Hivi 'chopa' ya CHADEMA inatumika Arusha na Moshi pekee?

Usikimbie mada, mada haiongelei uchaguzi mkuu, kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2011 CHADEMA imekuwa ikifanya siasa na 'CHOPA' hapo Arusha tu, kama unabisha, ni kwanini kwenye uchaguzi wa madiwani chopa haikuvuka mipaka ya Arusha?

Tuwaambie tunapoelekea na chopa mtulipue kama Saitoti! Wakati wa kampeni chopa imetua Tanga, Manyara, Kondoa, Bahi ispokuwa maeneo ya Morogoro na nyanda za juu kusini, tulitaarifiwa kwamba kuna mitambo ya kuangushia helkopter imetegwa, kwa hiyo tumieni magari tu. Pia Chama kinaendelea kufunga DVR kila kona na ndani ya mwezi huu tutatikisha mikoa yote... Wewe hujui kwa sababu ni gamba tu, unaropoka bila hata utafiti...
 
mkuu tayari povu kibao wazee wameguswa pole mkuu.

Povu? We kibwengo nani atoe povu kwa kipi hasa? Huo wivu wenu wa kijinga Chama kina miaka zaidi ya 50 hata bus tu hamna kutokana na kila kiongozi kujali wizi,na kujaza tumbo,kuuza unga,kuiba raslimali za taifa,kung'oa watu meno na kucha,kumwagia watu tindikali hebu uelezee umma wa jf ccm inamendeleo gani imefanya hapa Tanzania kwa kipindi chooote cha uhai wake na sasa hivi kinakwenda kufa?

Chadema muda mfupi tu wanayo CHOPA inawaumiza roho na mlivyo na roho mbaya kinawawasha hamuachi kuisemasema,badala ya kuleta maendeleo mumekalia wizi na umalaya utawasaidia nini nyie
 
Zanzibar ni sehemu ya jamhuri na kwa taarifa yenu itaendelea kubaki hivyo, mtake msitake.
Muda si mrefu utafahamu kuwa Zanzibar ni nchi jirani kama ilivyo kenya na Uganda!

Wenye akili timamu wanawekeza nguvu zao nyingi katika nchi yao! "kwanini utumie kisu chako kikali kumchinja mnyama asiyeliwa?"
 
WanaJF!

Ni imani yangu tuna tambua kuwa Tanzania yetu ni moja na watanzania wote ni wamoja katika mambo yote yanayohusu taifa letu, ikiwemo mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, na wote kama watanzania tuna stahiki kupata mambo haya kwa usawa.

Katika hali kama hiyo ya kupata hayo mambo kwa usawa, nasikitika kusema kuna kundi fulani la watu aidha hawapo tayari kutoa usawa huo ama hawajui kuwa ndio tamaduni na desturi yetu watanzania kushiriki kwa usawa kwenye mambo tajwa hapo juu.

Katika kulisisitiza hili, ningependa tutizame siasa za CHADEMA, hivi karibuni umefanyika uchaguzi wa madiwani kwenye zile kata ambazo madiwani wake aidha walitimuliwa ama walifariki hivyo kata kubaki wazi, katika chaguzi zile CHADEMA walifanya ubaguzi mkubwa mno.

Kata zilizo kuwana uchaguzi zilikuwa maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwemo Mbeya, Morogoro, Mara na Manyara, lakini 'CHOPA' ya CHADEMA ilipaa Arusha tu na wala haikuchungulia sehemu nyingine yoyote hapa nchini.

Aidha, huko Arusha 'CHOPA' ya CHADEMA ilikuwa busy kwenye kata zote, yani haikuwahi kutokea kampeni zifanywe bila matumizi ya 'CHOPA' hiyo kwa kipindi chote cha uchaguzi wa kata za pale Arusha.

Kama hiyo haitoshi, hivi sasa kamanda wa anga, bwana Mbowe, yupo Hai kama mbunge wa jimbo hilo, lakini kwa ubabe wake amehamua atumie 'CHOPA' hiyo kufanya shughuli zake zote, yani kama mbunge na pia mwenyekiti wa chama.

Kwa kufanywa hivyo inakuwa sio sawa, kama itakuwa hivyo basi na majimbo mengine nayo yapelekewa 'CHOPA' ya CHADEMA na isibaki Arusha na Moshi pekee, kwani ikiendelea hivyo itatafsiriwa kuwa CHADEMA ni chama cha ukanda.

maswali kama hayo usilete hapa, nenda kinondoni mtaa wa ufipa yalipo makao makuu ya Chadema kawaulize kwa nini chopa ilitumika arusha na moshi, na kama unahisi ni ubaguzi fikiria yafuatayo

1) kwanini mitambo ya kichakata gesi ifungwe bagamoyo na sio mtwara?

2) Amefanya nini la maana JK hadi kuzawadiwa heshima ya U dokta na kuachwa Nyerere aliyepambana hata kufanikisha uhuru na Muungano

3) Kwa nini JK hajazungumzia kashfa ya madawa ya kulevya hata sasa na hajachukua hatua yeyote licha ya kuwa alikiri kuwa na majina ya wauza unga kwa zaidi ya mwaka? Au tuamini kimya kimya ndani ya hayo majina na lake limo!
 
CCM sio chama cha kibaguzi, kina wasomi na wasio wasomi, hao watu wa mitaani ndio tuna wahitaji kweli ndani ya CCM kokote walipo CCM ipo na ina wahitaji, sasa kama ulidhani CCM ipo kwa ajili ya kundi fulani la watu basi hiyo sio CCM ya mwenyekiti wake Kikwete, labda hiyo unaijua wewe.
Ur thinking capacity is below the normal
 
WanaJF!

Ni imani yangu tuna tambua kuwa Tanzania yetu ni moja na watanzania wote ni wamoja katika mambo yote yanayohusu taifa letu, ikiwemo mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, na wote kama watanzania tuna stahiki kupata mambo haya kwa usawa.

Katika hali kama hiyo ya kupata hayo mambo kwa usawa, nasikitika kusema kuna kundi fulani la watu aidha hawapo tayari kutoa usawa huo ama hawajui kuwa ndio tamaduni na desturi yetu watanzania kushiriki kwa usawa kwenye mambo tajwa hapo juu.

Katika kulisisitiza hili, ningependa tutizame siasa za CHADEMA, hivi karibuni umefanyika uchaguzi wa madiwani kwenye zile kata ambazo madiwani wake aidha walitimuliwa ama walifariki hivyo kata kubaki wazi, katika chaguzi zile CHADEMA walifanya ubaguzi mkubwa mno.

Kata zilizo kuwana uchaguzi zilikuwa maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwemo Mbeya, Morogoro, Mara na Manyara, lakini 'CHOPA' ya CHADEMA ilipaa Arusha tu na wala haikuchungulia sehemu nyingine yoyote hapa nchini.

Aidha, huko Arusha 'CHOPA' ya CHADEMA ilikuwa busy kwenye kata zote, yani haikuwahi kutokea kampeni zifanywe bila matumizi ya 'CHOPA' hiyo kwa kipindi chote cha uchaguzi wa kata za pale Arusha.

Kama hiyo haitoshi, hivi sasa kamanda wa anga, bwana Mbowe, yupo Hai kama mbunge wa jimbo hilo, lakini kwa ubabe wake amehamua atumie 'CHOPA' hiyo kufanya shughuli zake zote, yani kama mbunge na pia mwenyekiti wa chama.

Kwa kufanywa hivyo inakuwa sio sawa, kama itakuwa hivyo basi na majimbo mengine nayo yapelekewa 'CHOPA' ya CHADEMA na isibaki Arusha na Moshi pekee, kwani ikiendelea hivyo itatafsiriwa kuwa CHADEMA ni chama cha ukanda.

Kwa hiyo Tangu mwaka 2005 helkopta haijatumika kwingine?

1:Kampeni za udiwani ziliratibiwa na kanda na uchaguzi uliopita uongozi wa kanda ya kaskazini ukishirikiana na wanachama wake ulifanya arrangement ya chopa.Hii ndiyo maana ya kugatua madaraka mzee.Fanya utafiti

2:Chadema kitatumia njia zote za usafiri tena zaidi ya helkopta katika mikutano yake ili kuongeza ufanisi maeneo yote nchini.Habari utaisikia kuanzia leo kama ratiba inavyoonyesha.Tafadhali urudi hapa kuomba radhi kwa uongo wako na hisia hasi
 
Mkuu wangu HAMY-D.

Hiyo CHOPA ni kwa ajili ya watu wa Kaskazini tu.
 
Last edited by a moderator:
Wewe nae ni fisadi tu maana kila ukiweka post lazima ukadai chako, na inaelekea unalipwa zaidi wewe.
Mtu anaetaka kulikomboa taifa hajadili upande mmoja kila siku kuna maovu mangapi chama tawala wanafanya, umeyapa nafasi ya kuyajadili zaidi ya kutetea hata kama ni maovu? Hoja zako hapa ni kutetea buku saba na si kukomboa taifa kama unavyodai.
 
We hayawani wa kike hivi Zanzibar wanakaa watu au hayawani? Tena fisi wanaopenda kuona damu za watu zikimwagika,kwa risasi,kiwamwagia watu wasio na hatia tindikali hakufai kuishi watu huko ni matatizo,halafi Chadema ni chama cha Tanganyika sio cha Zanzibar,wanataka kuvunja muungano kwa tamaa ya Madaraka akima Sharif Hamad na Karume haina haja Cdm kuwa Zanziba ile ni nchi nyingine apart from Tanganyika

Kinawapeleka nini huko kwa "mahayawani". Ukipenda boga upende na ua lake.
 
WanaJF!

Ni imani yangu tuna tambua kuwa Tanzania yetu ni moja na watanzania wote ni wamoja katika mambo yote yanayohusu taifa letu, ikiwemo mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, na wote kama watanzania tuna stahiki kupata mambo haya kwa usawa.

Katika hali kama hiyo ya kupata hayo mambo kwa usawa, nasikitika kusema kuna kundi fulani la watu aidha hawapo tayari kutoa usawa huo ama hawajui kuwa ndio tamaduni na desturi yetu watanzania kushiriki kwa usawa kwenye mambo tajwa hapo juu.

Katika kulisisitiza hili, ningependa tutizame siasa za CHADEMA, hivi karibuni umefanyika uchaguzi wa madiwani kwenye zile kata ambazo madiwani wake aidha walitimuliwa ama walifariki hivyo kata kubaki wazi, katika chaguzi zile CHADEMA walifanya ubaguzi mkubwa mno.

Kata zilizo kuwana uchaguzi zilikuwa maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwemo Mbeya, Morogoro, Mara na Manyara, lakini 'CHOPA' ya CHADEMA ilipaa Arusha tu na wala haikuchungulia sehemu nyingine yoyote hapa nchini.

Aidha, huko Arusha 'CHOPA' ya CHADEMA ilikuwa busy kwenye kata zote, yani haikuwahi kutokea kampeni zifanywe bila matumizi ya 'CHOPA' hiyo kwa kipindi chote cha uchaguzi wa kata za pale Arusha.

Kama hiyo haitoshi, hivi sasa kamanda wa anga, bwana Mbowe, yupo Hai kama mbunge wa jimbo hilo, lakini kwa ubabe wake amehamua atumie 'CHOPA' hiyo kufanya shughuli zake zote, yani kama mbunge na pia mwenyekiti wa chama.

Kwa kufanywa hivyo inakuwa sio sawa, kama itakuwa hivyo basi na majimbo mengine nayo yapelekewa 'CHOPA' ya CHADEMA na isibaki Arusha na Moshi pekee, kwani ikiendelea hivyo itatafsiriwa kuwa CHADEMA ni chama cha ukanda.

Pole sana Hamy D Nadhani ww hapa jamvini unapaswa kupewa darasa yawezekana unajua na unafanya makusudi au hujui kabisa,mosi sio kweli kuwa chopa ya chadema wakati wa uchaguzi wa kata uliofanyika nchini haikwenda maeneo mengine kwa mfano tu midogo Tanga sio kilimanjaro huko ilikwenda pili Monduli ilikwenda huku nako HAI,nadhni kuna hoja Za msingi unaweza kupost humu ambazo jamii ya kitanzania na vizazi vijavyo vinaadhirika juzi tu watoto wa darasa la saba nchini wamefanya mitihani ya majiribio zaidi ya wilaya 40 mitihani hiyo kwa upande wa hisabati haina majibu,tembo wetu wanauwawa kwa takwimu zilizopo kila siku ndovu zaidi ya 30 wanauwawa,madawa ya kulevya yanawadhulu vijana na yanaingilia JKIA ,na wanayowadhulu ni vijana ww unangangana na guity politcts za miaka ya zamani pole.Think twice .

  • :wave:
 
Mkuu kwani umechangia bei gani kwenye hiyo chopa! Au ndio yale mambo, ndoa afunge mwingine shanga uvae wewe.
 
Zanzibar ni nchi ya kigaidi,na iliyojaa mafezuri wanaojifanya wanamjua sana mungu!

Mbona hizo hisia zako uzionyeshi na kwa CHADEMA na kitendo walicho mfanyia kada wa CCM, Tesha, cha kumlowanisha na tindikali usoni na maeneo mbalimbali ya mwili?

Kama kweli wewe una utu basi ingekuwa ni vyema ukajumuika nasi katika kuiponda mawe CHADEMA kwa vitendo vyake vya kigaidi vya kumwagia raia wa Tanzania tindikali tena kisa mambo ya kiitikadi tu.
 
Back
Top Bottom