Hitimisho: CHADEMA kuna ombwe la uongozi

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,009
1,607
AMANI IWE JUU YENU ENYI WAJA WEMA WA BWANA MUNGU WANGU...!!!

Naomba niwaombe radhi kwa kukaa kimya na kutochangia lolote kwa muda mrefu katika jukwaa hili muhimu. Naomba nichukue fursa hii kuendelea kuwafikirisha katika mambo muhimu ya kisiasa yanayoendelea katika siasa za nchi yetu hasa kambi ya upinzani. Wachambuzi mbalimbali, wasomi na waandishi wameendelea kuandika wakijaribu kutoa maoni yao na mitazamo mbalimbali juu ya yale yanayoendelea katika kambi ya upinzani nchini, wengi wao wamesema kuwa yanayoendelea CUF na CHADEMA ni matokeo yanatokana na NGUVU YA VIPANDE VYA RUPIA vilivyoingia katika kambi hiyo tangu wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015. Kwa upande wangu nimekuwa nikijaribu kutoa mwelekeo mwingine wa fikra, mimi binafsi naamini kuwa SINTOFAHAMU iliyoikumba kambi hiyo inatokana na OMBWE LA UONGOZI.

Septemba 10, 2015 niliandika kuwa FEDHA ni tatizo lakini tatizo halisi ni kukosa Uongozi imara, hata sababu zilizopelekea kupokea FEDHA hiyo na kumpokea aliyezitoa kunatokana na sababu kuu ya OMBWE LA UONGOZI, nilionyesha udhaifu huo kwa maandishi haya CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

August 31, 2016 mwaka mmoja baadae na hasa baada ya kushindwa kwa operesheni ya UKUTA niliandika tena kwa msisitizo Msisitizo; CHADEMA kuna ombwe la uongozi nikieleza namna mipango yao ilivyo ya hovyo na unrealistic, ambayo imekuwa inashindwa wakati wote, nikaeleza kwa kina kuwa tatizo hasa ni OMBWE LA UONGOZI.

Na leo naandika tena nikihitimisha mjadala huu, kwa maana nimejiridhisha kuwa hawa ni watu wenye macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii wao ni kama wafu ama punda aliyefungwa hatamu, wakivutwa kulia wanafuata na wakigeuzwa kushoto ndio unakuwa mwelekeo wao. Hawana hoja, hawana mpango kazi na hawana ajenda, bado ni wanaharakati wanaoendeshwa kwa matukio.

Niliwahi kusema na kutoa ushauri katika vikao na kwa viongozi wa CHADEMA wakati nikiwa mwanachama wa Chama hiko kuwa "sina IMANI na uwezo na maarifa ya Mwenyekiti MBOWE kukivusha Chama katika wakati huu, ni vyema na ni kutokana na utaratibu wa kidemokrasia ndani ya Chama uliokuwepo kikatiba watu wengine waruhusiwe kugombea na ikiwa wanachama wengi watakubali kufanya mabadiliko ya Mwenyekiti, UAMUZI wao uheshimiwe, miongoni mwa wanaotaka mabadiliko hayo ni pamoja na Mimi." Baada ya kusema hayo niliondolewa CHADEMA. Lakini sikukaa kimya, niliendelea kusema na kukosoa aina ya uongozi dhaifu wa Kambi ya upinzani na nilifanya hivyo kwa maslahi mapana ya nchi yangu, nikaandika Ushuhuda: Freeman Mbowe ni kiongozi dhaifu nikiuambia Umma kuwa lipo tatizo kubwa kwenye upinzani nchini linalotokana na udhaifu wa Viongozi wake.

Kama ilivyo kawaida ya Vijana wa UFIPA wakajitokeza kwa wingi, wakitukana na kunikosoa bila hoja, wakisifu Ujio wa LOWASSA kwenye chama chao, wakipongeza uamuzi wa Mbowe wa kumuondoa SLAA na kumuweka MASHINJI, nilipowaambia Chama chao kimepotezwa mwelekeo na hakiungwi tena mkono na watu wenye akili na wanaojielewa, watu wote waliokuwa wakiandika na ku-praise upinzani wamegeuka na wengine wameduwaa kwa kinachoendelea kwenye upinzani, wamebaki wachache wasiojielewa na ambao binafsi niliwapuuza na kuwaambia watanzania wawapuuze kwa maneno haya Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu wengi katika umma wa watanzania wameendelea kuiona rangi halisi ya watu hawa na nashukuru wamekubaliana na mimi kuwapuuza watu wapuuzi. Kwanini wasiwapuuze kama leo kete yao ya turufu ni WEMA SEPETU, ndio mtoa hoja ndio msemaji na mtetezi wa upinzani, kwanini watanzania wasiwapuuze ikiwa MANGE ndio jiwe kuu na mwamba unaotumainiwa, kwanini msipuuzwe..???

Nimeandika hapa nifunge mjadala huu, kwa kuwa watanzania wameshashuhudia na imedhihirika kwao juu ya udhaifu wa upinzani, na namshukuru BWANA MUNGU WANGU kwa upendo wake kwa watanzania akatufunulia yale yaliyomo sirini mwao, YEYE ni shahidi na mwanga unaotuongoza.

Nchi sasa imetulia, nchi inasonga mbele na watanzania wameendelea kushuhudia UONGOZI uliotukuka na wenye nia ya kweli ya kuwakomboa na kutimiza ndoto na kiu yao ya muda mrefu ya kupata maendeleo.
 
Blah blah blah...

Mnaacha kudiscuss matatizo ya nchi kama kufifia kwa demokrasia nchini,viashiria vya udikteta,kupuuzwa kwa katiba,mihimili ya serikali kuingiliana kwenye kutimiza wajibu wake etc

Mnakazana na mambo ya chadema hivi, chadema vile.
Kwani kua chama kingine ndio tiketi ya kujitoa ufahamu, ifike kipindi hata kama hamna uwezo wa kufikiri basi walau mpretend mnaweza kufikiri.

Sasa umeandika nini hapa! mbaya zaidi unamhushisha Mungu na mambo ya mipasho,seriously!?!?

Jifunzeni kujenga hoja ili hata huko mjengoni muwe mnasupport mambo ya maana.
Huwa najifikiria sana inakuaje mtu kama kibajaji kila akiongea upuuzi watu wanagonga meza na kushangilia?

Leo nigundua tatizo hamna ma think tank...hamna watu wenye uwezo wa kuja na mada zenye maana na mantiki.
ukosefu wa uwezo wakujenga hoja zenye mashiko, outcome ndio andiko kama hili.
 
Nchi sasa imetulia, nchi inasonga mbele na watanzania wameendelea kushuhudia UONGOZI uliotukuka na wenye nia ya kweli ya kuwakomboa na kutimiza ndoto na kiu yao ya muda mrefu ya kupata maendeleo.


upload_2017-8-3_12-32-29.png
 
Jimbo lako linamaendeleo yeyote naona umesahau kilichokupeleka bungeni.Toa ushauri huu huko ulipo.Pilipili usiyoila inakuwashia nini?
 
Mleta mada kuna mtu jana aliwataka wanachama na wanazi wa ccm waseme wanamaanisha nini wanaposema wapinzani hawana hoja. Je ww unaweza ukatuambia hoja ni nini, na ipi ni tofauti kati ya hoja na sera? Ukiweza kujibu hilo utatusaidia sana.

Halafu Juliana Shonza huwa tunakushangaa, huwa huchangii mada za wengine hapa jukwaani lakini ww hupenda kuleta mada ndefu zinazokufurahisha ww tu, bila kuingia kwenye mada za wengine. Je umegeuza hili jukwaa ni jalala la ww kuja kumwaga takataka zako kisha usichangie lolote mpaka pale unapokutana na neno linalokuuma ndio ujibu tena kwa jazba? Jitafakari.
 
Juliana hakika wewe ndiye una ombwe katika ubongo wako, wewe ulishaachana na Chadema ni vema ukajikita katika sisa za CMM , mambo ya Chadema waachie wana Chadema wenyewe, mbona hutulii kwani ulisahau nini Chadema?

Wewe na mzee wako Mpendazoe kutwa kucha mnahangaika na Chadema, au sasa hivi kipaumbele cha CCM ni kupambana na Chadema badala ya kupambana na changamoto za kuwaletea Watanzania maendeleo?
 
Umenifurahisha sana hapo nchi imetulia,nchi inasonga mbele na watanzania wameendelea kushuhudia UONGOZI uliotukuka
Ki ukwel ccm inatakiwa iwafundishe hawa ndgu zang vyama vinapodai democracy vianze kuonyesha democracy ndan yake ..CHADEMA kikanda CHADEMA mwenyekiti hanyoshewi kidole kisa mchaga
.
.
.
kyenekyaka nkighanile une


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viti Maalumu Hatari Na Ugonjwa Kwa Taifa Futilia Mbali Kule Hawa Ndo Waliopitisha Sheria Za Makinikia Leo Mnawasumbua Wakina Profesa Kabudi Wakat Muda Huu Angekaa Kubuni Jambo Zuri Kwa Taifa Sasa Mzee Anahangaika Kule Kwa Ujinga Wa Watu Flani.
 
Juliana nina mashaka na uwezo wako wa kufikiri, Kama umeolewa huyo mumeo ana kazi sana sikutegemea mbunge wa viti maalum kuwa na mawazo na uandishi unaofanana na mtoto wangu wa darasa la nne, Badala ya kujadili hoja unamjadili Mbowe, Mbowe atakusaidia nini?

Mbowe ana uwezo wa kurusha ukoo wako wote huko kijijini pamoja na wajuu zako, Tatizo kubwa ulilonalo Umezaliwa familia maskini hivyo kuingia kwenye siasa na kutumia kodi zetu bungeni umeshasahau ndugu zako kwenye ukoo ambao kwa umaskini wao hata wewe binafsi hupendi kuongozana nao kisa umekuwa mbunge wa viti maalum.

Kikubwa angalia ulikotoka binti kesho utarudi mtaani kwani kuna Maisha nje ya bunge.

Usione mtu kama Nape na Mwigulu wamebadili aina ya siasa zao kwani wamegundua alama chafu walizoziacha bora wakae kimya ili watu wawasamehe, Wewe ni nani ndani ya CCM?

Hiki ni kipindi cha mpito cha uongozi watu wanajua kitapita iwe upinzani au ndani ya CCM
 
Sku zote kama ww ni mwanaharakati na ili ufanikishe lazma uwe na falsafa inayoeleweka mbele ya hadhira. Hapo ndipo utapata watu wakukuunga mkono.

Lakn usipokuwa na falsafa inayoeleweka utakuwa unapoteza nguvu yako bure.

Angalia revolution za akina Mao ze dong , vradimir ilych Lenin.

Walikuwa na misimamo juu ya kile wanachokipigania.

Hata ukiwasima akina Karl max wanasisitiza juu ya falsafa inayeleweka.

Wenzetu hapo mwanzo waliaminiwa sana baada ya kuanza kupiga vita ufisadi na wakawa wanaelezea kwa mifano hai na mpaka wananchi wakawaelewa lakn Mara ghafla wao wanaita gia angani wakabadili maada mpaka wale waliokuwa wanawatolea mifano wakawasafisha ..
Atakayeweza kuwaelewa hapo labda ni maiti pekee
 
Sina tatizo lolote kwa mwana ccm kuukosoa uongozi wa Chadema au CUF ya Maalimu Seif kwasababu huo ndio upinzani wenyewe.
Kwa upande wangu naomba nikuulize hivi Juliana; Ulijiunga ccm baada ya kufukuzwa Chadema (hukuondoka kwa hiyari, naomba records zikae sawa) ikiwa chini ya Jakaya Mrisho Kikwete, leo upo ccm chini ya JPM ambaye kusema ukweli ni kama anawakosoa sana watangulizi wake kivitendo though kimaneno haoneshi hivyo, swali Je! Imani yako kwa ccm hizi 2 ikoje? The second question is, mara baada ya wewe kufukuzwa Chadema uliwahi ku post picha za kumkejeri sana Dr. Slaa kule facebook (kama sikosei ilikua kipindi wakati anachaguliwa huyu papa wa RC, ulionesha kwamba Dr. Slaa kama sio madhambi yake huenda nae angekua kwenye team ya kumchagua Pope mpya). Nini msimamo wako kwa Dr. Slaa kiuongozi!? Naomba ujibu ukiwa unajua Mungu anakutazama hadi kwenye chembe ya moyo wako, I said so kwasababu wewe umewahi kuokoa so you know what I am saying!!!
 
Back
Top Bottom