Hitimisho: CHADEMA kuna ombwe la uongozi

Hitimisho: CHADEMA kuna ombwe la uongozi

Lumumba buku 7 baada ya kushindwa kuweka mtu wao ili waiendeshe CDM watakavyo basi wamenanza ku-retrieve vi-thread vya zama za kale.
 
AMANI IWE JUU YENU ENYI WAJA WEMA WA BWANA MUNGU WANGU...!!!

Naomba niwaombe radhi kwa kukaa kimya na kutochangia lolote kwa muda mrefu katika jukwaa hili muhimu. Naomba nichukue fursa hii kuendelea kuwafikirisha katika mambo muhimu ya kisiasa yanayoendelea katika siasa za nchi yetu hasa kambi ya upinzani. Wachambuzi mbalimbali, wasomi na waandishi wameendelea kuandika wakijaribu kutoa maoni yao na mitazamo mbalimbali juu ya yale yanayoendelea katika kambi ya upinzani nchini, wengi wao wamesema kuwa yanayoendelea CUF na CHADEMA ni matokeo yanatokana na NGUVU YA VIPANDE VYA RUPIA vilivyoingia katika kambi hiyo tangu wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015. Kwa upande wangu nimekuwa nikijaribu kutoa mwelekeo mwingine wa fikra, mimi binafsi naamini kuwa SINTOFAHAMU iliyoikumba kambi hiyo inatokana na OMBWE LA UONGOZI.

Septemba 10, 2015 niliandika kuwa FEDHA ni tatizo lakini tatizo halisi ni kukosa Uongozi imara, hata sababu zilizopelekea kupokea FEDHA hiyo na kumpokea aliyezitoa kunatokana na sababu kuu ya OMBWE LA UONGOZI, nilionyesha udhaifu huo kwa maandishi haya CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

August 31, 2016 mwaka mmoja baadae na hasa baada ya kushindwa kwa operesheni ya UKUTA niliandika tena kwa msisitizo Msisitizo; CHADEMA kuna ombwe la uongozi nikieleza namna mipango yao ilivyo ya hovyo na unrealistic, ambayo imekuwa inashindwa wakati wote, nikaeleza kwa kina kuwa tatizo hasa ni OMBWE LA UONGOZI.

Na leo naandika tena nikihitimisha mjadala huu, kwa maana nimejiridhisha kuwa hawa ni watu wenye macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii wao ni kama wafu ama punda aliyefungwa hatamu, wakivutwa kulia wanafuata na wakigeuzwa kushoto ndio unakuwa mwelekeo wao. Hawana hoja, hawana mpango kazi na hawana ajenda, bado ni wanaharakati wanaoendeshwa kwa matukio.

Niliwahi kusema na kutoa ushauri katika vikao na kwa viongozi wa CHADEMA wakati nikiwa mwanachama wa Chama hiko kuwa "sina IMANI na uwezo na maarifa ya Mwenyekiti MBOWE kukivusha Chama katika wakati huu, ni vyema na ni kutokana na utaratibu wa kidemokrasia ndani ya Chama uliokuwepo kikatiba watu wengine waruhusiwe kugombea na ikiwa wanachama wengi watakubali kufanya mabadiliko ya Mwenyekiti, UAMUZI wao uheshimiwe, miongoni mwa wanaotaka mabadiliko hayo ni pamoja na Mimi." Baada ya kusema hayo niliondolewa CHADEMA. Lakini sikukaa kimya, niliendelea kusema na kukosoa aina ya uongozi dhaifu wa Kambi ya upinzani na nilifanya hivyo kwa maslahi mapana ya nchi yangu, nikaandika Ushuhuda: Freeman Mbowe ni kiongozi dhaifu nikiuambia Umma kuwa lipo tatizo kubwa kwenye upinzani nchini linalotokana na udhaifu wa Viongozi wake.

Kama ilivyo kawaida ya Vijana wa UFIPA wakajitokeza kwa wingi, wakitukana na kunikosoa bila hoja, wakisifu Ujio wa LOWASSA kwenye chama chao, wakipongeza uamuzi wa Mbowe wa kumuondoa SLAA na kumuweka MASHINJI, nilipowaambia Chama chao kimepotezwa mwelekeo na hakiungwi tena mkono na watu wenye akili na wanaojielewa, watu wote waliokuwa wakiandika na ku-praise upinzani wamegeuka na wengine wameduwaa kwa kinachoendelea kwenye upinzani, wamebaki wachache wasiojielewa na ambao binafsi niliwapuuza na kuwaambia watanzania wawapuuze kwa maneno haya Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu wengi katika umma wa watanzania wameendelea kuiona rangi halisi ya watu hawa na nashukuru wamekubaliana na mimi kuwapuuza watu wapuuzi. Kwanini wasiwapuuze kama leo kete yao ya turufu ni WEMA SEPETU, ndio mtoa hoja ndio msemaji na mtetezi wa upinzani, kwanini watanzania wasiwapuuze ikiwa MANGE ndio jiwe kuu na mwamba unaotumainiwa, kwanini msipuuzwe..???

Nimeandika hapa nifunge mjadala huu, kwa kuwa watanzania wameshashuhudia na imedhihirika kwao juu ya udhaifu wa upinzani, na namshukuru BWANA MUNGU WANGU kwa upendo wake kwa watanzania akatufunulia yale yaliyomo sirini mwao, YEYE ni shahidi na mwanga unaotuongoza.

Nchi sasa imetulia, nchi inasonga mbele na watanzania wameendelea kushuhudia UONGOZI uliotukuka na wenye nia ya kweli ya kuwakomboa na kutimiza ndoto na kiu yao ya muda mrefu ya kupata maendeleo.
Wewe ni wa ajabu sana na shombo isiyomithilika.
1. Baadhi ya Watanzania sisi wa JF siyo wakuelezwa ili tukubaliane na upuuzi wako kwa sababu unalolisimamia linaeleweka.
2. Mimi mwana nchi huku mtaani najua kuwa kete yenu kubwa ni kuudhofisha uongozi wa upinzani kwa kuwawekea vibaraka wenu ili upinzani uwe dhaifu kwa sababu nyie ni dhaifu. Wakati huo huo mnatatiza fursa zote wasfinye siasa tena kinyume na sheria zilizopo.
3. Kuthibitisha kuwa nyie ni hovyo, mmejikita kwenye kuwashughulikia viongozi wa upinzani. Kwa taarifa yenu pamoja na vitisho vya kiimla na dola sisi wananchi tunajua upinzani una nguvu gani na nyie ni wadhaifu kiasi gani.
4. Ombwe la uongozi unaloliona kwa upinzani ni nafuu kuliko ombwe la uongozi wa awamu hii. Kwanza hakuna uongozi awamu hii zaidi ya unyapara. Kwa akili yako ya nyonga huna nafasi ya kupitia katiba ukajiridhisha kuwa mamlaka yanatokana na wananchi. Kila figisu zinafanywa kutupoka mamlaka sisi wenye tuliowaweka hapo mlipo. Na hayo kwa akili yenu mnahamisha ombwe la uongozi wenu kwa kuwabambikia maombwe viongozi wa upinzani.
HITIMISHO
Huko serikali mnatengeza haya maombwe ya uongozi ili muendeleze unyapara umbumbu ushamba na uimla. Yote ni ili mbaki madarakani. Hamjui sisi wananchi tuna umia kiasi gani kiuchumi na kijamii. Tunaishi kama tupo msituni kutokana na kukosekana uongozi wenu wakutarajiwa.
 
Juliana shonza ametumia haki yake ya kutoa maomi yake kama mtanzania huru!

Tatizo lenu vijana na wafuasi wa chadema ni kwamba huwa hampendi kuambiwa ukweli daima.

pale anapotokea mtu na kuwapasulia ukweli,basi nyinyi mtakaa mnamkashifu na kumtukana,huku mnajiita chama cha demokrasia, wakati hamuishi wala kuamini katika demokrasia,bali ni kundi kubwa la kikanda linaloishi kwa maslahi BINAFSI.

kama yanayoonekana kwenye uchaguzi wenu ndio demokrasia,
basi hii itakuwa ni demokrasia ya survival of the fittest!
ukimgusa mkubwa na wanawe inakula kwako.

Humu JF,
watu wa kada mbalimbali wanatoa maoni yao kuhusu suala la demokrasia ndani ya vyama vya upinzani Tanzania, lakini wanaambulia kejeli na matusi tena mengine ya ajabu.
hapo hamjashika ikulu,je kama hii ni ruzuku tu ndio inawagawa hivi,hebu mjitafakari kama mngepewa ikulu na hazina,PANGETOSHAA?.

MAENDELEO hayana vyama,ila mimi nasimama na JPM 2020-2025
 
Back
Top Bottom