Hivi hii ni starehe au ugonjwa?

ADUI

Member
Aug 6, 2009
82
10
Hivi hii ni starehe au ugonjwa?

Kuna kitu ambacho kimetawala sana katika jamii yetu kwa sasa, nacho ni utazamaji uliopilitiliza wa picha za ngono (pornography), iwe filamu au picha za kawaida.

Kilichonisukuma kuandika hili ni baada ya kuona kuwa sio vijana tu walioathirika na kitu hiki, bali watoto na hata wazee wenye familia zao. Tukisema ufanyike ukaguzi wa haraka ktk simu za watu au kompyuta tutakuta mambo ya aibu.

Mimi naamini hiki kitu kina madhara sana, na ni so addictive! Ndio maana naamini pia kuwa umefika wakati wa kuliongelea jambo hili kwa uwazi, vinginevyo kuna hatari ya kuwa na kizazi cha watu wenye matatizo mengi sana ya kisaikolojia yatokanayo na picha hizi.
 
anza wewe kubadilika yaelekea na wewe ni mtamzaji mzuri umejuaje watu wanatama hizi picha, watoto kwa wakubwa and how do you get access to their phones and computers?
 
Ni kweli no research no right to say,lakini ni kwamba hili jambo liko wazi sana kama si wewe basi kuna rafiki yako ambaye unaona kabisa asivyoweza kulala bila kuziangalia.Na pia nakubali mimi ndo "WALEWALE",ndio maana nimeandika ili kuona kama ni tatizo langu peke yangu au la...
 
Umekuwa mno mkali mpangwa1. Kujua kitu sio lazima uwe umefanya/unafanya.
 
nina mashaka na upeo wa mpangwa. mpangwa si kila kitu unachokijua umefanya reseach, unasema jamaa afanye utafit kuhusu "UWEPO WA JAMBO HILO" je wewe umefanya utafit "KUHUSU KUTOKUWEPO KWA JAMBO HILO"? Sina utafit niliofanya kuhusu hilo, lakin swala liko open kabisa na linaonekana, na madhara na kama ubakaji, maana mtu anapata stimulation halafu hana mwanamke wa kupunguza matatizo, kwenye mavyuo watu weng wanashriki kufanya punyeto(masturbation) usiniulize kama nashiriki.
 
Kaazi kwelikweli. Baadae utawasikia hawana nguvu za kiume maana wameshazoea booster ya ponography na chabo.
 
Mbona video za ngono sisi tuliokwenye ndoa tunazo nyingi sana, tunajifungia ndani mimi na wife tunaangalia then ni kichocheo cha....................kwani kuna ubaya katika matumizi haya????????????????Leteni zenu hoja
 
they do theory kisha wanafanya kivitendo.! hili janga lipo jamani acheni masihara sio lazima kila kitu kifanyiwe uchungzi wakati mambo yanaonekana dhahiri,kikkbwa kinachochangia watu hawana mawazo mbadala isipokuwa kuwaza ngono na kustareheka kwa watu wa tabaka la chini ndio imekuwa kawaida hasa kwa wale wasio kuwa na shughuli za kufaya.mi napenda kusema kwamba inabidi tuikemee hali hii kwa namna inayofaa,pia tuwapatie tiba na shughuli za kuziweka busy akili zetu zidi ya hizi fikra za ngono ngono.
 
Ni kweli no research no right to say,lakini ni kwamba hili jambo liko wazi sana kama si wewe basi kuna rafiki yako ambaye unaona kabisa asivyoweza kulala bila kuziangalia.Na pia nakubali mimi ndo "WALEWALE",ndio maana nimeandika ili kuona kama ni tatizo langu peke yangu au la...
kumbe wewe ulitaka kucompare ujue ni wangapi ili kama ni wengi uendelee na kama ni peke yako uache? Fanya kitu ambacho nafsi yako imekutuma ila si kwa kua mbona na fulani anafanya
 
lakini kwani hizi picha waliozitengeneza wanataka kina nani waangalie..

ila kwa watoto ndo naona kama ni tatizo . kwa nini watoto wawe na access ya kuangalia vitu vinavyowazidi umri ???
 
Mbona video za ngono sisi tuliokwenye ndoa tunazo nyingi sana, tunajifungia ndani mimi na wife tunaangalia then ni kichocheo cha....................kwani kuna ubaya katika matumizi haya????????????????Leteni zenu hoja

mie sioni ubaya wa kuangalia hizi picha sema kwa mie binafsi sizipendi na hazinipi mzuka wa kuziangalia
 
Back
Top Bottom