Vita ya Urusi na Ukraine: Akili na malengo ya Putin nchini Ukraine

Dr Count Capone

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
1,875
3,234
Na Jumaa Kilumbi,
Katika andiko hili fupi ningependa kutahadharisha kuwa hatutazungumza kiitikadi, kinafki wala kihisia, hatutazungumza mambo yanavyopaswa kuwa tutazungumza mambo yalivyo, tutazungumza kwa kuangalia ‘practical result’ na uhalisia tunaamini na tunafahamu dunia haiendeshwi kwa hisia bali kwa kanuni na misingi yenye kuleta matokeo.

VITA NI SEHEMU YA MAISHA YA MWANADAMU TANGU KALE
Vita zimekuwa ni sehemu ya maisha ya wanadamu tangu kale jamii zilikua zikivamiana kuibiana mifugo na mali na wakti mwingine kufanyana watumwa, Vita zimekuza himaya kubwa kuwahi kushuhudiwa duniani ikumbuke Dola ya Ugiriki, zimekuza chumi kubwa kumbuka uchumi wa Uingereza, zimeibua matajiri duniani unamkumbuka David Ricardo? Hivyo vita ni sehemu ya maendeleo ya mwanadamu ndio maana mpaka leo hata nchi zenye sera za ‘ki-pacifism’ bado wana kiwango fulani cha jeshi kuonesha hawapuuzi uwezekano wa vita maana ndio asili ya mwanadamu.
Ni muhimu kuelewa kuwa kwenye Vita zote kumekuwa na makundi ya aina mbili ya watu,

Moja, ni wale tunaowaita ‘Policy makers’ kundi hili wamo viongozi wa nchi wanaojua siri na misingi ya kuendesha nchi nawazungumzia Mawaziri, Waziri mkuu, Wakuu wa majeshi, wafalme na maRais wenyewe, hawa hawaongozwi kihisia, kwao nchi ndio kipaumbele chao, Usalama ndio hazina yao na watu ndio mitaji yao. Linapokuja suala la vita kundi hili litapinga au kuunga mkono kutokana na athari za vita hiyo kwa usalama wa nchi aidha ziwe hasi au chanya.

Kundi la pili, tunawaita ‘maamuma’ kundi hili lina watu wengi sana hapa wamo wananchi wa kawaida, viongozi wa dini na wote ambao hawako katika nafasi nyeti za nchi. Wao watapinga vita ikiwa wanaona watapata madhara moja kwa moja na misimamo yao inatengenezwa na ‘propaganda’ za serikali au vikundi vyenye ushawishi kwenye jamii, na wataunga mkono vita vilevile kutokana na ‘propaganda’ za watu za watu wenye ushawishi. Hawa hawaamini kuwa vita yaweza kuhalalishwa ila katika misingi ya kujilinda tu.

URUSI HAINA CHAGUO “DUMB IF THEY DUMB IF THEY DON’T”
Kama alivyowahi sema Jenerali na mwanamikamati wa Prussia Karl von Clausewitz “Vita ni muendelezo wa siasa katika namna nyingine”

Hii vita ya Ukraine na Urusi ni matokeo ya kushindwa kwa mazungumzo baina yao na nchi za Magharibi na Ukraine yenyewe. Ilipoanguka USSR miaka ya 1990 NATO waliihakikishia Urusi kuwa hawatojipanua wala kupokea wanachama wapya toka Ulaya mashariki ambapo Urusi huona ni kama kibarazani kwao. Moja ya kauli mashuhuri sana ni ile “Hata inchi moja mashariki” aliyoisema bwana James Baker (aliyekuwa katibu wa nchi wa Marekani). Ahadi zao zilikua ni maneno ya kilaghai kuwapumbaza Urusi huku wakijipatia ‘advantage’ kwa kufanya kinyume na ahadi zao.

NATO wamembana mbavu Putin, wamemuacha hana chaguo akiiacha Ukraine itajiunga NATO na akiivamia anawekewa vikwazo. Urusi hawataki NATO iwe kubwa, hawataki majirani zake wawe wanachama, hawataki kuona silaha na majeshi ya kigeni karibu na mipaka yao, hawataki kuona wanazingirwa kila pande. wanavyojisikia ni kama walivyojisikia Marekani mwaka 1962 walipowekewa nyuklia jirani kabisa pale Cuba, mpaka sasa NATO wameshawazunguka kwa upande wote wa magharibi wamebakisha Ukraine tu kumaliza mzunguko wao. Urusi wanajua hilo wamejipanga kuhakikisha kamwe halitokei na wanafanikiwa.

Madai haya ya Urusi yanawapa uhalali wa hii vita kimkakati japo vichwani mwa watu wengi kutokana na ushawishi mkubwa wa waMagharibi wanaona Urusi ni wagomvi wasio na huruma. Urusi itakua hatarini kama wataacha mambo yaende kama yalivyo, japo awali walijaribu Diplomasia kwa miaka zaidi ya 20 imeshindikana sasa ni wakti wa kutumia mabavu.

Kwenye siasa za kimataifa hii ni kawaida diplomasia inaposhindikana nguvu huwezekana, Marekani ya leo iliundwa baada ya Vita dhidi ya Uingereza na baadae ya wenyewe kwa wenyewe, Uingereza ilidumu kama kinara wa dunia kutokana na vita nyingi alizopigana ulimwenguni kote, Ujerumani isingekua hivi kama sio vita ya kuwaunganisha Wajerumani wote, Italia kamwe isingekua moja kama sio vita ya kuunganisha miji yao yote, Uhispania ingekua ya Waarabu kama sio vita Iliyopigwa Iberia kote.

Vivyo hivyo Saudia bila kupigana na Ottoman kamwe isingekua nchi tunayoijua leo, Ottomani bila umahiri wa kivita wasingeweza kutawala dunia, China bila vita wasingekuwepo walipo leo, Japan bila vita ya muda mrefu wasingefika hatua ya kuwa tishio kwa dunia, mifano iko mingi lakini ieleweke wazi kuwa maendeleo ya kisiasa kwa sehemu yamechangiwa na vita.

Hii vita kama yalivyo mambo mengine haipiganwi bila kulipia gharama, na gharama hii haiji kama fedha tu la, watu wamekufa, miundombinu inaharibika, chumi zinatetereka, vikwazo vinaongezeka na taswira ya Urusi inaharibika, ndio na hiyo ndio gharama za kuhakikisha Urusi inakuwa salama. Vita hii si tu inatuma ujumbe kwa NATO kuwa Urusi hawataki kuchezewa pia inaweka bayana wako ‘serious’ kiasi gani linapokuja suala la usalama. Watu huweza dhani wamekurupuka lakini huu ni mpango wa muda mrefu, walijua hii siku itafika na NATO walijua hii siku inakuja.

Wakati NATO na washirika wao wanaiadhibu Urusi kwa vikwazo, nchi inayoshika nafasi ya pili kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani China ipo tayari kuisaidia Urusi kuepuka vikwazo mpaka sasa tayari wameshasaini mkataba wa ‘ushirikiano bila kikomo’ sasa bidhaa zote zilizowekewa vikwazo ulaya zitauzwa China. Madai yao na Taiwan yanakaribia kufanana na ya Urusi kule Ukraine, hivyo China inaufanyia kazi ule msemo wa kiswahili unaosema “wema hauozi”, kwa maana ndani ya muda mchache nao watakua kwenye harakati za kuichukua Taiwan na watahitaji mshirika wa kuwaunga mkono, mshirika gani bora kuliko yule anaeongoza kwa mabomu ya nyuklia?

India nchi ambayo 60% ya silaha zake zinatokea Urusi hawajalaani wala kuungana na waMagharibi kuwawekea vikwazo sababu wanaelewa waMagharibi sio watu wa kuaminika, Brazil moja ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi wamejitenga na vikwazo dhidi ya Urusi. Africa pia hatuko nyuma kwa kuzingatia kuwa nusu ya silaha zote Africa zinatoka Urusi tumeamua kuwa ‘neutral’ na kutoweka vikwazo kwa Urusi katika mzozo wa huu tangu 2014.

Wakati dunia inailaumu Urusi kwa kinachoendelea inasahau kua Vita hii ni kama ya Marekani kule Iraq 2003 ni kama ile ya NATO nchini Libya mwaka 2001, ni kama ya Israel kule palestina tangu mwaka 1948, ni kama ya Ufaransa Algeria miaka ya 1950. wote wanapambania maslahi ya mataifa yao wote wanahakikisha usalama wa mataifa yao japo kwenye michakato hiyo vita haikwepeki na ndio asili ya mambo, Duniani vitu vyote ni vichache upatapopata jua kuna mtu kakosa, upotezapo jua kuna mtu kapata hatuwezi kushinda wote, ni aidha unashinda au unapoteza hakuna sare katika mchezo wa maisha.

NINI HATMA YA URUSI NCHINI UKRAINE?
Kimkakati haitawezekana kwa Urusi kuikalia Ukraine kwa nguvu (occupation) kwa muda mrefu na hii ni kutokana na sababu kuu mbili;

Moja, Warusi wameshindwa kupata ‘sapoti’ ya kutosha toka kwa raia wa Ukraine wenyewe. Kama alivyosema Machiavelli baba wa sayansi ya siasa kuwa unapovamia nchi ya kigeni ni lazima uigawe ili uitawale, lazima uungane na makundi dhaifu ili kulishinda lile lilo na nguvu. Kwa muktadha wa Ukraine Urusi kaungana na watu wa Donetsk na Luhansk kuishinda serikali kyiv lakini wamekosa sapoti ya wananchi walio wengi wa Ukraine na hii imesababishwa na kushindwa kwao kutumia vyombo vya habari kuhalalisha uvamizi wao. WaMagharibi wamewapiga bao kwenye hili maana kila mtu anawaonea huruma Ukraine na kuiona Urusi ni mvamizi badala ya mkombozi kama Urusi wanavyopenda kuonekana.

Mbili, idadi ya wanajeshi wa Urusi ndani ya Ukraine haitoshi kudhibiti nchi nzima ya Ukraine na watu wake milioni 40. Jeshi la Urusi lina askari zaidi ya milioni moja na kumi na nne elfu lakini katika uvamizi wake Ukraine inakadiriwa kupeleka 150,000 tu. Idadi hii ya askari haitoshi kudhibiti miji yote ya Ukraine na watu wake takribani milioni 40. Hii inatosha kuashiria kuwa Urusi hawakusudii kuikalia Ukraine.

NI YAPI MALENGO YA PUTIN?
Kama ambavyo Putin anaiita hii vita kuwa ni ‘Oparesheni maalum’ na wala si vita kamili, Putin kaingia Ukraine akiwa na malengo yake kadhaa katika hayo kuikalia kwa nguvu si moja ya malengo.

Mosi, Wanataka Ukraine iwe ‘neutral’ isiwe chini ya ushawishi wa Ulaya, kuhakikisha hili linatokea wanalenga kuivuruga Ukraine. Wameanza kwa kuigawa 2014 walipoichukua Crimea, na sasa wamezitambua jamhuri mbili mpya za Donetsk na Luhansk ambazo inatazamiwa baadae watazichukua zijiunge na Urusi.

Pili, wanataka kupunguza uwezo wa jeshi la Ukraine (de-militarization), malengo haya ni sawa na yale yaliyowasukuma waMarekani kuivamia Iraq mwaka 2013 na ndio yaleyale yanayowasukuma Israel kuishambulia Syria kila leo. Urusi inahofia kuona Ukraine panakua nyumbani kwa makombora ya waMagharibi. Sasa dunia inafanya tafiti za kina kugundua na kuendeleza ‘Hypersonic missiles’ Ukraine kujiunga NATO kutatoa fursa kwa Marekani kuyaweka humo, itachukua dakika 7 tu kwa kombora tokea Kyiv kushambulia Moscow. Suala hili halikubaliki kwa Urusi ndio maana wanalenga kupunguza kabisa uwezo wa jeshi la Ukraine.

Tatu, Kubadili serikali Ukraine na kusimika ile itakayolinda maslahi ya Urusi. Putin anawaita waNazi akina Zelensky (rais wa Ukraine) na wenzake walio madarakani sasa na moja ya lengo lake kuingia Ukraine ni kuwafurusha waNazi wote. Tafsiri yake anataka kubadili serikali aweke ile itakayokua na maslahi nae. Malengo haya yakitimia Putin atatoka Ukraine lakini ataendelea kuitazama kwa karibu kuhakikisha hawakengeuki maslahi ya Moscow.

NAFASI YA NATO KATIKA VITA HII
Katika huu mzozo Putin ana karata ya dhahabu, NATO hawataingilia kwa kuogopa vita ya tatu ya dunia. Inaaminika tangu mwaka 1985 Urusi walitengeneza mfumo unaoitwa ‘mkono mfu’ au ‘Dead Hand’ kwa kiingereza, mfumo huu wa Urusi hutuma makombora ya nyuklia kiotomatiki kwa nchi yoyote itakayo kuwa imeishambulia Urusi hata wakiua makamanda wote wa ngazi za juu au kuangamiza makao makuu ya jeshi. Mfumo huu unaweza kutambua shambulio la Nyuklia na lilipotoka na kurudisha mashambulizi huko yaliko tokea.

Hii inaipa Urusi usalama maana NATO wanaelewa fika wakikosea hesabu kivyovyote ulaya hapatakalika.

A58F6554-DA32-4ED0-868A-287F20F43BF7.jpeg


934B8A5E-3A0E-4340-800D-DCF8C1D8A768.jpeg


DAA2475F-7D48-4CA2-8145-88A15AC977F4.jpeg


6336B0E2-A239-4985-BB11-C19E4968ADB5.jpeg


EF9B7EE6-6AB8-4057-9CA3-DE2FDF8DDD82.jpeg
 
Hiyo ni sawa walikubaliana nato isijitanue lakini kwa dunia ya leo kila nchi ni huru inayo uwezo wa kuamua mambo yake bila kuingiliwa na nchi nyingine. Inachopigania ukrein ni uhuru wake wa kuamua mambo bila kuingiliwa na urusi. Kama vile urusi nayo inaamua mambo yake mwenyewe bila kuingiliwa na nchi nyingine. Mfano leo kenya na uganda wakea waamue Tanzania isijiunge na umoja fulani we unafikiri Tanzania itajisikia jee si ni bora waende vitani tuu ili wajue moja.
 
Count Capone Shukrani mkuu kwa uchambuzi mzuri wenye kuelezea ukweli na uwazi juu ya mgogoro huu.

Ila kwangu mimi naomba kujua je Urusi ilikuwa wapi mpaka NATO ikajitanua hadi mlangoni kwake toka zamani na akawa kimya kwanini kwa Ukraine amechukua hatua baada ya kugundua ana mpango wa kuungana na NATO?

Mbona majirani kadhaa wa Urusi wamejiunga NATO ila Urusi hakuchukua hatua kama hizi alizochukua kwa Ukraine?
 
Count Capone Shukrani mkuu kwa uchambuzi mzuri wenye kuelezea ukweli na uwazi juu ya mgogoro huu.

Ila kwangu mimi naomba kujua je Urusi ilikuwa wapi mpaka NATO ikajitanua hadi mlangoni kwake toka zamani na akawa kimya kwanini kwa Ukraine amechukua hatua baada ya kugundua ana mpango wa kuungana na NATO?

Mbona majirani kadhaa wa Urusi wamejiunga NATO ila Urusi hakuchukua hatua kama hizi alizochukua kwa Ukraine?
Naomba nijaribu kuchambua,
Ukiangalia ramani. Utaona nchi kubwa nyingine na inayopakana na Urusi ni Belarus hajajiunga, utaona nchi nyingine kubwa inayopakana kabisa na Urusi ni Ukraine, hao majirani wengine wapo mbali, NATO na vipuri vyao vinakingwa na Ukraine na Belarus, hizi nchi Kwa Mrusi ni NGAO, KINGA Fulani, sasa Ukarine akikubali NATO kuweka mizinga ina maana Vita yoyote, NATO wanaingia Russia kiulaini Kwa sababu wapo jirani wamepakana mpaka borders!
 
Hiyo ni sawa walikubaliana nato isijitanue lakini kwa dunia ya leo kila nchi ni huru inayo uwezo wa kuamua mambo yake bila kuingiliwa na nchi nyingine. Inachopigania ukrein ni uhuru wake wa kuamua mambo bila kuingiliwa na urusi. Kama vile urusi nayo inaamua mambo yake mwenyewe bila kuingiliwa na nchi nyingine. Mfano leo kenya na uganda wakea waamue Tanzania isijiunge na umoja fulani we unafikiri Tanzania itajisikia jee si ni bora waende vitani tuu ili wajue moja.
Lakini zamani huko mwanzoni kabisa urusi ilikuwa na makubaliano na Ukraine kuwa hawatajiunga na NATO ila kilichotokea kwa Ukraine ni kuwa wamekuwa viburi baada ya kudanganywa na USA na Nato wakahisi watapewa backup!

Putin kwa busara tu alitaka raisi wa Ukraine afanye marejeo juu ya walichokubaliana miaka hio kisha atekeleze kama mkataba unavyotaka regardless yeye ni Sovereign state. Ila kiusalama angeihatarishia urusi usalama na wao hawakutaka kumsikiliza Putin ndipo alipoamuru nguvu ya kijeshi itumike. Putin sio kichaa ama mshenzi kama watu wanavyomchukulia.
 
Naomba nijaribu kuchambua,
Ukiangalia ramani. Utaona nchi kubwa nyingine na inayopakana na Urusi ni Belarus hajajiunga, utaona nchi nyingine kubwa inayopakana kabisa na Urusi ni Ukraine, hao majirani wengine wapo mbali, NATO na vipuri vyao vinakingwa na Ukraine na Belarus, hizi nchi Kwa Mrusi ni NGAO, KINGA Fulani, sasa Ukarine akikubali NATO kuweka mizinga ina maana Vita yoyote, NATO wanaingia Russia kiulaini Kwa sababu wapo jirani wamepakana mpaka borders!
Kwani nuclear za NATO haziwezi kuwa pale Poland je Urusi haathiriki kwa Poland kuwa mwanachama wa NATO?
 
Lakini zamani huko mwanzoni kabisa urusi ilikuwa na makubaliano na Ukraine kuwa hawatajiunga na NATO ila kilichotokea kwa Ukraine ni kuwa wamekuwa viburi baada ya kudanganywa na USA na Nato wakahisi watapewa backup!

Putin kwa busara tu alitaka raisi wa Ukraine afanye marejeo juu ya walichokubaliana miaka hio kisha atekeleze kama mkataba unavyotaka regardless yeye ni Sovereign state. Ila kiusalama angeihatarishia urusi usalama na wao hawakutaka kumsikiliza Putin ndipo alipoamuru nguvu ya kijeshi itumike. Putin sio kichaa ama mshenzi kama watu wanavyomchukulia.
Sawa kabisa, na NATO washenzi, wamemponza mwenzao, anapigana Vita mwenyewe, na Warusi wanahitaji hilo eneo ili wamarekani na vibaraka wao, wawe mbali! Crimea kule mrusi anaiangalia Bahari, wakitaka kuleta manowari zao yupo!

In fact puppet masters wamarekani wamebambwa na hila zao!
 
Back
Top Bottom