Hivi hii tabia ya mataifa yenye nguvu kupigania kwenye mataifa mengine na kuya haribu wakati kwao kukiwa salama ita isha lini jamani?

RTI

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2018
Messages
1,009
Points
2,000

RTI

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2018
1,009 2,000
Kama kichwa cha habari kinavyo sema,imekuwa ni desturi kwa mataifa yenye nguvu kuyatumia mataifa dhaifu kuoneshana umwamba hivyo kuyaharibu mataifa husika na kuwahangaisha raia wake.

Mfano mzuri ni kinacho endelea ndani ya ardhi ya Iraq kati ya Iran na marekani, baada ya kupigania nchini sirya na kuhiaribu vibaya sana nchi hiyo, sasa vita kati yao wamevihamishia nchini Iraq.

Nahili tukio la marekani kumuua kamanda wa kiirani ndio kabisa limeharibu mambo hapa naona damu za wairaq zikimwagika kwa masilai ya marekani na Iran,yaani wao hawajari ya kwamba vitendo vyao vinasababisha mamilioni kukosa makazi, kuteseka kwa njaa,kufa wao wanacho jari ni masilai ya mataifa Yao.

Wakati marekani na Iran wakisambaza silaa nchini Iraq na sirya zinazo sababisha maelfu kuawa na mamiliomi kukosa makazi wao kwenye nchi zao kupo salama na raia wao wanaishi kwa amani.

Mifano mingine ni Iran vs saudia nchini Yemen,Urusi na Marekani nchini Ukiraini, na sasa hivi nasikia wanataka kuhamia libya na Uturuki inataka kutuma wanajeshi nchini humo yaan inasikitisha sana.

Dah dunia hii haina usawa kabisa yaan raia wa taifa moja wana teseka kwa ajili ya mataifa mengine kwa sababu tu taifa lao halina uwezo wa kijeshi.

Kwakweli sisi tunao ishi kwenye mataifa ambayo bado ni dhaifu hatuko salama hata kidogo sisi ni wakimbizi watarajiwa ni suala la muda tu.

La msingi ni kuomba mungu na sisi tusije jikuta katikati ya hawa wanaojiita wababe wa dunia.
Maana wao hawajari hata mfe mamilioni,ili mradi tu masilai yao yasi athiriwe yaan inasikitisha sana tena Sana.
 

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
2,947
Points
2,000

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
2,947 2,000
Dunia inajiendesha katika mfumo huo tangu enzi na enzi.

Hilo halitakaa libadilike, si leo wala kesho as long as kuna uwepo wa binadamu katika Dunia yetu hii.

Kila mmoja ana matamanio ya kuwa in control katika ulimwengu huu ili kujihakikishia usalama wake na maslahi yake kwa ujumla. (No Peace)

Kulifanya hilo liwezekane, unahitaji kuwafanya wale walioko karibu yako kuwa dhaifu as soon as possible kabla ya wao hawajafanya the very same thing to you. (No Trust)

Hapo ndipo uvamizi wa hapa na pale unapokuwepo na utaendelea kuwepo huku ukiwafanya wenye nguvu kuwa na nguvu zaidi na wale dhaifu wakiendelea kuwa dhaifu wasijue nini cha kufanya zaidi ya kuyafuatisha maamuzi ya wenye nguvu kuwa yao.

The stronger make the rules and they do so to their own advantage. (No Equality)

So, you choose, uwe na nguvu utawale ama uwe dhaifu utawaliwe kwa namna moja ama nyingine. There is no in between, no compromise. Huo ndio msingi wa maisha ya Kidunia.
 

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
11,164
Points
2,000

dudus

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
11,164 2,000
Habari inayo trend kwa sasa ni Kamanda Mkuu wa vikosi vya mapinduzi ya Iran Quds; mtu wa pili kwa nguvu na sauti Iran akitanguliwa na Ayatollah tu Generali (kwa rank za Iran) Qassemi Sleiman kuuliwa kama kuku hizo nyingine stori tu za kufurahisha kijiwe. Rais Trump kaamua kutoa zawadi ya kuanzia mwaka.
 

RTI

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2018
Messages
1,009
Points
2,000

RTI

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2018
1,009 2,000
Habari inayo trend kwa sasa ni Kamanda Mkuu wa vikosi vya mapinduzi ya Iran Quds; mtu wa pili kwa nguvu na sauti Iran akitanguliwa na Ayatollah tu Generali (kwa rank za Iran) Qassemi Sleiman kuuliwa kama kuku hizo nyingine stori tu za kufurahisha kijiwe. Rais Trump kaamua kutoa zawadi ya kuanzia mwaka.
Jikite kwenye mada.
 

Forum statistics

Threads 1,390,211
Members 528,114
Posts 34,046,065
Top