kuiba mali za umma na kutuachia umasikini? Bora tuendelee kutukana.
Sikujua mengi kuhusu siasa lakini malezi, mavazi, lugha na ustaarabu ulikuwa mzuri sana kipindi nakua kuna utofauti Sana na sasa
 
Muda huu kuna majamaa yaliyopostiwa mchana Happy Fathers Day, yapo mitandaoni yana share video za porn. Unabaki kushangaa tu , hili taifa lina watu wa ina gani
 
Sikujua mengi kuhusu siasa lakini malezi, mavazi, lugha na ustaarabu ulikuwa mzuri sana kipindi nakua kuna utofauti Sana na sasa
Hakukuwa tu na mitandao ya kijamii. Binadamu ni washenzi toka zamani sana.
 
Hakukuwa tu na mitandao ya kijamii. Binadamu ni washenzi toka zamani sana.
[/QUOTE
Haya ninayoyaona sasa ni makubwa mno kuzidi uoni wa macho yangu ukiacha hayo ya kwenye mitandao kwenye simu yangu apps ni mbili WhatsApp na jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…