kuna ukakasi mwingi sana kwenye maneno ya huyo mama mtoto..
MOJA:
anajiita housegirl kwa kufanya kazi ya kulea mtoto wake. kazi ya kulea mtoto sio ya housegirl ni ya mama Mzazi. House girl anasaidia kama mama anatoka anaenda kazini.
PILI:
anataka apongezwe kwa kazi ya kulea mtoto, kitu ambacho ni cha ajabu sana. wewe unalea mtoto unataka zawadi. mimi ninaehangaika kutafuta hela ya pampas, unga wa mtoto, kulipia bima ya mtoto, kununua dawa, mbona siombi zawadi? mimi nani anatakiwa anipe zawadi? wewe pekee ndo una majukumu kwa huyo mtoto na mimi vyote ninavyofanya ni kazi bure na havina mashiko?
TATU:
akumbuke kila mtu kwenye familia ana wajibu wake na inabidi awajibike kwa kadiri ya uwezo wake.
baba analeta ugali mama analea watoto. yeye anamshukurugi mumewe kwa kuleta chakula kila siku? kwamba hakuna hata siku amelala njaa, ameshawahi kumshukuru mumewe kwa hilo?
Wanawake muangalie na mambo ya kunung'unikia vitu vingine ni wajibu wenu kuvifanya na havihitaji pongezi wala kupigiwa makofi.