Hivi Dr. Gama huoni kama unawaaibisha wasomi na mawazo yako finyu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Dr. Gama huoni kama unawaaibisha wasomi na mawazo yako finyu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Trustme, Apr 25, 2012.

 1. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mi naona nilete kwenu wana JF kuhusu huyu Msomi wetu (aah msomi wa CCM) anayemshauri Mh Dr.JK kuhusu maswala ya siasa hapa TZ. Jana alipokua anaulizwa na mwambishi wa habari kuhusu utendaji wa mawaziri wa serikali ya JK, alisema SERIKALI HAIENDESHWI NA MASHINIKIZO YA WATU. Kinachonishangaza mimi ni hiki, Yan Dr. Gama haujuiserikali imechaguliwa na watu? na watu hao ndiyo wanaishinikiza serikali kufanya waliyowatuma wafanye baada ya kushindwa kuwajibika ilivyokuwa inatarajiwa!!! Pili, Nashindwa kuelewa, kwa nini baadhi ya waandishi wa habari kila mara wanamfuata Dr. Gama peke yake kutafuta maoni yake? Wakati wanajua fika ni mropokaji na anatumiwa na CCM kwa manufaa yake binafsi? Tatu, hivi JK hana washauri wengine wa mambo ya kisiasa kweli? kwa sababu Mshauri kama Gama hana jipya,tunamjua tangu alipokua kule REDET na utafiti wake wa uwongo na JK akaingia mtegoni na kumfanya mashauri! Kweli mtu unatoa taarifa za uwongo halifu ndiyo unapewa cheo? Nawasilisha Mada
   
 2. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Dr. Gama ni nani?? Lete CV kwanza!!!!!!
   
 3. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Au unamaanisha Dr. Bana??????????????????????????
   
 4. K

  Korongwe Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Mhh Dr. Gama!!! BANA
   
 5. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yes Dr. BANA!
   
 6. O

  One Man Army JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  magamba kazini..
   
 7. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Mkuu, nasikia wengine wanatoa chochote ili mradi tu waonekane kwenye runinga. Usishangae wasomi hao hao ndio wanaozungumzia masuala yote nchini, Madini, kilimo, maliasili, uchumi, sheria, etc etc. Kinachoniudhi ni kuwa vyombo vya habari vinayachukulia mawazo yao finyu kuwa yanawakilisha "WASOMI" wa TZ.

  Inachosha kila kukicha na kuchwa wasomi wa nchi hii ni wale wale na wengi wao ni wale wanaolamba viatu vya watawala. Hata kwenye masuala nyeti kama kamati ya Katiba ni hao hao. Wa-TZ wakilalamika wanaambiwa "mbona wasomi mmewakilishwa"! Hiyo ndiyo TZ
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,688
  Likes Received: 12,725
  Trophy Points: 280
  huyo ndio Dr.Bana a.k.a Dr gamba lepesi kuling'oa maana adhabu yake ni kulipuuza
   
 9. h

  happy patrick New Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uyu nae anawaibisha wasomi wenzake zama hz c zakuropka au UDOKT wakupewa??
   
 10. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Bana ni msomi wa kiwango cha PhD.
  Inawezekana ni mwachama wa CCM.Kama ndivyo tuheshimu uamuzi wake huo.Na pia tuheshimu mawazo yake hata kama hatukubalani naye.
   
 11. A

  August JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Zainab mwenyewe ndio huyu? anayesema hivi?
  CHAMA cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS), kimesema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inatumia nembo ya chama hicho kinyume cha sheria.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Dk. Zainabu Gama wakati wa kuadhimisha Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani ambayo kaulimbiu yake ni "Vijana katika mwendo."

  Alisema nembo hiyo inapotumika katika magari ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na hospitali za umma na za watu binafsi ni makosa, na hata jeshi haliruhusiwi kuitumia isipokuwa wakati wa vita wanapokuwa wanatoa huduma za afya.

  "Nembo hii imetolewa kisheria na inalindwa na mikataba ya kimataifa ya Geneva. Pia ni utambulisho na hutumika kulinda watu walioathiriwa na vita na majanga mbalimbali, kulinda mali za chama pamoja na wafanyakazi wanaotoa huduma," alisema Dk. Gama.

  Kwa mujibu wa Dk. Gama, watu wengi hawajui matumizi sahihi ya nembo hiyo na inasikitisha kuona baadhi ya vijana wanaokaa pembezoni mwa barabara inapotokea ajali hukimbia eneo la tukio na kuwaibiwa majeruhi huku wakiwa wamevaa shati zenye nembo ya chama hicho.

  Alisema, katika maadhimisho hayo, wamezindua kampeni ya kitaifa ya kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya nembo yao yenye kaulimbiu ya "Ilinde nembo ya Msalaba Mwekundu ikusaidie."

  Alisema kampeni hiyo inakwenda sambamba na mchakato wa kurekebisha Sheria Namba 71 ya Mwaka 1962 iliyoanzisha chama hicho ili iendane na mazingira ya sasa na kuainisha adhabu kwa wanaoitumia vibaya.
   
 12. CHIHAYA

  CHIHAYA Senior Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Uko sawa kabisaa mkuu. Mimi nipo sua lakini sijapata kuona waandishi wakiwafuata wataalamu wa kilimo, mifugo, uchumi kilimo ambao wako hapa kutoa maoni yao zaidi kila kitu ni akina Bana, Bashiru na wenzao. Wapo watu mhimu kwa utaalamu husika na waandishi wa habari watambue hilo.
   
 13. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,980
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kama anaona wananchi hawaishinikizi serikali angojee majibu ya uchaguzi 2015 !!!!! 'Dalili za mvua ni mawingu', msemo wa waswahili!!!Mwenye macho haambiwi tazama!!
   
Loading...