Unauliwaje Kichawi? Hivi ndivyo inavyokuwa

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
39,741
Reaction score
92,197
KUULIWA KICHAWI. KULOGWA. HIVI NDIVYO INAVYOKUWA​

Na, Robert Heriel

Uliwahi kujiuliza, inakuwaje mtu yupo Mwanza lakini analogwa na mtu aliyepo Dar es Salaam, au kinyume chake, au mahali popote pale?
Uliwahi kujiuliza inakuwaje mtu yupo Kigoma lakini akitaka kumuona mtu aliyepo Arusha akaenda kwa Mganga wa kienyeji anamuona, uliwahi kujiuliza sanaa hiyo au sayansi hiyo?

Leo tutajadiliana kwa kifupi sana, kuhusiana na jambo hili. Nafikiri kila mmoja ataelewa kulingana na urefu wa fikra zake.

Twende sasa.

Mtu ni kiumbe ambacho kimegawanyika katika sehemu tatu.

1. Mwili (Nafsi ya nje)
2. Kobu (Nafsi ya ndani)
3. Roho

Mambo hayo matatu yakiwa pamoja huitwa ZOKO na ndio huunda kiumbe aitwaye Mtu yaani mimi na wewe.
Mambo haya hushirikiana kwa pamoja na kumfanya mtu awe vile alivyo. Roho ndio msingi wa vyote. Roho hukaribiana na Kobu(Nafsi ya ndani) Kuliko mwili. Na Kobu hukaribiana na Mwili kuliko Roho.

Ukiudhuru Mwili, haiwezi kuleta madhara kwa KOBU, Lakini ukidhuru Kobu basi mwili wa nje huweza kuwa mashakani. Lakini ukidhuru Roho basi unadhuru Mwili na Kobu.

1. MWILI (Nafsi ya nje) HARDCOPY

Mwili hujengwa na mambo yafuatayo
1.1. SELI
1.2. Tishu
1.3. Ogani
1.4. Mfumo wa Ogani
1.5. Kiumbe chenye mwili.

Kikawaida Seli ndio kizio kidogo cha maisha ya mwili, yaani mwili huanza kuchomoza kuanzia kwenye seli. Wote tunafahamu kuwa sisi ni matokeo ya muunganiko wa Mbegu ya Kiume (XY) au (Y) na Mbegu ya kike X Ambazo ni seli. Zipo pia seli za damu zikiwemo Limfu(Lymphocyte), plasma, na seli nyekundu za damu(Haemoglobin)

TISHU (Tissue) ni seli za aina moja ambazo zinakusanyika kwa pamoja kufanya kazi maalumu katika kiumbehai. Kisha viungo vinaundwa kwa muunganiko wa tishu mbalimbali. Kwa mfano wa Tishu ni damu.

OGANI ni viungo maalumu kwenye mwili vinavyofanya kazi mahususi. Kwa mfano kuna Ogani za milango ya fahamu kama Macho, pua, Ulimi, Ngozi, na masikio. Ili Ogani ifanye kazi lazima seli ziwe hai. Ushirikiano wa ogani unaofanya ogani ifanye kazi unaunda kitu kinaitwa mfumo wa ogani, kama vile mfumo wa ufahamu, ambao unatawaliwa na ogani iitwayo Ubungo, mfumo wa damu unaotawaliwa na ogani iitwayo Moyo, mfumo wa kuona, macho, mfumo wa mkojo, figo, mfumo wa upumuaji, mapafu n.k

Mifumo hii lazima ishirikiane ili mwili uwe salama.

Mwili ni HARDCOPY Kwenye ZOKO yaani kwa kiumbe aitwaye Mtu. Mwili huwa sehemu moja kwa wakati mmoja

2. KOBU (Nafsi ya ndani) SOFYCOPY

Hii ni sehemu ya mtu ambayo ipo ndani ya mtu. Sehemu hii ndio msingi wa sehemu wa nje. Bila Kobu hakuna Mwili, lakini Kobu anaweza kuwepo pasipo Mwili. Hata sasa Kobu ndiye anayesoma makala hii ingawaje akisaidiwa na macho yaliyopo mwilini. Kobu ambayo ni nafsi ya ndani huhusisha, fikra, akili, ufahamu, mihemko, n.k.
Kunayo mahusiano ya karibu baina ya Kobu na mwili, kwa sababu Kobu ndio huunda mwili.

Kobu ndio Mtu halisi. Na mada yetu itajikita hapa. KOBU ni kama Softcopy ipo kila mahala.

3. ROHO

Hii ndio chanzo kikubwa cha vyote viwili ambavyo mtu anavyo, mwili na Kobu. Roho ipo mbali zaidi ya mwili lakini inaikaribia Kobu yaani nafsi ya ndani.
Roho ikiusogelea Kobu, Mwili huzimia kwa mudahalikadhalika Roho ikikaa mbali na Kobu pia mwili hufa au kuzimia.
Roho huwa katika mifumo ya kiungu ambapo Miungu yenye nguvu ndio hujua habari zake.

MTU ANALOGWAJE AU ANAULIWAJE KICHAWI?

Uchawi upo wa aina nyingi hasa ule wa kumloga mtu mpaka alogeke yaani apate madhara hasi au chanya.

AINA ZA UCHAWI KATIKA KULOGWA

1. Uchawi wa kuloga mwili
2. Uchawi wa Kuloga Kobu.

Uchawi wa Kuloga mwili ni ule uchawi ambao mtu huenda kumfanyizia mtu ulozi kwa mganga au kwa wachawi au watu wote wenye sanaa ya uchawi na kumpa madhara hasi au chanya.

Uchawi huu huzingatia zaidi miti shamba, madini, ngozi, vimiminika n.k Vitu hivyo hutumiwa kulogea mtu apate madhara hasi au chanya.

Uchawi huu unaweza usitumie hata viumbe wa rohoni yaani majini kwa aina zake, mizimu kwa aina yao, Deva kwa aina zake, n.k
Hapa mganga anaweza kukupa majani ambayo ni sumu akakuambia ukifika yaweke kwenye maji yake ya kuoga, chai, chakula. Au anaweza kukupa kitu akakuambia kivae mwilini ambacho kitu hicho kikawa kinga kwako, kutegemeana na mchanganyiko wa kitu hicho na vitu vinavyozuiwa na kitu hicho.

Pia Uchawi huu hutumika kwa waganga wanaoagua watu ambao ukifika kama unaumwa ugonjwa fulani basi utamuelezea Mganga kisha atakufukiza kwa mchanganyiko wa dawa kulingana na kisomo chake. Au atakupaka madawa aua atakupa dawa unywe. Uchawi huu hata usipotumia majini unaweza kufanyika tuu. Muhimu Mganga awe na uelewa wa kuagua(Ku-diagnosis) na kutambua ugonjwa uliopo mwilini na jinsi ya kuuondoa na dawa.

Mtu anayelogwa kimwili Nafsi yake haiwezi kupata madhara, atateseka tuu kimwili kutokana na sumu za kichawi alizopewa.

2. UCHAWI WA KULOGA KOBU

Huu ndio uchawi halisi na wenye nguvu. Ambapo kinachologwa ni nafsi na wala sio Mwili.
Hapa Mganga au mchawi huweza kumtupia Ulozi mtu hata akiwa marekani.
Uchawi huu huhusu nafsi ya ndani ya mtu.

Mtu atampigia mtu Ramli na kumsoma mtu amtakaye kumloga.

Katika somo lililopita nilieleza kuwa Hakuna Mwanadamu anayelindwa na Malaika. Malaika hatembei na mtu bega kwa bega. Malaika sio Bodyguard. Na katika masuala ya Kobu na kiroho mtu halindwi kila sehemu yaani bega kwa bega. Hata katika uchawi hakuna majini yanayolinda watu.

Kitakachofanyika Mganga ataangalia kama Mtu anayetaka kumloga kuwa ameshajisajili kwenye mifumo ya kichawi, yaani Database ya kichawi. Na kama amejisajili basi itakuwa rahisi kwake kumloga hata angekuwa yupo wapi. Kitakacho hitajika ni kibali tuu ambacho mhusika atapewa masharti kadhaa akiyaweza basi unalogwa kama tuu upo kwenye Database ya kichawi.

Kumbuka Nafsi ya ndani(Kobu) ni Softcopy yaani ipo kila sehemu. Ipo hivi.
Mimi Taikon kwa sasa Nipo Dar es Salaam kimwili lakini nafsi yangu ya ndani ipo popote duniani. Yaani aliyepo Kigoma akiamua kuiona anaweza kuiona na kuifanya chochote kama ataiona haina kinga.

Nafsi ya ndani ni kama Laini ya simu, au simu, kuna Softcopy na hardcopy. Simu uliyoishika na laini uliyonayo ni hardcopy, TCRA wanauwezo wa kuifunga simu yako au laini yako isifanye kazi ingawaje wao wapo Dar es salaam na wewe upo Tandahimba huko Mtwara. Hii ni kwa sababu wewe unahardcopy ya simu lakini wao wanasoftcopy ya simu yako.

Kwa nini wanaweza kuzizima, ni kwasababu wamezisajili na kuzihifadhi code za softcopy ya simu yako. Hata wenye makampuni ya uzalishaji wa simu kama vle Samsung, Itel, Tecno wakiamua usiitumie hiyo simu yako sasa hivi wanaweza kuifunga na ikawa haifanyi kazi.

Hii pia ipo kwenye Uchawi. Nafsi za ndani zote zimehifadhiwa katika Database ya Muumbaji yaani Mungu. Lakini Wachawi huzidukua na kuzisajidili kwenye mifumo yao ya kichawi kwa ajili ya matumizi yao ya leo na baadaye.

Waganga wengi ukifika lazima wachukue damu yako kwa namna mbalimbali, namna maarufu ni kukuweka chale, hapo akishachukua damu atachukua Vinasaba vyako(DNA) Kufikia hapo utakuwa umesajiliwa rasmi kwenye mifumo ya kichawi.

Mtu yeyote akitaka kukuloga kama umeshajisajili kwenye mifumo ya kichawi atafanikiwa tuu labda ashindwe kwenye ukataji wa vibali cha kukuloga kutokana na masharti.

Ukishasajiliwa kwenye mifumo ya kichawi basi hapo huna ujanja. Unaweza kupigwa na yeyote kutoka popote. Yaani mtu yupo Dodoma anakupiga wewe uliyepo Mwanza na unakaa.

Mbinu kubwa za kuzuia usajili kwenye mifumo ya kichawi

1. Kutoenda kwa waganga wa kienyeji na kuchukuliwa damu, nywele, kucha au jambo lolote linaloweza kufanya Vinasaba vyako vikachukuliwa

2. Kuacha uzinzi kwani, shahaw/ manii, na maji maji yanayotoka ukeni huchukuliwa na mawakala wa kichawi wa ngazi ya kata walioko eneo utakalofanyia ufuska

3. Kumuamini Mungu sana na kuzishika sheria zake

4. Kama humuamini Mungu basi nenda kwa mganga aliyebobea katika masuala ya uchawi akakuzike kaburini siku tatu au saba ukiwa ndani ya kaburi kisha ukitoka basi yeyote atakaye kukuloga hatakuona kwenye mifumo ya kichawi bali ataona ulikufa miaka mingi iliyopita.

Wachawi wakishaiteka nafsi yako huweza kukufanyia lolote watakalo. Huweza kukuletea sanaa ya kifo na watu wakakuona umekufa wakakuzika kumbe wewe upo unadunda katika falme za kichawi.

Kiroho katika falme za kimungu, Sanaa ya kifo aliifanya Yesu pale Msalabani. Yesu hakuuawa, bali alifanya sanaa ya kifo pale msalabani, watu wakamuona amekufa lakini yeye mwenyewe hakuwepo aliondoka na kuelekea kuzimu kwenye nafsi zilizokufa zamani.

Mtume Petro anakuambia, Yesu alipokufa Msalabani(Sanaa ya kifo) hakufa kikamilifu, bali alishuka mpaka kuzimu akazihubiri roho zilizokufa zamani

1Petro 3:
18 Maana Kristo pia alikufa mara moja tu kwa wakati wote; mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili atulete kwa Mungu. Mwili wake uliuawa lakini akafanywa hai katika roho yake. 19 Naye akiwa katika roho alik wenda kuhubiria roho zilizofungwa kifungoni.

Hii ni kusema wapo wanakufa kwa mapenzi ya Mungu na wapo wanaokufa kwa ushirikina na kuwekwa kifungoni wakitumikishwa na wachawi mpaka siku yao ya kufa iliyopangwa na Mungu itakapofika.

Muhimu: Ili uchawi usikuchezee ni lazima uwe nje ya mfumo wa kichawi. Yaani uwe haujasajiliwa.

Kwa leo niishie hapa. Acha nipumziike sasa.
 
Umesema kifupi sana, sasa mbona ndefu sana
 
Lengo lako tumelijua, na hatuokoki ng'ooo😂😂😂😂
 
Safi sana kiongozi, kalibu tena...
 
Nakubaliana na pande tatu za mwanadamu ; mwili, nafsi na roho na kwamba mtu anaweza kuloga mwili au hata nafsi lakini sio roho kwani hii ni pumzi ya Mungu ndani ya mwanadamu haifi wala hailogeki. Nafikiri pia nafsi ya mwanadamu haipo kila mahali, pia nafsi ya viumbe kama malaika, au viumbe vya giza kama majini, au mashetani hazipo kila mahali. Nafsi iliyopo kila mahali ni ya Mungu Mwenyezi pekee. Viumbe vingine vyote husafiri kwenda sehemu mbalimbali kwanda mwendo unaotofautiana. Ndio maana wachawi waweza kuruka kwa ungo na majini husafiri huku na huko kukusanya taarifa. Simu za kiroho zipo na zinaweza kupigwa na kupata taarifa ndani ya muda mfupi sana kama iliyo simu za kawaida au hata kwa kasi zaidi.

Hakuna njia ya kujikinga na kazi za nguvu za giza isipokuwa kwa nguvu kinzani yaani nguvu ya Mungu Mwenyezi pekee. Namna nzuri na yenye nguvu sana ni kwa kupitia nafsi ya Yesu Kristo pekee. Kazi zote za waganga wa kienyeji kama vile uponyaji na miujiza hufanywa kwa msaada ya mapepo/majini ukiachilia zile za asili ambazo mtu yeyote anayetumia akili anaweza kufanya kama vile kujua mzizi ambao ni dawa na kumpatia mgonjwa. Unaweza kukata mawasiliano au connection za mapepo kwa kujiunganisha na Yesu Kristo kwa toba, kukiri utu upya, kuacha dhambi na kwa sala/maombi. Ni maisha ya raha sana kuwa huru ndani ya Kristo Yesu nakiri kwamba wengi hawajui jambo hili na ni eneo la vita vya kiroho.
 
Mimi swali langu nikwamba? Kwanini wachawi wanaingia ndani kichawi uchi yaani usiku wakija kukufanyia michezo michafu
 
mie nisaidie swali hili, kwa nini wachawi hua hawaugui haya maradhi ya homa mara kichwa, je wao wamesalimikaje na haya maradhi maana ni ngumu sana kusikia mtu anaesemekana ni mchawi kalazwa hospital
 
Nguvu za giza zipo, lakini hazina nguvu mbele ya Bwana Yesu.
Yesu ni nguvu original, mwanzo na mwisho.
 
mie nisaidie swali hili, kwa nini wachawi hua hawaugui haya maradhi ya homa mara kichwa, je wao wamesalimikaje na haya maradhi maana ni ngumu sana kusikia mtu anaesemekana ni mchawi kalazwa hospital
Aisee
 
Kama mtu ameshalogwa atajitibu vipi? Miaka ya nyuma niliwahi kupelekwa Kwa mganga kuuawa lakin mganga alishindwa na pia nikaanza kusikia vitu vinatembea mwilini kwenye mishipa ya damu
 
Back
Top Bottom