Hivi hawa the so called EWURA kazi yao ni nini?

kifuruko

Member
Sep 27, 2011
20
2
jamani ewura mpaka sasa ni mwez bei za mafuta ni zilezile hazija shuka,na ahadi zenu watanzania wanazisikiliza na kuzifatilia,tupeni majibu au na nishati ni siasa?
 
Ewura pia ni wasanii wanapenda kujilipa ili watatutue matatizo yao lakini hakuna ushauri wa wadau kwani nao wanafaidika kwa kuongeza bei maana asilimia inaongeza kiasi kadri pesa inapoongezeka
Angalia bei ya mafuta kama kweli wako makini Dar shs 1890 na Mz shs 1880
Dom shs 2000 Dar shs 2200 Je wananchi ni mazuzu kiasi hicho Acheni usanii.
Je wananchi hawajui kuwa mnalipwa na wenye masheli? Je mwajua kuwa miongoni mwenu mnawasimulia mnaowanyonya au mwadhani ni wajinga hawana kumbukumbu? Au mwadhani waliokaribu yenu hawasemi siri zetu? au mwajua kuwa tuko katika karne ya technolojia? Bei ya nje inauhusiano gani kama mafuta yanakuja pamoja na yanakaa muda mrefu?
Je kukokotoa kwenu ni kwa halali? kama kwa halali kwanini bei zenu hazizingatiwi?
Dhuluma mbaya naamini ipo siku mtaaumbuka na nyonyeni kwani wakurugenzi wametoka miongoni mwa tabaka la wanasiasa wanyonyaji ndo maana wanaona kila kitu sawa na wananchi watu wa kupelekewa tu amri
Amini dhuluma mwala sana na dhuluma ina mwisho mbaya! "TENDENI HAKI KWA WANYONGE MAFUTA YA TAA HAYANUNULIWI TENA ULIZENI MARAFIKI ZENU WA SHELI" Umeme nao ni shida Rushwa pamoja na nyie kupandisha bei ya kuunganisha umeme
 
Sijaelewa, naona bei ya petrol leo ipo juu na sijasikia tamko lolote, vp wadau, nyie mna taarifa?
 
Bei za jumla na rejareja kwa aina zote za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 07 Machi 2012.

Katika toleo hili, bei ya rejareja kwa mafuta aina zote zimepanda kama ifuatavyo:
Petroli imeongezeka kwa Sh 87/lita sawa na asilimia 4.06; Dizeli imeongezeka kwa Sh 3/lita sawa na asilimia 0.14;
na Mafuta ya taa yameongezeka kwa Sh 12/lita sawa na asilimia 0.59.Mabadiliko haya ya bei za mafuta hapa nchini yametokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia ambapo bei ya mafuta ya petroli imeongezeka kwa wastani wa dola za marekani 95.7kwa tani sawa na asilimia 9.09, mafuta ya dizeli yameongezeka kwa wastani wa dola za marekani 27.1 kwa tani sawa na asilimia 2.76, na mafuta ya taa kwa dola za marekani 34.04 kwa tani sawa na asilimia 3.28. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimebadilika kama ifuatavyo:petroli imeongezeka kwa Sh 87.18/lita sawa na asilimia 4.21; Dizeli imeongezeka kwa Sh 2.61/lita sawa na asilimia 0.13; na
Mafuta ya taa yameongezeka kwa Sh 12.32/lita, sawa na asilimia 0.62.(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta
 
ukweli ni kwamba bei ktk soko la dunia imeshuka ni ni dola 106 kwa pipa na shilingi imeongezeka thamani ikilinganishwa ba dola sasa ongezeko limetokana na nini. Waseme uongo mwingine tu. Mbona nchi jirani wameshusha.
 
ha ha ha ha ha ha Mtakoma kuichagua chadema arumeru. Lazima tuwachape viboko indirectly. chezea CCM!!
 
Kwa bei hiyo, uko mkoa gani? mbona kwa Dar mimi nimenunua kwa bei ileile. Halafu mtu anapouliza kitu badala ya kumpatia jibu unakuta jitu linatukana tu, mimi huwa ninashangaa sana kwa watu wa namna hii. Jitu linaandika tu Pumbavu sana Sumatra hilo kwani ndilo jibu alilokuwa anahitaji kweli?.
 
Hivi ndugu wana jamvi JF hawa EWURA kazi yao ni nini?
Boti tiketi imeandikwa shlng 20000 lakn unalipa 30000 mchezo mchzfu unachezwa hapa ma agent wanauza tiketi zote kwa walanguzi na ukienda kukata tiketi unaambiwa zimeisha una haraka huna jinsi lazma utoboke hizo pesa kwa vibaka hao lakin hili si la leo wala jana sasa mchezo huu unachezwa ubungo kwa wanao safiri mikaoni bei inayo andikwa kwenye tiketi sio abilia anayo lipa. Kwenye viwanja vya ndege upande wa tiketi mchezo huo mchafu unaendela sasa the so called EWURA anawajibika kwa nani?
 
Mtu mwenye anwani zao, hususani simu na e-mail atoe ili tuwaulize. Tuwaeleze (wasije sema hatujui) na wakishindwa kuweka mambo sawa; TUWAHUKUMU
 
badisha bro ni EWURA na sio HEURA

sawa mkuu najaribu ku edit lkn haeading haibadiliki najua wana jamii F ni great thinker so kosa hilo la kiuandishi haliiwezi ikawa sababu ya kutokuchangia mada ilioko uwanjani
 
Back
Top Bottom