Trustme
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,169
- 349
Mi naona nilete kwenu wana JF kuhusu huyu Msomi wetu (aah msomi wa CCM) anayemshauri Mh Dr.JK kuhusu maswala ya siasa hapa TZ. Jana alipokua anaulizwa na mwambishi wa habari kuhusu utendaji wa mawaziri wa serikali ya JK, alisema SERIKALI HAIENDESHWI NA MASHINIKIZO YA WATU. Kinachonishangaza mimi ni hiki, Yan Dr. Gama haujuiserikali imechaguliwa na watu? na watu hao ndiyo wanaishinikiza serikali kufanya waliyowatuma wafanye baada ya kushindwa kuwajibika ilivyokuwa inatarajiwa!!! Pili, Nashindwa kuelewa, kwa nini baadhi ya waandishi wa habari kila mara wanamfuata Dr. Gama peke yake kutafuta maoni yake? Wakati wanajua fika ni mropokaji na anatumiwa na CCM kwa manufaa yake binafsi? Tatu, hivi JK hana washauri wengine wa mambo ya kisiasa kweli? kwa sababu Mshauri kama Gama hana jipya,tunamjua tangu alipokua kule REDET na utafiti wake wa uwongo na JK akaingia mtegoni na kumfanya mashauri! Kweli mtu unatoa taarifa za uwongo halifu ndiyo unapewa cheo? Nawasilisha Mada