VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Kisiasa, unapoisha uchaguzi mmoja maandalizi ya uchaguzi mwingine huanza. Maandalizi ya uchaguzi wa mwaka huu 2020 (kuihusu CCM pekee) yalianza tangu mwaka 2015. Makada walijipanga kutetea majimbo na kata na wengine wakitamani kuzipoka kata na majimbo kutoka kwa wasasa. Maandalizi ya kiuchaguzi hayakufanyika kwa wapinzani tu. Wao waliminywa vya kutosha na kutisha na kulazimishwa kufanya mambo yao ya kisiasa kimyakimya na sirini kama kuuza gongo, bangi au ngada.
Makada wa CCM, kabla ya maigizo yaliyoanzishwa jana ya kutoa namba ya simu ya kuripoti vitendo vya rushwa, walishatoa rushwa na kujijenga ipasavyo. Tazama ayafanyayo Naibu Spika Dr. Tulia kule Mbeya. Amekuwa akijibanza kwenye taasisi yake ya Tulia Trust kugawa rushwa na kusaka ushawishi ili aweze kugombea na kushinda jimbo la Mbeya Mjini linaloshikiliwa na CHADEMA. Mtazame Silvestry Koka wa Kibaha Mjini. Ameshagawa baiskeli na pikipiki kwa makada wa CCM tayari kutaka kuutetea ubunge wake. Majimbo yote hali ipo hivyo, wataripotiwa wangapi? Watafanywaje?
Rushwa, as always, imeota mizizi na kutamalaki ndani ya CCM. Rushwa ndiyo inayowapa ushindi makada ndani ya CCM na hata kwenye uchaguzi mkuu. Rushwa ni njia pekee ya kuibuka kidedea huku ukichekelea ndani ya CCM. Mafao ya Ubunge mara baada ya kuvunjwa kwa Bunge ndiyo hutumika kugawa mahela kwa makada na wananchi na kuwawezesha watu kutetea viti vyao. Ni vichekesho, utapeli na ulaghai kusema kuwa CCM inachukia rushwa. Sisi wanaCCM tunajua ukweli huo. Hakuna haja ya kudanganyana.
Kazi ya kupambana na kuzuia rushwa ni ya TAKUKURU. Lakini, wakati kama huu wa uchaguzi, CCM ndiyo huwakingia vifua makada wake wanaotiwa mbaroni kwa rushwa na kuwaharibia kazi TAKUKURU. Inashangaza kutapeli na kulaghai wananchi kuwa chama chetu cha CCM kinachukia na kupambana na rushwa. Ni ajabu inayofaa kuingia kwenye kitabu cha maajabu ya kidunia.Wananchi wamekosa nini hadi wadanganywe na kulaghaiwa kiasi hiki? Kinaendelea nini kwenye kukamatwa kwa Rage kule Tabora?
Uchaguzi ndani ya CCM bila rushwa hauwezekani!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Nzega, Tabora)