MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,596
- Thread starter
-
- #21
Kigeu geu....hukitaki ukiwa nacho ila ukiona kwamba mwingine anaweza kitaka/kitamani na kukichukua unataka urudishiwe.
Ubinafsi....wakati anakusema hufai anafanya vile kujifurahisha kwa kukufanya wewe ujione duni na sio kweli anavyokuona.Ndio maana anapoona mtu mwingine anafaidi anarudi mbio kulia "nimekosa...nimekosa."
Uroho....sikutaki pia nakutaka.Hawa ndo wale wanataka raha ya kuangalia chakula na kukila pia...kitu ambacho huwezi kuwa navyo viwili moja kwa moja....na kuchagua kimoja hawawezi.
Unyanyasaji....furaha yake inatokana na kuwafanya watu wengine waamini/wajione wao sio kitu.Anakuondolea/punguza kujiamini kwako ili uwe "Mwindwaji" mzuri.Unakua sehemu ya mchezo aupendao...akitaka kufurahi anakutapika...siku akiona vipi anakuweka mdomoni na sio anakumeza.Hapa kazi inabaki weka mdomoni...tema...weka..tema ikiwa utakubali kufanywa hivyo.
Kusema ukweli binadamu wengi kama sio wote tumeumbwa na roho ya wivu bila kuacha kigeu geu.Leo hii kuna mtu anaweza kutupa ndoo asioipenda sana kwasababu imepasuka ila kesho akimuona nayo jirani yake anavyoifurahia vaada ya kuichomea karoho kanamuuma na kutamani kwenda kudai ‘ndoo yake‘. Hivyo hivyo kwa wapenzi wakati mwingine mmoja anaweza kumuona mwenzake sio ‘hadhi yake‘...‘mchovu‘...‘mshamba‘...‘amefulia‘ n.k akamwacha kwa sababu hizo ila ikitokea yule mpenzi akakutana na mtu mwingine ambaye yeye ataenda mbali na kujaribu kumuinua na akabadilisha hayo/hicho kilichofanya aaachwe mwanzo lazima yule aliyeacha atamtamani huyu ex-mpenzi alikua upgraded na kuumwa roho kwamba "uzuri wote ule anafaidi/atafaidi mwenzangu?!SITAKI KABISA" Na ndio hapo usumbufu unapoanza maana all of the sudden unaonekana u-bora na sio choka mbaya anymore.
waswahili wasema, ukiwa nacho wakiona kibaya kumbe kuna wengine wanakitamani
Kizuri ni kile ambacho huna!
...........Hii inawezekana kabisa Elyer....yaani ukiwa nacho wakiona ca kawaida na kipo lakini kikitoweka unakitaka upya!
eehh, umenikumbusha msemo wa "kutema Big G kwa karanga za kuonjeshwa..."
"huwezi jua thamani ya mtu mpaka umpoteze...!"
hahahahaha lol! Nilikuwa najiuliza Mbu leo vipi!? 🙂 mbona hayuko katika hii "sredi"? 🙂 basi nilipokuona nikabaki na tabasamu kubwa sana 🙂 Jioni njema Mkubwa.
mkali wa kukopi... Big up sm mj1 unaweza kushinda BSS.
[/FONT][/SIZE]
....ha ha ha, Bro BaK ulifikiri nishatemwa nini? LOL![/FONT][/SIZE]
we all want what we cant have.........
Grass is Always Greener on the Other Side....., lakini ukifika huko unagundua kwamba Aint no Sunshine When She is Gone...
In short watu huwa tuna-concentrate on the negatives za mtu kwahiyo tunatafuta perfect partner tunajikuta tunaruka majivu tunakanyaga moto.. kwahiyo tukishamwacha mtu na kukutana na negatives za kule tunaanza kukumbuka positives tulizoziacha, na mara nyingi tukirudi the cycle inajirudia
Umeona eeee Babu!! We take for granted vile tulivyo navyo............Instead of learning to want what we have
Speak for yourself...
Mamii nna principle yangu ambayo inaniepusha na we all want what we cant have......sikubali wala sijiruhusu kutaka kitu chochote ambacho najua fika siwezi kukipata/kuwa nacho.Iwe mpenzi...nguo..kiatu au gari...IF I CANT AFFORD IT I DONT WANT IT.HAhahahhahh Lizzy una visa!! Haya twambie mwenzetu unafanyafanyaje kuepuka vimbwanga vya kibinaadam?