Hivi Hatumuoni Huyu......! au yuko sawa?

Hivi Hatumuoni Huyu......! au yuko sawa?

huyu jamaa ana nguvu ya ziada.
kumbukeni aliwahi kukiri hadharani kuwa yeye na JK hawajakutana barabarani

inawezekana kabisa anamuogopa na ana sababu kuu na ya msingi ya kumuogopa.

but all in all, hatima ya nchi yetu bado ipo mikononi mwetu sisi wananchi kwa kiasi kikubwa
tutumie vizuri nafasi ya kuchagua kiongozi mwenye sifa na maadili. sio fisadi mmwaga mapesa katika majumba ya ibada.
 
Ni kama serikali na chama chake wanamgwaya!!! Matokeo ya analolifanya yatatupeleka pabaya maana kila siku tunawasikia wakisema MSICHANGANYE SIASA na DINI!!!!! Sasa mtu anapoamua kufanya nyumba za ibada uwanja wake wa kujitambulisha=JANGA
 
Hakuna mtu wa kumzuia Lowassa. Wananchi wanampenda na hela anayo. Hata kama hupendi huna budi kukubaliana na ukweli japo ninaelewa unaumia lakini ndiyo hakuna namna ya kuubadilisha. Huwezi kuukimbia ukweli.
 
Sina uhakika kama huwa unaelewa mada kabla ya kuchangia.Suala la msingi ni kufuata kanuni na maadili ya msingi ambayo yatasaidia wagombea kutoingia kwenye hali ya kuligawa taifa; na kisha baada ya hapo si uchaguzi upo bwana? sasa ya nini tupige makelele ?
 
CCM ndio waumini wa siasa za udini,hivi ndugu zangu watanzania mambo hayo angefanya zito,mbowe au slaa angeachwa hivi hivi na watanzania achilia mbali chama chake? Tafakali chukua hatua
 
Sina uhakika kama huwa unaelewa mada kabla ya kuchangia.Suala la msingi ni kufuata kanuni na maadili ya msingi ambayo yatasaidia wagombea kutoingia kwenye hali ya kuligawa taifa; na kisha baada ya hapo si uchaguzi upo bwana? sasa ya nini tupige makelele ?
1016130_616543391703911_1333343654_n.jpg
 
  • Huyu mtu ana mpango wa kugombea urais 2015,

  • Huyu mtu huyu hutangazia nia yake maeneo ya ibada,

  • Huyu mtu huyu hutanguliza vibahasha katika maeneo hayo ya ibada kabla ya kutangaza nia (na vibahasha vyake vya ukweliii).

  • Huyu mtu huyu wengine humlaumu eti ni fisadi.

Sasa mimi wasi wasi wangu ni pale ninapoona hakuna mtu anayemkemea.Najiuliza je! ina maana huyu mtu yuko sahihi? Kama tunadhani yuko sahihi; ni kwa nini? Hatuoni kuwa kama akiendelea hivi, wenzake ambao nao wana nia ya kugombea urais 2015, wataanza kuingia na vibahasha kwenye maeneo ya ibada na hiyo sio tu kwamba itakuwa ni aina fulani ya rushwa bali pia itachochea migawanyiko ya kidini?

Kama hayuko sahihi; kwa nini vyombo mbali mbali vya kitaifa kama vile Chama chake, Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Rais, TISS, n.k wasimshauri? Je! inamaana watakuwa hawaoni, au wanamuogopa, au wana maslahi na kinachofanyika?

Kwa maoni yangu jambo hili linachukuliwa kama mzaha ila mwisho wa siku linaweza kuleta migawanyiko mibaya.Wenzake watakuwa wanasoma upepo, wakiona hili la kutoa na kusaidia kuchangisha fedha kwenye maeneo ya ibada linasaidia nao watawekeza huko huko.Mwisho wake watu wataanza kuhoji fulani kachangia msikiti au kanisa? kama kachangia kanisa kachangia bei gani na msikiti kachangia kiasi gani? kisha kwa nini kule kachangia zaidi ya kule ? kwa nini kwetu hajachangia? kwa nini kapendelea dini ile au hii? fulani na yeye na aje kwenye dini hii au ile n.k. Hii ni hatari aisee.

Nashauri katika kuchangia msitaje majina ya watu.Changieni tu hoja kwa ujumla wake kwa sababu mkitaja taja majina ya watu, upo uwezekano wa uzi huu kupoteza muelekeo na kisha kufungiwa

Kama una ushahidi tuwekee,ila tujiulize mtu ameiba na tayari anazo pesa na hajachukuliwa hatua.Kaamua kutumia hizo hizo pesa kuimarisha nyumba za ibada badala ya kujijengea majumba ya kifahari nje ya nchi pengine ni moja ya namna yake ya kutubu je unataka kuwashauri viongozi wa nyumba za ibada wazikatae? Kuna majangili na wachawi na wauza madawa ya kulevya na wauza miili nk wanatoa sadaka ndani na nje ya nyumba za ibada bila kujitangaza.Tuwaache watumie hizo pesa watakavyo ilimradi wasivunje sheria.

Huyo mtu sidhani kama ana shida ya Urais maana kama nia ni hiyo angewahonga Nec ya chama chake kwani unauhakika gani kama atapitishwa na chama chake?

Tukirudi kwako je ww ni mkamilifu kiasi gani? Hujawahi kupiga deal? Ulipofanikisha haukutoa sadaka unaposali? Au hukununua zawadi kwa watu wa nyumbani kwako? Tusemeje sasa, tusitembee na hisia na wala tisiwe na hofu zisizo za lazima najua mtangulizi wake hawezi kumpa nafasi nafikiri nimeheshimu ushauri wako wa kutotaja majina ya watu.
 
Nape atoe jibu maana yeye ndiye katangaza kuwa mwanaccm atakayeanza kampeni ya urais mapema atachukuliwa hatua. Sasa mbona EL anaendelea kwa kasi baada ya kumaliza makanisa sasa kaingia kwa machinga na vijana. Muda si mrefu atahamia kwa wakulima na wafanyabiashara. Nape utamuweza EL kweli au ndio zile kelele za barua ndani ya siku 90 wawe wamejitoa mpaka leo kimya kama maiti!
 
tujiulize mtu ameiba na tayari anazo pesa na hajachukuliwa hatua.Kaamua kutumia hizo hizo pesa kuimarisha nyumba za ibada badala ya kujijengea majumba ya kifahari nje ya nchi pengine ni moja ya namna yake ya kutubu
Hudhani kama mtu kaiba na anataka kutubu; basi dawa ni kukiri mbele ya aliemuibia kwamba alimuibia na sasa anaomba radhi na kisha kurudisha alichoiba?
je unataka kuwashauri viongozi wa nyumba za ibada wazikatae?
Siungi mkono utaratibu wa viongozi wa dini kuwaalika wanasiassa waongoze harambee za kidini.Kwa nini viongozi wa kidini wasiongoze masuala ya kidini na viongozi wa kisiasa wakaongoza masuala ya kisiasa?
Huyo mtu sidhani kama ana shida ya Urais
Hata mimi sijui kama ana shida ya uraisi .Ila tu tujue baada ya kutoa mchango wake hutangaza dhamira moja kwa moja , au kiufichouficho.Hata hivyo mimi sijui kwa nini haya yanafanyika sasa kuelekea uchaguzi mkuu.Labda unaweza kutusaidia.
maana kama nia ni hiyo angewahonga Nec ya chama chake kwani unauhakika gani kama atapitishwa na chama chake?
Tunajadili yale tunayoyaona.Wewe unajua mambo yanayofanyika ndani ya NEC ya CCM?
 
Hakuna mtu wa kumzuia Lowassa. Wananchi wanampenda na hela anayo. Hata kama hupendi huna budi kukubaliana na ukweli japo ninaelewa unaumia lakini ndiyo hakuna namna ya kuubadilisha. Huwezi kuukimbia ukweli.
Nadhani mda mwingine hata unachosema hukijui. Hebu tetea hoja yako ieleweke we kibaka sio una jamba jamba tu humu. Kakufanyia nini la maana huyo fisadi?
 
Wewe umenena kitu. Jamaa anaweza kuhama chamaaa... Na mimi huko atakakoenda kura yangu itamfuata hukohuko.
 
Watu wa chama chake na wao wanalalamika pembeni bila ya kumfesi mhusika tena hawathubutu hata kumtaja jina kama mwanzisha mada alivyoogopa kumtaja jina.
Kuna kitu si cha kawaida kwa Lowasa, kwa nini anaogopwa na kila mtu hapa nchini?
Hadi mwenyekiti wa chama chake anamwogopa.

Fedha yake ndiyo inayowafanya watu wamwogope kwani anaweza kufanya lo lote. Chezea nguvu ya pesa wewe.
 
Sina uhakika kama huwa unaelewa mada kabla ya kuchangia.Suala la msingi ni kufuata kanuni na maadili ya msingi ambayo yatasaidia wagombea kutoingia kwenye hali ya kuligawa taifa; na kisha baada ya hapo si uchaguzi upo bwana? sasa ya nini tupige makelele ?

Ndiyo maana ni mara chache sana huwa ninawaReply watu wanaoniQuote hapa Jukwaani kwasababu ya "pumba" zenu.

Kuchangia kwake ujenzi wa nyumba za ibada analigawa vipi taifa? It seems like you are INSECURE.

Kwanza hii thread yenyewe imejaa nadharia tupu ni kwavile umetukuta sisi waSwahili tunapenda mambo marahisi marahisi lakini kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuchangia thread ambayo imejaa nadharia tupu (umeshindwa hata kulitaja jina la huyo muhusika umeishia kutuaambia "huyu mtu").

Ni aibu kwa threads za namna hii kuruhusiwa kuwepo hapa kwenye Jukwaa la Siasa. Huyu mtu?! WTF?
 
Asante kuliona hilo...sijui huyu jamaa anaogopewa nini? hakuna chombo cha habari kinachomfichua zaidi ya kummwagia sifa. au ndiyo vibahasha vyenyewe? Msitegemee Mr. Dhaifu akafanya hivyo kwa kuwa yeye ni dhaifu. Msajili mimi humwita Bwana Porojo...ukimsikiliza unakuwa kama unaangalia Origino Comedy vile, sioni uhalisia kwake. Nani mwingine, Katibu Mkuu wetu, Majanga...kana kwamba kaambiwa ukisema tu na mimi nalipua. kimyaaaaaaaaaa! M/Mwenyekiti, yeye ni bwana Mikwara...hana lolote. Labda akimaliza fungate. alishawahi kutishia kuwa atafukuza wote waliongia kwa rushwa....mpaka Yesu atakaporudi. Nani mwingine....Nyerere, amekufa!

Akiisha pata, nawaapia mtalipia mpaka senti ya mwisho ya fedha zote alizowapa! Ninukuu hapa! Kivipi? Mtajua wenyewe, si mlikula, mkashiba? Mtalipia!

Kwa hiyo, hakuna wa kumkemea mtu huyu! Full Stop!
 
Ndiyo maana ni mara chache sana huwa ninawaReply watu wanaoniQuote hapa Jukwaani kwasababu ya "pumba" zenu.

Kuchangia kwake ujenzi wa nyumba za ibada analigawa vipi taifa? It seems like you are INSECURE.

Kwanza hii thread yenyewe imejaa nadharia tupu ni kwavile umetukuta sisi waSwahili tunapenda mambo marahisi marahisi lakini kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuchangia thread ambayo imejaa nadharia tupu (umeshindwa hata kulitaja jina la huyo muhusika umeishia kutuaambia "huyu mtu").

Ni aibu kwa threads za namna hii kuruhusiwa kuwepo hapa kwenye Jukwaa la Siasa. Huyu mtu?! WTF?
navyoamini mimi fisadi huyu hawezi kuwa rais wa nchi yetu labda kama sikuzaliwa mara!ikitokea akawa basi bwana!
 
Nawewe niwalwale mafisadi huwezi kuwalazimisha watu cha kuchangia. Na unachokifanya ndicho vyombo husika havichukui hatua kwakuwa wote ni wanafiki eti wanaogopa kupoteza mwelekeo.
 
navyoamini mimi fisadi huyu hawezi kuwa rais wa nchi yetu labda kama sikuzaliwa mara!ikitokea akawa basi bwana!
kuna siku utakuja kukimbia kivuli chako mwenyewe .nakuambia hizi dini bora zisingekuwepo zimerudisha maendeleo nyuma sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom