Hivi biashara ya mayai ya kware iliishia wapi jamani?

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,968
Hii biashara ilivuma sana hasa ikihusisha na nguvu za kiume na watu walipiga hela sana kwa kuanzisha ufugaji wa kware na kuuza mayai yake lakini sasa naona kimyaa. Watu wakianza kuvumisha kitu hasa kukihusisha na nguvu za kiume kinapata soko sana. Akiibuka mtu leo na kusema mayai ya nyoka yanaongeza nguvu za kiume msako mkali utaanza kutafuta mayai ya nyoka popote mashimoni na mapangoni na ukitaka watu waanze kufuga nyoka tangaza kuwa mayai yake yanaleta nguvu za kiume
 
unganisha na biashara ya kuku wa kuchi, na kikombe cha babu wa loliondo, vyote hivyo vinaendana, ni dugu moja.
 
Ndo maana kuna siku kwenye Friji ya ndugu yangu flani nliyaonaa Mengiii... Ilaa baadae nkakuta hayaliwii tenaa yapoo tuu
 
Dah ile heading ukiisoma ilikuwa inazuzua hatari,

"... Biashara yenye utajiri ambayo hakuna bank itataka uijue.. "

Bahati mbaya sikuwa na hela kipindi hicho nahic nngeunguzaga account aisee
Mkuu
Ilikuwa Kama Serikali Ya Viwanda
Yaani Kilikuwa Kiwanda Kidogo Kikanyoosha Watu Sana
 
Hahaha nimecheka sana aisee.

Sijui ilikuwa project ya mjanja gani ile.

Watu walifuga sana kware.

Bila kusahau biashara ya sungura pia, nayo ilishika kasi sana, sijui bado ipo?
 
Ukisema kinyesi cha mtot aliyezaliwa tarehe 29/2 ya kila mwaka inaongeza nguvu za kiume itakuwaje? Maan ni baada ya miaka kadhaaa
 
Back
Top Bottom