Hivi Bi. Kijo ni mwanasiasa ama mtetezi wa haki za bidadamu?

ULIMI MKUBWA

Senior Member
Mar 27, 2016
195
182
Yanatokea mengi sana tanzania mfano ubakaji wa wanawake na wasichana lakini pia uuaji wa maalbino hali kadhalika watoto wanaotelekezwa na wazazi wao ni mengi sana nikianza kuyataja hapa sitamaliza kuyaandika... Mishahara kidogo kwa watumishi wa umma kama maaskari, walimu, madaktari n.k matumizi ya madawa ya kulevya n.k

Chakushangaza ni kwamba bi kijo hajawahi kemea mambo tajwa hapo juu!!!

Anatetea na kulaani kitendo cha wabunge waliokiuka sheria za bunge wazi wazi kuwa hawajatendewa haki? Je bisimba kwa nini hajawahi laani kitendo cha wabunge wa chadema cha kusema hawamtambui rais magufuli?

Huyu mama nadhani ana kaubia na chadema maana anaacha mambo ya kitaifa yeye anakuwa one sided !!!!

Binafsi sioni umuhimu wakuwa eti na taasisi ya haki za binadamu wakati hatuoni juhudi zozote zinazofannywa na lrhc!!

Anashindwa tetea watoto wanaokaa chini mashuleni kwa kukosa madawati yeye anatetea watu ambao wamekiuka sheria waziwazi

Binafsi mimi kama mtanzania nimechukizwa na kuhudhunishwa sana n kitendo cha ni kijo kujiingiza kisiasa zaidi!!
 
Siku kadhaa zilizopita yametokea mauaji ya kinyama kanda ya ziwa, lakini huyu mama na kituo chake hawakuwahi kudiriki kutoa kauli hata mara moja. Kwake yeye suala la mauaji si suala la haki za binadamu, ila akisikia tu Chadema wameadabishwa basi utamsikia haraka haraka akiitisha press conference.
 
Diamonds alipopata mtoto Watanzania wote walijua. Sio kama mastar wengine hawapati watoto. (Siasa kwa sasa ipo juu Tanzania ndio maana unasikia akiongea mambo ya siasa tu. Hayo mengine hata akiongea hayapewi media kama akiongelea mambo ya siasa.)
 
Siku kadhaa zilizopita yametokea mauaji ya kinyama kanda ya ziwa, lakini huyu mama na kituo chake hawakuwahi kudiriki kutoa kauli hata mara moja. Kwake yeye suala la mauaji si suala la haki za binadamu, ila akisikia tu Chadema wameadabishwa basi utamsikia haraka haraka akiitisha press conference.[/QUOTE?]

wacha umbea wa lumumba buku 7 na UVCCM
huyu mama ni mmoja alifanya ccm na huyo raisi wenu kuchukua nchi.


swissme
 
Back
Top Bottom