Hitimisho: CHADEMA kuna ombwe la uongozi

Hitimisho: CHADEMA kuna ombwe la uongozi

Samahani kidogo, naomba kujua una elimu gani na umesomea wapi..?
Pia nataka kujua kama umewahi kushiriki shughuli yeyote ya kisiasa ama kuwahi kugombea hata ujumbe wa serikali za mitaa tu..?
Kuwa na uelewa wa siasa sio lazima ugombee serikali za mitaa au ubunge. Siasa ni taaluma inayosomewa shule.
Isitoshe, ni kifuata rules and morals.
Am a political scientist, nimesoma chuo gani haikuhusu. Jadili hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wooow, kama vyuo vyeti vinazalisha political scientist wa mfano wako basi tuna tatizo kubwa zaidi kuliko nilivyodhani.
i} Hakuna unachokijua kuhusu siasa zaidi ya jina lenyewe "siasa".
ii} Kuna mahusiano yasiyo ya moja kwa moja baina ya pilitical thoughts za akina Niccolo Machiavelli na kinachoendelea kwenye siasa zetu, na hii inasababishwa na vitu vingi sana. Kudhani kuwa kumuelewa sana Machievelli ni kuwa mwanasiasa bora wa kizazi chetu ni kujidanganya.

Either way, sijajua najadili na mtu mwenye ufahamu kiasi gani kwa kuwa umekataa kudisclose taarifa ya obvious kama vile chuo ulichosoma na elimu uliyonayo....unatumia ID anonymous, unashindwa kujenga na kutetea hoja, unaulizwa kama umesoma na umesoma wapi unashindwa kusema na bado unataka kujadili na mtu ambaye ID yake ni verified, anajulikana elimu yake na kazi yake, anajenga hoja na kupinga hoja kwa hoja. Hakuna ulali kwenye hili, naomba nikuache na u-fake wako.
 
Juliana wewe ni Mbunge Ila sina hakika na uwezo wako wa kufikiri! Na siyo ajabu ukawa ufikiri Ila "unawaza" na kuandika tu, ili kuendelea kuhalalisha status yako baada ya kukosa uungwaji mkono kutoka kwa Vijana wengi Nchini! Ukweli wewe "unawaza" Ila uwezi kufikiri kabisa tena ni wa kupuuzwa tu!

Tangu umeamia kwa these blank devils of CCM na wewe umekuwa hivyo hivyo tu,

Twambie wewe tangu umeamia Chama cha Mapunduzi, umefanya nini kama unaona udhaifu wa wengine zaidi ya kuwashitaki wabunge wenzio kwa speaker kama mtoto mdogo!!!!! wewe umebadilisha nini uko CCM!!! , kama Kuna udhaifu upinzani na unasema uliposema ukatimuliwa CHADEMA, uko CCM umeshauri nini kikafanyika??

Uwezi kuendelea kujipa ualali wakati tiari umekatika mkiwa wewe ni wa kutupwa tu bila shaka maana sura na rangi yako vina mashaka na damu ya unafiki na Msaliti mkubwa wa MAGEUZI.

Kaa endelea kura hisani ya ubunge wako, hama fikiri tofauti, Kuna watu wamekuwa vilema wa Muda na Maisha, Kuna watu wamenyanganywa Mali zao, Kuna watu wameteswa, Kuna watu wanapitia tanuru la moto, Kuna watu wamepoteza maisha Kama Alfonce Mawazo, na wengine wengi, na Kuna watu wamefungwa, mambo yote haya yamesababishwa na hao unawaza wana uhalali na miliki ya Taifa letu!! Wewe siyo mfuasi wa Itikadi na falsafa Bali mkate na tamaa ya maitaji yako, uliyasaliti MAGEUZI kwa tamaa ya mkate wa Muda endelea "kuwaza " hivyo wakati sisi tukipigania MAGEUZI ya dhati.

Tumia Elimu yako vyema kuliko kuitumia kinyume na malengo yake, jifunze kuchutama dada, ulisha amua kuwa Msaliti wa MAGEUZI endelea kuwa hivyo hivyo tu na dhambi hii haitakuacha salama, utazikubuka nyakati kama zile!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wooow, kama vyuo vyeti vinazalisha political scientist wa mfano wako basi tuna tatizo kubwa zaidi kuliko nilivyodhani.
i} Hakuna unachokijua kuhusu siasa zaidi ya jina lenyewe "siasa".
ii} Kuna mahusiano yasiyo ya moja kwa moja baina ya pilitical thoughts za akina Niccolo Machiavelli na kinachoendelea kwenye siasa zetu, na hii inasababishwa na vitu vingi sana. Kudhani kuwa kumuelewa sana Machievelli ni kuwa mwanasiasa bora wa kizazi chetu ni kujidanganya.

Either way, sijajua najadili na mtu mwenye ufahamu kiasi gani kwa kuwa umekataa kudisclose taarifa ya obvious kama vile chuo ulichosoma na elimu uliyonayo....unatumia ID anonymous, unashindwa kujenga na kutetea hoja, unaulizwa kama umesoma na umesoma wapi unashindwa kusema na bado unataka kujadili na mtu ambaye ID yake ni verified, anajulikana elimu yake na kazi yake, anajenga hoja na kupinga hoja kwa hoja. Hakuna ulali kwenye hili, naomba nikuache na u-fake wako.
Kama hunifahamu basi usinidharau. Ila kwa kuwa wewe umejitambulisha na tunakuona kila unalofanya, tuna nafasi kubwa ya kukushauri.
Na kama vyuo vyetu ndio vinazalisha wanasiasa kama wewe basi tuna hasara kama Taifa.
Kama tuna wasomi wasiojua kuihoji serikali ili itekeleze kile wananchi wanachokitaka; wasio na critical thinking, kama tuna wabunge waliojaa gubu kwa kufukuzwa; kama tuna wansiasa wenye kujipendekeza kama wewe, kwa kweli tuna hasara.
Shonza wewe ulionyesha usaliti Chadema, hukutaka kuwatii viongozi wako ukafukuzwa. Wasaliti wenzako unawajua wote mlifukuzwa.
Hicho kinawauma sana, ndio maana kila kukicha mnaishabulia Chadema tu.
Umesahau hata majukumu yako kama Mbunge kazi yako ni kushambulia Chadema maana umejaa uchungu na hasira za kufukuzwa.
Kama ulikuwa na uwezo kisiasa, ungegombea jimboni uone kama utachaguliwa, sio huo ubunge wa kupewa baada ya kufanya usaliti wako.
Nakushauri hebu punguza jazba, try to be yourself, kisha jiulize unatakiwa kuifanyia nini nchi yako.
Ni kweli kufukuzwa kunauma, lakini wewe samehe na uanze maisha mapya, maadamu ubunge unao.
Nakwambia hivyo, kwa sababu sijawahi kuona post wala mchango wako wa maana bungeni zaidi ya kuilalamikia Chadema.
Yaliyopita si ndwele, tugangr yajayo. Achana na Chadema, fanya siasa zako ndani ya CCM, mambo yatakwenda tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tapatalk_1501845248438.jpeg
mtaucheza huu muziki mpaka 2020
 
AMANI IWE JUU YENU ENYI WAJA WEMA WA BWANA MUNGU WANGU...!!!

Naomba niwaombe radhi kwa kukaa kimya na kutochangia lolote kwa muda mrefu katika jukwaa hili muhimu. Naomba nichukue fursa hii kuendelea kuwafikirisha katika mambo muhimu ya kisiasa yanayoendelea katika siasa za nchi yetu hasa kambi ya upinzani. Wachambuzi mbalimbali, wasomi na waandishi wameendelea kuandika wakijaribu kutoa maoni yao na mitazamo mbalimbali mimi binafsi naamini kuwa SINTOFAHAMU iliyoikumba kambi hiyo inatokana na OMBWE LA UONGOZI.

Nchi sasa imetulia, nchi inasonga mbele na watanzania wameendelea kushuhudia UONGOZI uliotukuka na wenye nia ya kweli ya kuwakomboa na kutimiza ndoto na kiu yao ya muda mrefu ya kupata maendeleo.
Mkuu Juliana Shonza, kwanza naunga mkono hoja.
Lile la Nasari, na hili la Lissu, ni uthibitisho wa hoja zako kwenye bandiko hili.

Pili naomba angalia PM yako, imenibidi niku PM maana uvumilivu umenishinda.

P
 
Hahaha kaka, PM ni umbea, ukitaka mawasiliano yenu yawe siri mtafute kwa number za wizara kisha upate number yake binafsi, unamuomba nini huko PM?!
Huwezi kuja hadharani kisha unanong'oneza, anyway kama umeomba mkapate chakula cha mchana au jioni pamoja,nikutakie ulaji mwema.
 
Viti maalumu vilikua kwa wasioona, wasiosikia, vilema. Wanawake waliongezwa kwasababu walikuwa hawachaguliki licha ya wao kuwa wengi. Siku hizi viti maalum hadi wanaume tena wenye uwezo kujieleza na kushindana kisiasa.
Halafu viti maalumu wasio chaguliwa, ndio wanapewa unaibu waziri, uwaziri, ukatibu ukuu, uwenyekiti wa NEC, ukuu wa mikoa, wilaya na ukurugenzi wa halmashauri. Unakataliwa na wananchi kwa chujio la haki ya kuomba na kukataliwa, halafu unakuwa mkubwa kuliko hata aliyechaguliwa na wananchi.
Halafu watu wanasema serikali inahujumiwa, wakati hawa viti maalum ndio wahujumu wakubwa.
Katiba ingeondoa viti maalumu vya leo irudishe vile hasa maalum, viziwi, vipofu, vilema na kama hivyo vingine.
 
Chakula ya mtaa wa lumumba.

AMANI IWE JUU YENU ENYI WAJA WEMA WA BWANA MUNGU WANGU...!!!

Naomba niwaombe radhi kwa kukaa kimya na kutochangia lolote kwa muda mrefu katika jukwaa hili muhimu. Naomba nichukue fursa hii kuendelea kuwafikirisha katika mambo muhimu ya kisiasa yanayoendelea katika siasa za nchi yetu hasa kambi ya upinzani. Wachambuzi mbalimbali, wasomi na waandishi wameendelea kuandika wakijaribu kutoa maoni yao na mitazamo mbalimbali juu ya yale yanayoendelea katika kambi ya upinzani nchini, wengi wao wamesema kuwa yanayoendelea CUF na CHADEMA ni matokeo yanatokana na NGUVU YA VIPANDE VYA RUPIA vilivyoingia katika kambi hiyo tangu wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015. Kwa upande wangu nimekuwa nikijaribu kutoa mwelekeo mwingine wa fikra, mimi binafsi naamini kuwa SINTOFAHAMU iliyoikumba kambi hiyo inatokana na OMBWE LA UONGOZI.

Septemba 10, 2015 niliandika kuwa FEDHA ni tatizo lakini tatizo halisi ni kukosa Uongozi imara, hata sababu zilizopelekea kupokea FEDHA hiyo na kumpokea aliyezitoa kunatokana na sababu kuu ya OMBWE LA UONGOZI, nilionyesha udhaifu huo kwa maandishi haya CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

August 31, 2016 mwaka mmoja baadae na hasa baada ya kushindwa kwa operesheni ya UKUTA niliandika tena kwa msisitizo Msisitizo; CHADEMA kuna ombwe la uongozi nikieleza namna mipango yao ilivyo ya hovyo na unrealistic, ambayo imekuwa inashindwa wakati wote, nikaeleza kwa kina kuwa tatizo hasa ni OMBWE LA UONGOZI.

Na leo naandika tena nikihitimisha mjadala huu, kwa maana nimejiridhisha kuwa hawa ni watu wenye macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii wao ni kama wafu ama punda aliyefungwa hatamu, wakivutwa kulia wanafuata na wakigeuzwa kushoto ndio unakuwa mwelekeo wao. Hawana hoja, hawana mpango kazi na hawana ajenda, bado ni wanaharakati wanaoendeshwa kwa matukio.

Niliwahi kusema na kutoa ushauri katika vikao na kwa viongozi wa CHADEMA wakati nikiwa mwanachama wa Chama hiko kuwa "sina IMANI na uwezo na maarifa ya Mwenyekiti MBOWE kukivusha Chama katika wakati huu, ni vyema na ni kutokana na utaratibu wa kidemokrasia ndani ya Chama uliokuwepo kikatiba watu wengine waruhusiwe kugombea na ikiwa wanachama wengi watakubali kufanya mabadiliko ya Mwenyekiti, UAMUZI wao uheshimiwe, miongoni mwa wanaotaka mabadiliko hayo ni pamoja na Mimi." Baada ya kusema hayo niliondolewa CHADEMA. Lakini sikukaa kimya, niliendelea kusema na kukosoa aina ya uongozi dhaifu wa Kambi ya upinzani na nilifanya hivyo kwa maslahi mapana ya nchi yangu, nikaandika Ushuhuda: Freeman Mbowe ni kiongozi dhaifu nikiuambia Umma kuwa lipo tatizo kubwa kwenye upinzani nchini linalotokana na udhaifu wa Viongozi wake.

Kama ilivyo kawaida ya Vijana wa UFIPA wakajitokeza kwa wingi, wakitukana na kunikosoa bila hoja, wakisifu Ujio wa LOWASSA kwenye chama chao, wakipongeza uamuzi wa Mbowe wa kumuondoa SLAA na kumuweka MASHINJI, nilipowaambia Chama chao kimepotezwa mwelekeo na hakiungwi tena mkono na watu wenye akili na wanaojielewa, watu wote waliokuwa wakiandika na ku-praise upinzani wamegeuka na wengine wameduwaa kwa kinachoendelea kwenye upinzani, wamebaki wachache wasiojielewa na ambao binafsi niliwapuuza na kuwaambia watanzania wawapuuze kwa maneno haya Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu wengi katika umma wa watanzania wameendelea kuiona rangi halisi ya watu hawa na nashukuru wamekubaliana na mimi kuwapuuza watu wapuuzi. Kwanini wasiwapuuze kama leo kete yao ya turufu ni WEMA SEPETU, ndio mtoa hoja ndio msemaji na mtetezi wa upinzani, kwanini watanzania wasiwapuuze ikiwa MANGE ndio jiwe kuu na mwamba unaotumainiwa, kwanini msipuuzwe..???

Nimeandika hapa nifunge mjadala huu, kwa kuwa watanzania wameshashuhudia na imedhihirika kwao juu ya udhaifu wa upinzani, na namshukuru BWANA MUNGU WANGU kwa upendo wake kwa watanzania akatufunulia yale yaliyomo sirini mwao, YEYE ni shahidi na mwanga unaotuongoza.

Nchi sasa imetulia, nchi inasonga mbele na watanzania wameendelea kushuhudia UONGOZI uliotukuka na wenye nia ya kweli ya kuwakomboa na kutimiza ndoto na kiu yao ya muda mrefu ya kupata maendeleo.
 
Hivi Juliana Shonza ombwe la uongozi CHADEMA kwa nini linakuuma sana kama vile mtakatifu anavyowaona watu wakitenda dhambi? Ina maana Uongozi ni Mwenyekiti tu ama uongozi ni mfumo wa taasisi unaosimamiwa na watu?

Huyu alikuwa anapigania kuhongwa uwaziri mdogo, ameshapata alichokuwa anakitaka. Na ashukuru ni waziri mdogo, angekuwa waziri mkubwa angekuwa ameshatumbuliwa kitambo.
 
Mkuu Juliana Shonza, kwanza naunga mkono hoja.
Lile la Nasari, na hili la Lissu, ni uthibitisho wa hoja zako kwenye bandiko hili.

Pili naomba angalia PM yako, imenibidi niku PM maana uvumilivu umenishinda.

P
Kwi kwi kwi, Pascal na cheupe utaishia kuimba ule wimbo "zabibu ni zako zile taratibu ...."
Kila LA kheri, haina kushindwa!
 
Mkuu Juliana Shonza, kwanza naunga mkono hoja.
Lile la Nasari, na hili la Lissu, ni uthibitisho wa hoja zako kwenye bandiko hili.

Pili naomba angalia PM yako, imenibidi niku PM maana uvumilivu umenishinda.

P
Dah... Bosi...yaani umeshindwa kuvumilia kweli?
 
Ulifukuzwa CHADEMA baada ya ku misbehave;uko ccm unaenjoy maisha,haya mambo ya CHADEMA na MBOWE unayafuatilia kwa nini?unam-potray kama weak leader kama ndivyo kwa nini uumie ww green guard badala ya kifurahia.
Na kama MBOWE ni weak leader why mnaendelea kumuandama kwa visa lukuki.
Hiyo unayofanya mimi naitaga political masturbation
 
Back
Top Bottom