Hivi Dr D.W Slaa alihama CHADEMA kwa sababu Lowassa alihamia au aligombea urais kwa tiketi ya CHADEMA?

Wanajamvi,

Balozi Dr Slaa, ambaye yumo humu lakini sijamsikia zaidi ya kuona akitoa likes kwa wana ccm wenzake, alisema kuwa kitendo cha Lowassa kuhamia chadema ni sawa na “choo kuhamishiwa sebuleni”

Lakini Sasa Lowassa amerudi ccm, Slaa yumo humo, hivyo yuko chooni na hapo hapo sebuleni. Hii ni kwa mujibu wake yeye mwenyewe.

Kuna wanaodhani kuwa sasa atarudi chadema. Na hii imefikia hadi kwa mwana jamvi maarufu na madai mkubwa wa chadema humu, Salary Slip kuanzisha mada inayosema kuwa “ije mvua lije jua, Slaa asiruhusiwe kurudi chadema”. Lakini pia kuna wanajamvi wanaodhani kuwa si rahisi kwa Slaa kuachia “Keki” kwasababu ya ubalozi aliopewa na Maghufuli mara baada ya kum sapoti kwenye mbio za urais na kukupigia chama alichoshiriki kwa kiasi kikubwa sana kukijenga!

Ni wazi kuwa kurudi kwa Lowassa ccm kuna consequences zake. Mojawapo ni issue ya Slaa. Sana sana ni kwasababu ya legacy yake. Kama ni kweli hakuwa na tamaa ya urais, na alihama chama kwasababu tu ya Lowassa kuhamia, basi shurti atoke ccm. Great thinker anyeitwa barafu , alisema “asiyempenda kaja”. Hivyo kuonyesha msimamo hapa ni muhimu.

Lakini kama alihama kwasababu alipoteza ile nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, basi ni wazi itabidi awaombe msamaha wanajamvi wenzetu humu ambao na walijitoa kindakindaki kumsapoti na hata kuwa na mawazo hasi kabisa kwa baadhi yao. Mfano Mzee Mwanakijiji pamoja na MTAZAMO . Lakini mkuu idawa yeye kidogo alikuwa bado ana “balance”! Pamoja na great thinker mwingine Nguruvi3 . Lakini msimamo wa JokaKuu haukubadilika. Ningependa kusikia maoni yao kuhusu hilo. Pamoja na ushauri wowote kwa Dr Slaa kama wanao!

Nisiseme mengi kwa sasa.
Jmushi1..Slaa alirudi CCM lini?
 
Mimi binafsi ni mtu ninayeheshimu.mchango wa Dr. Slaa ndani ya cdm na sina shaka na weledi wake. Ila sioni haja yoyote ya kumlazimisha kurejea cdm kwani tayari walishahitilifiana na viongozi waliopo. Pia Slaa ni mzee na sitegemei aweze tena siasa za mikiki mikiki, sana sana arejee kama mshauri na sio kupata nafasi ya uongozi wa juu tena. Iwapo Slaa ataridhia kurejea kama mshauri hiyo ni sawa lakini kama kiongozi ni kuua vipaji vya vijana bila sababu ya msingi.
Vijana gani hao wenye vipaji..na Ni vipaji gani hivyo?
 
Dr.Slaa ameondoka CHADEMA baada ya kuona kumbe CHADEMA kipo kwa ajili ya maslahi ya watu Fulani ndio maana mtu akija na mipesa yake anauziwa nafasi ya kugombea uraisi
Hawezi kurudi mwacheni apumzike nyinyi CHADEMA subirini 2020 aje kigogo mwingine na mipesa yake mumuzie kiti cha kugombea uraisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ubishi wa kilocal.....hivi hukusikia alivyosema chadema wameleta uchafu sebuleni kwa mana ya Lowassa?Huu ni ubishi wa ibilisi!!
Sasa hapo kabisha nini?Kuna sehem Slaa alirudi CCM?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Slaa alisema amestaafu siasa za vyama sio za nchi. Ukiteuliwa na Magufuli ww ni mwanaccm taka usitake. Hata Magufuli alishasema hilo, kwake hamna mteule neutral.
Siasa za vyama sio za Nchi hahahahahahah. Hivi wewe bavicha sikuizi umekuaje?Hizo siasa za Nchi ndio siasa gani?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Jmushi1..Slaa alirudi CCM lini?

Magufuli alisema hadharani mchana wa jua kali kwamba akikuteua huwezi kuwa neutral. Kuna post yako niliiona ukisema eti Slaa ni mtumishi wa serikali. Lini aliomba ajira serikalini? Siku hizi serikali inaajiri watu walioko above 60yrs? Yeye ni mteule wa rais, anafuata atakacho rais. Iwapo jeshi limetengwa na siasa kikatiba na bado Magufuli alipokea wanaccm waliohamia toka cdm kwenye hafla ya kijeshi, ndio itakuwa Slaa aliyeiziria cdm kwa kukosa nafasi ya kugombea urais?
 
Mhn! Labda, ngoja tubiri. Nimeshindwa kuelewa. Lakini ni kweli alijiuzulu siasa kwasababu ya Lowassa. Nafikiri kupokelewa "bila masharti" kwa alivyosema.

Taharuki imetanda juu ya wapi alipo Katibu mkuu wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa. kila mtu anazungumza lake kwa kadri anavyoelewa. wengine wakisema yupo kwenye maandalizi ya vikao vya kamati kuu na wengine wakisema amejificha kwa sababu hakubaliani na maamuzi ya kumleta EL kwenye chama.

Mimi kama kada wa chadema wa muda mrefu na mwanasheria mzoefu nimefanya utafiti na nimejiridhisha bila shaka yoyote kuwa hali si shwari ndani ya chadema licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa kuonesha kuwa hakuna tatizo.

Ukweli ni upi? Ukweli ni kuwa Dr.Wilbroad Slaa hakubaliani na maamuzi yaliyofanywa na kamati kuu ya Kumleta EL na kumpa nafasi ya kugombea Urais bila kufanya utafiti wa kutosha. Slaa anadai kuwa maamuzi haya ni ya haraka mno na chama kilitakiwa kijitafakari zaidi kabla ya kumpa ridhaa ya kugombea Urais.

Ikumbukwe siku ya jumapili tar.26 wakati UKAWA wamefanya kikao cha mwisho na EL Dr.Slaa alikuwepo na baada ya hapo akapotea kabisa na hajaonekana hadharani hadi leo.


Ukweli ni kwamba ndani ya kikao kile chs jumapili Slaa alionesha msimamo wake juu ya EL na kudai kuwa watanzania hawatatuelewa wakituona tukipita kumsafisha mtu yuleyule tuliyemchafua awali.

Hivyo Slaa akatoa masharti mawili makubwa. La kwanza ni EL aitishe Press na ajisafishe mwenyewe kabla hajatangaza kuja UKAWA. Aruhusu waandishi wamuulize maswali yote kuhusu Richmond na kashfa nyingine ikiwemo umiliki wa jengo la Ubalozi wa S.Africa na EL ajibu hoja zote kwa maelezo ya kueleweka. Sharti la pili la Slaa ni kuwa EL asupewe nafasi ya kugombea urais kwa sasa kwani ni ngumu kupima dhamir yake kama ni ya kweli. Slaa akapendekeza EL aje CHADEMA na aisaidie UKAWA kuchukua dola bila kugombea Urais.

Lakini Mbowe akampinga sana Slaa na akasema Katibu mkuu hawezi kuweka "ultimutum" ya EL kujiunga na chadema. Mbowe akapuuza mawazo ya Slaa na akaagiza mchakato wa kumpokea uanze mara moja na kesho yake Mbatia akaambiwa atoe tamko la kumkaribisha EL UKAWA.

Hali hii ilimfanya Slaa kujihisi mnyonge na aliyepuuzwa. akahisi hathaminiki ndani ya chama licha ya mchango mkubwa alioutoa kukijenga chadema. jambo la ajabu Mbowe alipopelekewa taarifa hizo alijibu kwa kejeli kuwa liwalo na liwe. yani yuko tayari kumpoteza Slaa na kumkumbatia EL.

Haikujulikana wazi Mbowe ana maslahi gani katika hili la EL na kwanini aamue kuwa na msimamo mkali hivyo wa kumtetea EL.

Inadaiwa tangu jumapili Slaa alipoachana na viongozi wenzie wa UKAWA hadi sasa yupo ndani hajatoka na hakuna mgeni anayeruhusiwa kumuona. Anautumia muda huu kusali na kushauriana na marafiki zake kwa njia ya simu (wengi ni maaskofu) juu ya nini afanye katika kipindi hiki.

Wengi wamemshauri aachane na siasa na ajiuzulu nafasi yake ya SG ndani ya chadema wazo ambalo limeungwa mkono na mkewe Josephine na baadhi ya watu wenye misimamo mikali.

Baada ya ushauri huu mkewe wa Slaa ameonekana kufurahia na ameanza kuelezea kwenye mitandao ya kijamii. Jsna kupitia kundi la Nyakahoja la whatsapp Josephine alisema mumewe ameteseka sana na chama hiki na amekitoa mbali sana. Dr.Slaa alivunjika mkono na hadi sasa ana ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kuitetea chadema. yeye mwenyewe alipigwa na kuharibiwa mimba mwaka 2011 kwa sababu ya chadema halafu leo wanapuuzwa kama vile si chochote ndani ya chama.

Anasema ni afadhali Mbowe angesikiliza ushauri wa Slaa wa EL kujisafisha kwanza kabla hajaja chadema maana kuja bila kujisafisha ni kuwaweka viongozi wote wa chadema kwenye mtego.

Madai ya Mbowe kupewa fedha na EL. Yapo madai kuwa Mbowe amehongwa sh. bil 12 ili kumpokea EL. Fedha hizi ameziweka kwenye akaunti yake binafsi na amewawia kidogo wale aliowaona wanaweza kumchallenge. baadhi ya watu waliopata mgao ni wajumbe wa kamati kuu ili kuwaziba mdomo. na si wajumbe wote bali wale wachache viherehere. baadhi yao ni Godbless Lema (anadaiwa kupokea milioni 120), Peter Msigwa (mil 135), Tundu Lissu (mil 180), Salum Mwalimu (Mil 180).

Pesa hizi ndizo zinazodaiwa kuwafumba macho kamati kuu na kuamua kumpitisha EL bila kufikiri mara mbili. Kitu cha ajabu kamati kuu imefunga dirisha la kuchukua fomu na kusema eti kamati kuu inamuunga mkono Lowassa tu.

Huu ni ujinga ambao hata CCM haiwezi kuufanya. Kamati kuu inatakiwa kuwa neutral. kamati kuu haitakiwi kuwa na mgombea. kamati kuu haitakiwi kuzuia watu kuchuku fomu. acha wachukue wengi kadri iwezekanavyo halafu wachujwe abaki mmoja.

Kama EL anajiamini yeye ni bora zaidi na ana nguvu zaidi kwanini anaitumia kamati kuu kuzuia watu wasichukue fomu? Siku chache zilizopita watu walilalamikia kamati kuu ya CCM kuwa ilikua na mgombea wake mbona hawaoni hili la kamati kuu ya chadema?

Ikiwa madai haya ya kuhongwa kamati kuu ni ya kweli basi chadema inaelekea ukingoni katika siasa za nchi hii. jambo la ajabu viongozi wanaodaiwa kuhongwa akiwemo Mbowe hawajakanusha habari hizi. halafu wanatuma ujumbe kw Slaa eti wakamsihi asiondoke. wajumbe wote waliotumwa wakaishia getini na hawakufunguliwa mlango. mlitegemea mfunguliwe mlango wakati kuna madai mmehongwa na hamjakanusha? kanusheni kwanza ndio muende kumuona Slaa. Au mnataka mkamhonge na yeye? Kama msipokanusha habari hizo mkienda mtafungiwa tena nje maana nyumbani kwa Slaa hakitaingia chochote kilicho kichafu.

Response ya Chadema. ni kama vile hawajali yanayoendelea. na bahati mbaya zaidi vijana wa chadema wameanzisha movement ya kumtukana Josephine kuwa yeye ndio anamponza mumewe. kwenye mtandao wa jamiiforums, facebook ma magroup ya whatsapp wanamtukana sana.

kwenye group moja la wabunge wa chadema wameanzisha movement iitwayo "Josephine Bring Back our Dr". wengine wanamwita mwanamke mpumbavu, wengine wanasema ana hasira ya kukosa ufirst lady, lakini wengine wamefika mbali na kudai anatumiwa na TISS na CCM.

Kimsingi madai yote hapo juu hayana mashiko. Josephine hatumiwi na TISS wala CCM. Hana uchungu wa kukosa ufirst lady wala nini. anachofanya ni kutetea haki ya mumewe. haki ya kuthaminiwa, haki ya kuheshimiwa, haki ya kutoa mawazo yake na kusikilizwa.

Hivi mumeo anapuuzwa kwenye vikao vikubwa vya maamuzi halafu unaambiwa waliompuuza wamehongwa fedha na hawajakanusha habari hizo, halafu ukimtetea mumeo unaambiwa unatumika na TISS. this is ridiculous.

Hakuna cha TISS wala CCM mchawi wa chadema ni chadema wenyewe na mchawi wa ukawa ni chadema. Hizi porojo za TISS ni mbinu inayotumika ili Slaa akiamua kutangaza msimamo wake ionekane anatumiwa na CCM. Chadema acheni siasa za kitoto. hivi Slaa aliyepigania chadema zaidi ya miaka 20 akitoa sadaka maisha yake kwenu ndio wa kutumika na TISS leo aache kutumika huyo EL aliyekuja jana? this is very interesting. chadema kitaingia katika rekodi za dunia za kuwa chama cha kwanza kumtilia shaka mwanachama wake wa miaka 20 na kumuamini mwanachama wa siku moja.

Nini kifanyike? Jambo linaloweza kufanyika na kusaidia kuiokoa chadema na UKAWA kwa ujumla ni mediation. zitafutwe mbinu nzuri za kukutana na Slaa na kuongea nae. aeleze yanayomhusu na chama kioneshe concern ya kuyatatua.

pia kwa kuwa Josephine anaonekana kuwa na nguvu kubwa sana kwa Slaa hivi sasa ni bora Watafutwe wanawake wenye heshima ndani ya chama wakaongee nae. kwa mfano Mama Regina Lowassa, mama Ntagazwa na mama Mbatia waende kumuona mwanamke mwenzao waongee nae. hii itasaidia kupunguza hasira za huyu mama maana tangu juzi anatukanwa mitandaoni akidaiwa ndiye anayemzuia Slaa.

Ni vizuri mambo haya yafanyike mapema maana taarifa zilizopo ni kuwa kufikia wiki ijayo kama chama kitakua hakijatoa msimamo kuhusu Slaa basi yeye atatangaza msimamo wake wa kujiuzulu wadhifa wake chadema na kuamua kuachana na siasa kabisa. kisa wataondoka nchini yeye na familia yake kwenda Italia ambapo ataishi huko kwa miaka mitano kabla ya kurudi nchini na kumalizia maisha yake Karatu. mipango ya Slaa kwenda kuishi Italia kwa miaka mitano inaratibiwa na shirika mija la kiroho la kanisa katoliki na maandalizi yanaendelea vizuri.

Hivyo basi ni vema kazi hii ikafanywa mapema na kwa umakini ili tusivuruge kazi yote ya kuijenga Ukawa na kuujenga upinzani nchini. ukweli ni kuwa Slaa akiamua kujiuzulu siasa za upinzani zitapoteza uelekeo na tutashindwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kuanzia udiwani, ubunge hata urais. maana yake ni kuwa kazi yote iliyofanyika kuujenga upinzani inabomolewa siku moja na kuifanya CCM izidi kushamiri. na ikiwa Slaa ataondoka itachukua miska zaidi ya 100 kupata upinzani mwingine wenye nguvu kama huu. hivyo basi juhudi za haraka zinatakiwa.

Mwandishi wa makala haya ni ndugu A.N Chilongola, mwanachama wa chadema na mkurugenzi wa kampuni ya uwakili ya Chilongola &Advocates iliyopo MabiboDar.anchilongola@gmail.com
Kwahiyo kwa maelezo nlo soma kidogo mbowe kakiweka chama mfukon asa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umewakilisha mawazo yangu kwa asilimia karibia zote. Dr Slaa alistaafu siasa, alivyojitoa CCM na kwenda Chadema hakurudisha kadi yake lakini kwa mujibu wa sheria zetu ukijiunga chama kingine unakuwa umejifuta uanachama kule ulikotoka automatically.

Alivyojiondoa chadema pia hakurudisha kadi vile vile ambazo anabaki nazo kama kumbukumbu lakini hakuwahi kujiunga na chama chochote. Unaweza kuitumikia nchi yako bila kuwa mwanachama wa chama chochote na ndio anachofanya Dr Slaa.

Wengi hamfahamu alichofanyiwa Dr Slaa na chama chake tena watu aliowaamini sana. Inabidi tumuache mzee ampumzike na aliyofanya yanatosha.

Turudishe imani na matumaini kwa vijana waliopo kama Nassari, Mnyika, Mdee n.k ili kuijenga Chadema mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nassari sijaona kama ana upepo huo labda unambie msigwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za vyama sio za Nchi hahahahahahah. Hivi wewe bavicha sikuizi umekuaje?Hizo siasa za Nchi ndio siasa gani?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.

Najua kwanini unajibu kwa jazba, najua ni wapi nilikupa kitu inawasha ndio maana unajaribu kusawazisha. Nina uelewa mpana na kuweza kujua muelekeo wa aina ya majibu. I know how to provoke guys of your Calibre, I know that I get you right in your neck. Now your dancing my tunes right in my fingertips. Keep it up.
 
Ukiwasoma wafuasi wengi wa Chadema humu wanapenda sana kuona Dr Slaa akirejea Chadema.

Ila hawapo tayari kuonyesha hisia zao hadharani kulingana na jinsi walivyomtenda.

Wakijenga hoja kuwa mbona aliemkimbia amerudi ccm...

Kwa kuweka kumbukumbu sawa, Dr Slaa alitangaza kuachana/kustaafu na siasa za vyama kwa maana za majukwaani...

Pili hajawahi kurudi CCM, hakuna kiongozi yoyote yule wa CCM aliempokea kama ilivyotokea kwa viongozi wengine waliorejea.

Na hata akitaka kurudi siasa za majukwaani sidhani kama anaweza kurudi Chadema..

Kashfa mlizompa 2015 zinatosha sana, endeleeni kukomaa na waliopo Chamani.

Ni mda muafaka sasa kuinua mioyo ya akina Mnyika, Nassari, Salumu Mwalimu na wengineo wenye mioyo na upendo wa dhati kwa Chadema ili kusonga mbele...

Siku Chadema watakapoyatambua mapungufu ya Mbowe ndio siku watakayopiga hatua moja mbele....
Sipendi slaa arudi kwenye chama chochote cha upinzani labda amuache mushumbusi aliyeshika akili yake
 
Slaa alisema amestaafu siasa za vyama sio za nchi. Ukiteuliwa na Magufuli ww ni mwanaccm taka usitake. Hata Magufuli alishasema hilo, kwake hamna mteule neutral.
Pamoja mkuu, shukran kwa kuweka rekodi sawa.
 
Back
Top Bottom