Historia ya Sarafu Yetu Tanzania

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,209
2,000
Umetukumbusha mbali ingawa sio mbali sana kwa maisha
Nimeziona za mkoloni mpaka zilipokuja kubadilika na kuja za uhuru
Senti 20 unapata chapati zako na kachumbari
Kilo ya nyama nakumbuka ilikuwa Tsh 1.70
Utumbo senti 60
Yaani nikikumbuka hela yetu ilivyokuwa na thamani
Ilipotoka noti ya masai nadhani ndio ikaanza kushuka kidogo
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,148
2,000
Kuanzia mwaka 1998, sarafu yetu ilikuwa imara tena na haijatolewa sarafu nyingine mpya kwa karibu miaka tisa sasa. Mpaka sasa sarafu kubwa zinazotumika ni zile za shillingi 50, 100 na 200 zionekazo hapa chini:

Shilingi 50

Shilingi 100

Shilingi 200

Hata hivyo, sarafu zote zilizowahi kutolewa na benki kuu ya Tanzania bado ni halali ingawa ama hazipatikani tena kwenye mzunguko au zimashekuwa na thamani ndogo kiasi kuwa zinahitajika nyingi sana ili kufanya manunuzi ya aina yoyote. Katika historia ya benki kuu, hakuna sarafu yake iliyowahi kufutwa.

Usisahau kusoma Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania
nini maana ya neno SHILINGI??
kwa nn tulibadili kutoka CENT kwenda SHILINGI?? maana tungekua na "cent 100,cent 10,000 cent 100,000 n.k
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,148
2,000
Ndugu Ousofia, Kuanzia mwaka 1920 nchi za Afrika ya mashariki zilikuwa zinatumia sarafu moja; sarafu ya kwanza ilikuwa ni East African Florin, ambayo ilikuwa replaced na East African Shilling baada ya muda mfupi usiozidi miezi sita. Nchi hizo zilitengana mwaka 1966 ambapo kila nchi ikawa na sarafu yake ingwa zote zileiendelea kutumia Shillingi; yaani kukawa na shilingi ya Kenya, shillingi ya Uganda na Shillingi ya Tanzania.
nini maana ya neno SHILINGI??
kwa nn tulibadili kutoka CENT kwenda SHILINGI?? maana tungekua na "cent 100,cent 10,000 cent 100,000 n.k
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,148
2,000
name nimekumbuka sarafu nilizotumia kutokana na umri wangu, kuazia sent 50 hadi hizi za leo
nini maana ya neno SHILINGI??
kwa nn tulibadili kutoka CENT kwenda SHILINGI?? maana tungekua na "cent 100,cent 10,000 cent 100,000 n.k
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,411
2,000
nini maana ya neno SHILINGI??
kwa nn tulibadili kutoka CENT kwenda SHILINGI?? maana tungekua na "cent 100,cent 10,000 cent 100,000 n.k
Jina la Shillingi limetokana na neno la kijerumani la Schilling ambalo asili yake ni neno la zamani sana (miaka takriban mia elfu mbili zilozopita) katika lugha za Vikings wa nchi za Scandinavia la Skilling lililokuwa na maana ya thamani wakati huo. Waingereza waliamua kutumia sarafu ya Shilingi katika makoloni yake yote mwaka 1920 baada ya vita kwa vile sarafu hiyo ilikuwa maarufu katika nchi kadhaa za Ulaya ambako Ujerumani ilikuwa imepoteza influence. Ilitumika katika nchi kama Australia, New Zealand, Austria, Uholanzi na kwingineko. Senti moja ni sehemu mia moja za shillingi; nadhani unajua kuwa katika vipimo kuna vitu kama sentimita yaani sehemu mia moja za mita, sentilita, yaani sehemu mia moja za lita na kadhalika. Kwa hiyo Senti haikubadilishwa kwa shillingi, ila baada ya shilingi kuporomoka thamani kiasi hcvho ilikuwa ni wazi kuwa vipande vyake havikuwa na thamani pia katika matumizi ya kawaida, ndiyo maana huzioni senti huko mitaani.
 
shukran mkuu nimekuelewa
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,411
2,000
 1. Nimekuwa natafiti pole pole kutafuta picha za pesa tulizowahi kutumia hapa kwetu, nikaona nizitundike hapa kukumbushana tulikotoka. Kuna sarafu ambazo nimeshindwa kupata picha zake, lakini hata hivyo nadhani nimefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 kukusanya ukweli kuhusu sarafu yetu. Najua kuwa hadithi hii ni ndefu sana, hata hivyo kama unataka kujua historia ya sarafu yetu jipe dakika kumi hivi kuisoma yote hapa; ni burudani ya aina yake.

  Kabla ya mwaka 1884, nchi yetu ilikuwa inatumia sarafu moja ya Riyal iliyokuwa imetolewa na Sultan wa Zanzibar chini ya Sultani wa Oman. Sarafu za Riyal zilikuwa kama ifuatavyo

  Riyal

  Baada ya 1884, Zanzibar ilitumia sarafu za aina tatu kwa mpigo. Sarafu ya kwanza ilijulikana kama Maria Theresa Thaler iliyotolewa Italy, ilikuwa na sura ifuatayo.

  Maria Theresa Saler

  Sarafu ya pili ilikuwa ni rupia ya kihindi pamoja na visehemu vyake ambavyo vilikuwa vingi kidogo. Sehemu kubwa za rupia zilikuwa ni Anna, pice , robo rupia na nusu rupia:

  1 Anna

  1/4 rupee  1/2 rupee

  1 rupee  Pesa hizi zilikuwa ngumu sana hasa kwa vile Anna ilikuwa na vipande vingine kama 1/12 ya Anna, 1/6 ya Anna, 1/4 ya Anna na kadhalika. Sikuweka picha za vipande hivi ingawa ninavyo.

  Sarafu ya tatu ilikuwa inajulikana kama Zanzibari Rupee ambao kimsingi ilikuwa sawa na rupee ya kiingereza iliyokuwa ikutumika Kenya na Uganda. Sikupata picha yake.

 2. senti 20

  senti 50

  Shilingi 1

  Sarafu hizi zinaendelea kutumika hadi leo ingawa thamani ya shilingi imeshuka kiasi kuwa zinaonekana hazina thamani yoyote. Ilipofika mwaka 1971 wakati wa sherehe za miaka kumi ya uhuru, sarafu mpya ya shilingi tano iliyokuwa na pembe kumi na mbili ilitolewa. Wakati huo exchange rate ya dola kwa shilingi ilikuwa ni shilingi tano kwa dola moja ya kimarekani. Kwa hiyo sarafu hii ya shilingi tano ilijuikana pia kama "dola" au "DALA" ingawa kwenye mikoa ya ziwa ilijulikana zaidi kama "Scania." Nadhani mnakumbukua chanzo cha neno "dala dala" ni kutokana na nauli ya mabasi hayo wakati huo kuwa shilingi tano. Sarafu hii ya miaka kumi ya uhuru haikudumu sana na mwaka 1972 ikabadilishwa sura na kuwa na pembe kumi kama ifuatavyo.

  Shilingi 5

  Kuna taarifa kuwa mwaka 1974 sarafu mpya za shilingi 25 na shilingi 1000 zilitolewa ingawa benki kuu haikutunza picha zake. Ingawa sikuweza kupata sura ya sarafu ya shillingi 1000, nimefanikiwa kupata picha ya sarafu ya shillingi 25 ambayo ilikuwa na sura ifuatayo:

  shilingi 25

  Mara baada ya kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977, thamani ya pesa ilianza kupunguka pole pole kiasi kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na sarafu kati ya senti ishirini na senti tano. Hivyo sarafu ya senti kumi iliingizwa kwenye mzunguko; sarafu hii ilikuwa kama ifuatavyo.

  senti 10

  Kufuatia mkutano wa FAO uliofanyika Arusha mwezi September mwaka 1978, sarafu chache za shillingi 5 zilitolewa kukumbukia mkutano huo; sarafu hizo zikuwa na sura ifuatayo

  Shillingi 5

  Baada ya hapo, hakukuwa na sarafu mpya hadi mwaka 1982 wakati wa sherehe za miaka 20ya uhuru ambapo sarafu mpya ya shillingi 20 ilitolewa ikiwa na sura ifuatayo.
.................Inaendelea.
Hii inajulikana kitaalamu kuwa ni plagiarism!
 
Mgwisha

Member
Jul 23, 2012
23
45
Ogah,

wewe unaziona hizo picha za sarafu?

mimi naona vijialama vya times (x) rangi nyekundu tu.
Mi naziona tena vizuri kabisa na nyingi kwa bahati za kuanzia 1966 nimeztumia nikiwa mdogo miaka ya sabini mwishoni na kuendelea
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom