Hivi hii ni sawaa?

tatizo kubwa nnaloliona kwa bi wakubwa zetu wa kiafrika, hawataki kumchukulia yule mkamwana kama mtoto wake, huwa wanawachukulia kama wapinzani flani yaaan ful kumfatilia na kumkosoa hapo ndo inaleta ugumu kuishi pamoja....na katika hii case huyu mama ana mji wake na mume si arudi na kwake
 
Kweli kabisa, sawa mkwe ataamua kumchukulia yeye kama mama, lakini je mama yuko tayari kumchukulia mkwewe kama mwanae? Hapo ndipo taabu inapoanzia.
 

ni haki mkwe wetu kuja kukaa kwetu. hata angeishi miaka yote kwetu sina shida ..maneno lazima yawepo ukiolewa ukiwa unasikiliza maneno ya kipuuzi hutaweza kuishi kwa furaha kwenye ndoa yako..kuna maneno mengine lazima uyapuuzie...maadam sio mume anang'onga ni mkwe ambae hulali nae kitanda kimoja unayachukulia kama ushuzi hayo maneno..na hao wanaokuja kukwambia hayo maneno ningewauliza walikuwa wanazungumza nin hadi wakaniongelea? ukiolewa sio wote watakupenda ..kuna wengine wamejaliwa kusema tuu..maneno hayaui ..watasema mchana usiku watalala na maisha yataenda...hakikisha kwenye ndoa yako unakuwa na furaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…