Hivi huyu ni Dr. Charles Kimei wa CRDB ninayemfahamu au wa leo labda alikuwa ni Pacha wake?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,570
108,911
Dr. Charles Kimei hasa yule wa kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2015 na ambaye hata Mimi GENTAMYCINE nilikuwa namkuabali sana alikuwa mwenye Sifa zifuatazo:
  1. Makini
  2. Anajiamini
  3. Hayumbishwi
  4. Hatishwi
  5. Jeuri wa Kitaaluma na Kiuweledi
  6. Mchangamfu
  7. Amejawa mipango tupu ya Kimaendeleo
ILA

Dr. Charles Kimei huyu wa kati ya mwaka 2015 hadi huu wa 2018 na ' hasa hasa ' huyu niliyemkodolea / niliyemtizama leo akitiririka na kuserereka kutokea Kanda ya Ziwa kiukweli amenitisha kama pia siyo kunisikitisha hasa kwa jinsi alivyokuwa. Kimei wa leo alikuwa:

  1. Anaongea huku muda mwingi akijitetea
  2. Anasifu mno hata pale ambapo Sifa hazikustahili
  3. Anafumba na kufichaficha sana mambo
  4. Anaongea kwa Uwoga huku muda mwingi akitetemeka
  5. Zungumza yake muda mwingi ilikuwa ni ya Kutunga matukio tupu
  6. Ni mwenye kutia huruma kama siyo simanzi sana
  7. Alikuwa analazimisha mno kuaminika Kimaelezo hasa kwa yule aliyekuwa akimuelezea
Nini kimemkumba Dr. Charles Kimei?

Nawasilisha.
 
Kamuulize Manji,Rugemalila,Singasinga wanajua siri hio.

Hao ndiyo wamemfanya awe hivyo au? Sijakuelewa hapa Mkuu hebu niweke sawa ili nami nijue kwani huyu Mzee Dr. Kimei leo amenishtua sana ukilinganisha na vile nilivyokuwa nikimfahamu huko nyuma / kitambo.
 
Kuna theory flani hivi wapumbavu wanayo.

Huamini walionacho wakizidi kutajirika basi jamii huwa maskini zaidi.

Ila ukifuatilia kwa undani, matajiri wakiongezeka utajiri wao kwa kiasi flani huelekea jamii kwa njia mbali mbali kama kodi kuongezeka, ajira, misaada, uboreshaji wa huduma na bidhaa sokoni, vipato kuongezeka nk

Huyu wetu anaamini kama kundi lile la kwanza(hususani ujamaa)
 
Mkuu watu wanaangalia upepo una vuma Upande upi na Kuufata wewe ukienda nao Against basi tegemea Chombo chako kupotea njia, Mtu smart na master mind kama kimei ni mjanja na Anaishi kwa Kufata Hali iliyopo ili aweze kusurvive, Apa namkumbuka Darwin na Mambo yako ya Survive for the fittest
 
Kweli mkuu, "you cant make the poor rich (stronger) by weakening the rich"
 
Hao ndiyo wamemfanya awe hivyo au? Sijakuelewa hapa Mkuu hebu niweke sawa ili nami nijue kwani huyu Mzee Dr. Kimei leo amenishtua sana ukilinganisha na vile nilivyokuwa nikimfahamu huko nyuma / kitambo.
hivi mkuu hujajiuliza kwanini amesema mwaka huu anataka astaafu na hataki kuongeza tena mkataba?
na hujiulizi kwanini amesema raisi ndiye kafanya utafiti kuhusu ujenzi wa bank kule chato na sio wao crdb?
 
  • Anaongea huku muda mwingi akijitetea
  • Anasifu mno hata pale ambapo Sifa hazikustahili
  • Anafumba na kufichaficha sana mambo
  • Anaongea kwa Uwoga huku muda mwingi akitetemeka
  • Zungumza yake muda mwingi ilikuwa ni ya Kutunga matukio tupu
  • Ni mwenye kutia huruma kama siyo simanzi sana
  • Alikuwa analazimisha mno kuaminika Kimaelezo hasa kwa yule aliyekuwa akimuelezea
Msamehe bure ata wewe ungekuwa hivyo. Jamaa aliyekaribu nae anabadirika kama kinyonga hatabiriki.
 
Mkuu watu wanaangalia upepo una vuma Upande upi na Kuufata wewe ukienda nao Against basi tegemea Chombo chako kupotea njia, Mtu smart na master mind kama kimei ni mjanja na Anaishi kwa Kufata Hali iliyopo ili aweze kusurvive, Apa namkumbuka Darwin na Mambo yako ya Survive for the fittest

Kwahiyo unataka kuniambia kwamba na Yeye kumbe kuna sehemu kabanwa mbavu ya ' Kiuchumi ' hivyo hafurukuti?
 
hivi mkuu hujajiuliza kwanini amesema mwaka huu anataka astaafu na hataki kuongeza tena mkataba?
na hujiulizi kwanini amesema raisi ndiye kafanya utafiti kuhusu ujenzi wa bank kule chato na sio wao crdb?

Hakika Dr. Charles Kimei wa leo ndiyo amenithibitishia kwamba hakuna Watu ' Wanafiki ' duniani na pengine hata kule Mbinguni kama Watanzania.
 
Msamehe bure ata wewe ungekuwa hivyo. Jamaa aliyekaribu nae anabadirika kama kinyonga hatabiriki.

Hivi kumbe Mtu unaweza ukawa Msomi kabisa tena wa Kiwango cha juu na Kimataifa na Mweledi wa Kutukuka na bado tena ukawa Mwoga / Nyali? Mimi nilidhani PhD na PhD haziogopani Mkuu kumbe kuna PhD ya Mwanamume na PhD ya Mwanaume au Mvulana?
 
Dr. Charles Kimei hasa yule wa kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2015 na ambaye hata Mimi GENTAMYCINE nilikuwa namkuabali sana alikuwa mwenye Sifa zifuatazo:
  1. Makini
  2. Anajiamini
  3. Hayumbishwi
  4. Hatishwi
  5. Jeuri wa Kitaaluma na Kiuweledi
  6. Mchangamfu
  7. Amejawa mipango tupu ya Kimaendeleo
ILA

Dr. Charles Kimei huyu wa kati ya mwaka 2015 hadi huu wa 2018 na ' hasa hasa ' huyu niliyemkodolea / niliyemtizama leo akitiririka na kuserereka kutokea Kanda ya Ziwa kiukweli amenitisha kama pia siyo kunisikitisha hasa kwa jinsi alivyokuwa. Kimei wa leo alikuwa:

  1. Anaongea huku muda mwingi akijitetea
  2. Anasifu mno hata pale ambapo Sifa hazikustahili
  3. Anafumba na kufichaficha sana mambo
  4. Anaongea kwa Uwoga huku muda mwingi akitetemeka
  5. Zungumza yake muda mwingi ilikuwa ni ya Kutunga matukio tupu
  6. Ni mwenye kutia huruma kama siyo simanzi sana
  7. Alikuwa analazimisha mno kuaminika Kimaelezo hasa kwa yule aliyekuwa akimuelezea
Nini kimemkumba Dr. Charles Kimei?

Nawasilisha.
Inawezekana ulimkubali pale tu mawazo yake na yako yalishahabiana. Ila kwa leo yametofautiana, human being is a rational being. Hamuwezi kukubalina maono kila siku. Ubinadamu ni kukubali katika kutofautiana. Yawezekana hajakumbwa na kitu bali hivyo ndivyo anavyoamini na yeye anawashangaa wasio na mawazo kama yeye, 'wamekumbwa na nini?'
 
Back
Top Bottom