Uchaguzi 2020 Hitaji la katiba ya JMT ibara ya 98, kifungu kidogo cha 1(b) ndiyo sababu kuu ya kuenguliwa wagombea ubunge wa ACT Wazalendo, Pemba

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Mada ya uzi huu si ngeni kwetu sisi Watanzania. Nina uhakika wengi (kama si wote) tunaIfahamu vyema hii kitu lakini ni wakati muafaka kuweka msisitizo hususani kutokana na mazingira tuliyo nayo sasa kuhusiana na mwenendo wa teuzi za wagombea urais, ubunge na madiwani kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Ibara tajwa hapo juu inahitaji kwamba mabadiliko yoyote katika Toleo la 1977 la Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (JMT) ni lazima yapitishwe na theluthi mbili (2/3) ya wabunge kutoka upande wa Zanzibar.

Tangu 2016 kumekuwepo na jitihada kubwa (za wazi na za kificho) kwa wana CCM wengi (hususani wabunge wa chama hiki) kupenyeza ajenda ya kutaka ama kurefusha muhula wa urais kutoka miaka 5 ya sasa au kuongeza idadi ya mihula kutoka 2 ya sasa. Kwa jinsi walivyokuwa na munkari baada ya urais kupitia CCM kukoswakoswa kidogo sana kwenye uchaguzi wa 2015, dhamira ya CCM ilikuwa kufanya hivi mapema lakini kilichowakwamisha ni kukosekana kwa theluthi mbili kutoka kwa wabunge wa Zanzibar ambapo wabunge wa CCM pekee wasingeweza kufikisha quota hiyo. Ile nunua nunua ya wabunge, pamoja na malengo mengine ya kisiasa, ulikuwa pia ni mkakati wa kutaka kuwanasa wabunge wa CUF kutokea Zanzibar lakini tumshukuru Mungu kuwa Wazanzibari ni watu wanaojitambua sana kuliko watu wa huku bara.

Kwa hiyo ni wazi kabisa sarakasi zinazoendelea huko Pemba ni mkakati wa makusudi wa kufikia lengo hilo ovu la kuihujumu haki ya Watanzania kupitia mabadiliko haramu ya katiba.

Watanzania tuwe macho ili kuilinda nchi yetu isiwe dola ya kiimla. TUWE MACHO!.
 
Hii sababu itoshe kwa Chadema, ACT na CHAUMA kutamka uenguaji wa wagombea wao ni haramu na washughulikie hilo kabla ya kuendelea na kampeni
 
Back
Top Bottom