Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,198
- 7,536
- Huyu mtu ana mpango wa kugombea urais 2015,
- Huyu mtu huyu hutangazia nia yake maeneo ya ibada,
- Huyu mtu huyu hutanguliza vibahasha katika maeneo hayo ya ibada kabla ya kutangaza nia (na vibahasha vyake vya ukweliii).
- Huyu mtu huyu wengine humlaumu eti ni fisadi.
Sasa mimi wasi wasi wangu ni pale ninapoona hakuna mtu anayemkemea.Najiuliza je! ina maana huyu mtu yuko sahihi? Kama tunadhani yuko sahihi; ni kwa nini? Hatuoni kuwa kama akiendelea hivi, wenzake ambao nao wana nia ya kugombea urais 2015, wataanza kuingia na vibahasha kwenye maeneo ya ibada na hiyo sio tu kwamba itakuwa ni aina fulani ya rushwa bali pia itachochea migawanyiko ya kidini?
Kama hayuko sahihi; kwa nini vyombo mbali mbali vya kitaifa kama vile Chama chake, Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Rais, TISS, n.k wasimshauri? Je! inamaana watakuwa hawaoni, au wanamuogopa, au wana maslahi na kinachofanyika?
Kwa maoni yangu jambo hili linachukuliwa kama mzaha ila mwisho wa siku linaweza kuleta migawanyiko mibaya.Wenzake watakuwa wanasoma upepo, wakiona hili la kutoa na kusaidia kuchangisha fedha kwenye maeneo ya ibada linasaidia nao watawekeza huko huko.Mwisho wake watu wataanza kuhoji fulani kachangia msikiti au kanisa? kama kachangia kanisa kachangia bei gani na msikiti kachangia kiasi gani? kisha kwa nini kule kachangia zaidi ya kule ? kwa nini kwetu hajachangia? kwa nini kapendelea dini ile au hii? fulani na yeye na aje kwenye dini hii au ile n.k. Hii ni hatari aisee.
Nashauri katika kuchangia msitaje majina ya watu.Changieni tu hoja kwa ujumla wake kwa sababu mkitaja taja majina ya watu, upo uwezekano wa uzi huu kupoteza muelekeo na kisha kufungiwa