Hivi haya maandiko yana maanisha hivi?

sisi wapagani tunaamini kwamba mungu wetu aliumba mwanamke na mwanaume ili waijaze dunia kwa kuzaana bila masharti, na ndio maana wazee wetu walioa wanawake wengi bila masharti, lakini hawa wakoloni wametuletea dini ambazo zinatuwekea msharti, mara kuoa mke mmoja, mara kuoa mwisho wanawake wanne..... Na masharti kibao.
Sisi wapagani hatujui kuoa tunajua kuzaa tu basi, hakuna mahali mungu alisema muoane, bali alisema muende mkazaane muijaze dunia........

Mnaniudhi nyie na dini zenu hizo..................lol


hahahaaaa, inabidi nifurahi maana kwa ulivyolalamika inaonekana wazi kuwa wamekubania sana kupiga gemu, wanakuudhi eeh? Pole ndugu. Lakini haujakatazwa, ni wewe mwenyewe tu, jitume.
 
Mkuu kila dini ina Mungu wao, kwa mfano kule India kuna Miungu zaidi ya 1000, na hata wapagani wana Mungu wao............ Yaani yule wanayeamani kwamba ndio aliyewaumba na kuwaleta hapa duniani.

Hivi unajua upagani ni nini?Ukishaamini uwepo wa Mungu wewe sio mpagani!
 
Mmmmh sijui mambo haya Bhan kila mtu na FANI yake mie hapa fani yangu inajulikan sana, ni kupiga story na kuuza gahawa, sasa haya mambo mie nimesoma, nimeyaona na nimefurahi ila nina NENO moja tu, kwamba ukiangalia uumbaji wa huyu ASIEONEKANA ni kwamba ulienda hierarchically kwa hio kama ni hivyo MUNGU alianza kuumba dunia, wanyama, kisha akatafuta kitu/mtu wa kuitawala na kuisimamia hio dunia na vilivyomo (yaani mkubwa zaidi) ndipo akaumba KIDUME cha Mbegu lakini akaona hiki kidume nacho sometimes zinafyatuka vile, akaona huyu nae kimeo tu ngoja Nimtafutie mkubwa wake atakayemtawala "KIMTINDO" bila ya yeye kujijua, ndipo MWANANMKE alipokuja sasa,
Ukiangalia ukweli wa mambo haya upo, cheki story za Delila Vs Samson, Ester Vs Naamani, Mamaake MUSA Vs Mfalme, Angalia pia story ya ABIGAILI vs MUMEWE, Raheli Vs Ufalme wa Herode, na Utume wa Hosea Vs Mwanamke Kahaba na wengine wengi, so huyu MZEE MZIMA SIR GOD anajua anachokifanya.
 
  • Thanks
Reactions: LD
My lovely Wife Kaunga,mi nadhani wakati Adam anaumbwa na Mungu kuna kazi aliyopewa,lakini kuzaliana kwa wanadamu kulikuja baadae.Kazi ambayo Adam alipewa ilionekana inahitaji msaidizi,hapo ndo akapatikana mwanamke,na kuzaana kulipokuja. . . . . . . . . . . . .. . 0 Hivyo basi,mwanaume aliumbwa aifanye kazi ya Mungu,mwanamke hakuwepo kwenye mpango wa uumbaji wa mwanzo,alikuja kuumbwa kwaajili ya mwanaume,amsaidie mwanaume kutimiza kazi aliyopewa huyo mwanaume. . . . . . . . . . . . .. .. Lakini mwanaume hakuumbwa kwaajili ya mwanamke,bali aliumbwa akamilishe kazi iliyosababisha aumbwe. . . . . . . . . . . . . . . . . . Wife halafu leo nataka unipikie mtori na utumbo na chapati za kumimina,nimemisi sana huo msosi!
 
Hivi nilishakuambiaga kuwa nakupendaga sana my lil bro? Kama bado, its official! I love you!

I knw ma lovely dada,nataka leo uje home,kuna msori wifi yako nimemuambia aandae,plz usiache dada yangu mpenzi!
 
LD,unapoleta tatizo ili kutetea tatizo unakua unaongeza tatizo.Kutokuwepo MWANAUME haiondoi ukweli(kama ni ukweli) kuwa mwanamke aliumbwa kwaajili ya mwanaume.Tatizo ulilolitaja limezungukwa na matatizo mengine mengi na linahitaji mada nyingine!
 
  • Thanks
Reactions: LD
@eiyer,
ukisoma mwanzo 3:16 imeandikwa:
"kisha akamwambia mwanamke, nitakuzidishia uchungu wa kuzaa,
kwa uchungu utazaa watoto;
utakuwa na hamu na mumeo,
hata hivyo nae atakutawala."

kibiblia mwanamke aliumbwa baada ya mwanaume kuwa mpweke duniani, sikubaliani unaposema kuwa lengo ni kumsaidia mwanaume atimize malengo ya Mungu, bali kila nafsi inatimiza malengo ya Mungu na mke anaweza kumuokoa mume asiyeamini na mume anaweza kumuokoa mkewe, ndo maana andiko linasema
"ndio maana mwanaume humuacha baba yake na mama yake akaambatana na mkewe, nao wawili hao huwa mwili mmoja"
maana kama lengo ni kumsaidia mwanaume atimize majukumu yake kwa mungu, kwa nini mwanamke aliadhibiwa walipokula tunda? kwa nini asipewe mwanaume peke yake adhabu?





Kwenye Biblia,Mw 2:18 imeandikwa;"BWANA Mungu akasema,Si vema huyo mtu awe peke yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae".Ndipo akamletea wanyama kibao lakini hakuonekana wa kufanana nae,Mw 2:19-20,ndipo Mungu alipomuumba mwanamke kutoka ubavuni mwa Adam. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Hapa nimegundua kuwa,Mwanaume alianza kuhitaji msaidizi wa kawaida lakini ngono sio sababu ya kuumbwa mwanamke.Pili,mwanaume alihitaji kusaidiwa,hii maana yake ni kwamba,Mwanaume kamwe hawezi kutimiza majukumu yake bila mwanamke.Tatu,mwamke aliumbwa kwaajili ya mwanaume,lakini mwanaume hakuumbwa kwaajili ya mwanamke.Nne,kazi iliyomleta au kusababisha mwanamke kuumbwa ni kumsaidia mwanaume tu.Tano,malengo ya uumbaji wa Mungu hayakumhusisha mwanamke,yaani mwanamke yupo duniani si kwaajili ya kutimiza malengo ya uumbaji wa Mungu bali kumsaidia mwanaume kuyatimiza malengo ya Mungu. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Jamani msinirushie mawe,kama Mungu hakumaanisha hivyo leta tafsiri yako,unless uwe huiamini Biblia.Hebu tujadiliane inawezekana nimepotoka!
 
BADILI TABIA,hayo mambo ya kuzaa kwa uchungu yamekuja baadae,mimi nazungumzia kabla bana.Hivi mwanaume asingehitaji msaidizi kungekua na mwanamke leo?
 
mawazo ya Mungu hayalinganishwi na malaika, mwanadamu wala shetan yako mbali sana na mtawaza sana.
 
Ila Mungu nae kisirani chake! Nilitaka kuuliza adamu na hawa walijuana tu kupata watoto. Hii mambo ya sijui viuno na shanga ndo imeanza kuleta balaa! Kumbe hamu ni sehemu ya adhabu! Ngoja nikatafute ukombozi kwa damu ya Yesu! Kha!
@eiyer,
ukisoma mwanzo 3:16 imeandikwa:
"
utakuwa na hamu na mumeo,
hata hivyo nae atakutawala."

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom