Historia ya Sarafu Yetu Tanzania

mourisous

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2016
Messages
441
Points
500

mourisous

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2016
441 500
aiseee ngoja nikimbile Bank nikazichange zile gunia mbili za shilingi tano zangu maana niliziacha kama ukumbusho kumbe PESA IPO ndani Na mm nalia njaa
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Messages
35,020
Points
2,000

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2017
35,020 2,000
Shukrani sana Kichuguu kwa historia nzuri sana.
Umenifumbua macho na kuona mengi niliyokuwa siyajui hasa kwa sarafu za nchi yetu na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Pia nimejua chanzo cha neno Dala dala.

Big up mkuu.

So far away

Member
Joined
Jan 7, 2017
Messages
59
Points
150

So far away

Member
Joined Jan 7, 2017
59 150
 1. Nimekuwa natafiti pole pole kutafuta picha za pesa tulizowahi kutumia hapa kwetu, nikaona nizitundike hapa kukumbushana tulikotoka. Kuna sarafu ambazo nimeshindwa kupata picha zake, lakini hata hivyo nadhani nimefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 kukusanya ukweli kuhusu sarafu yetu. Najua kuwa hadithi hii ni ndefu sana, hata hivyo kama unataka kujua historia ya sarafu yetu jipe dakika kumi hivi kuisoma yote hapa; ni burudani ya aina yake.

  Kabla ya mwaka 1884, nchi yetu ilikuwa inatumia sarafu moja ya Riyal iliyokuwa imetolewa na Sultan wa Zanzibar chini ya Sultani wa Oman. Sarafu za Riyal zilikuwa kama ifuatavyo

  Riyal

  Baada ya 1884, Zanzibar ilitumia sarafu za aina tatu kwa mpigo. Sarafu ya kwanza ilijulikana kama Maria Theresa Thaler iliyotolewa Italy, ilikuwa na sura ifuatayo.

  Maria Theresa Saler

  Sarafu ya pili ilikuwa ni rupia ya kihindi pamoja na visehemu vyake ambavyo vilikuwa vingi kidogo. Sehemu kubwa za rupia zilikuwa ni Anna, pice , robo rupia na nusu rupia:

  1 Anna

  1/4 rupee  1/2 rupee

  1 rupee  Pesa hizi zilikuwa ngumu sana hasa kwa vile Anna ilikuwa na vipande vingine kama 1/12 ya Anna, 1/6 ya Anna, 1/4 ya Anna na kadhalika. Sikuweka picha za vipande hivi ingawa ninavyo.

  Sarafu ya tatu ilikuwa inajulikana kama Zanzibari Rupee ambao kimsingi ilikuwa sawa na rupee ya kiingereza iliyokuwa ikutumika Kenya na Uganda. Sikupata picha yake.

 2. senti 20

  senti 50

  Shilingi 1

  Sarafu hizi zinaendelea kutumika hadi leo ingawa thamani ya shilingi imeshuka kiasi kuwa zinaonekana hazina thamani yoyote. Ilipofika mwaka 1971 wakati wa sherehe za miaka kumi ya uhuru, sarafu mpya ya shilingi tano iliyokuwa na pembe kumi na mbili ilitolewa. Wakati huo exchange rate ya dola kwa shilingi ilikuwa ni shilingi tano kwa dola moja ya kimarekani. Kwa hiyo sarafu hii ya shilingi tano ilijuikana pia kama "dola" au "DALA" ingawa kwenye mikoa ya ziwa ilijulikana zaidi kama "Scania." Nadhani mnakumbukua chanzo cha neno "dala dala" ni kutokana na nauli ya mabasi hayo wakati huo kuwa shilingi tano. Sarafu hii ya miaka kumi ya uhuru haikudumu sana na mwaka 1972 ikabadilishwa sura na kuwa na pembe kumi kama ifuatavyo.

  Shilingi 5

  Kuna taarifa kuwa mwaka 1974 sarafu mpya za shilingi 25 na shilingi 1000 zilitolewa ingawa benki kuu haikutunza picha zake. Ingawa sikuweza kupata sura ya sarafu ya shillingi 1000, nimefanikiwa kupata picha ya sarafu ya shillingi 25 ambayo ilikuwa na sura ifuatayo:

  shilingi 25

  Mara baada ya kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977, thamani ya pesa ilianza kupunguka pole pole kiasi kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na sarafu kati ya senti ishirini na senti tano. Hivyo sarafu ya senti kumi iliingizwa kwenye mzunguko; sarafu hii ilikuwa kama ifuatavyo.

  senti 10

  Kufuatia mkutano wa FAO uliofanyika Arusha mwezi September mwaka 1978, sarafu chache za shillingi 5 zilitolewa kukumbukia mkutano huo; sarafu hizo zikuwa na sura ifuatayo

  Shillingi 5

  Baada ya hapo, hakukuwa na sarafu mpya hadi mwaka 1982 wakati wa sherehe za miaka 20ya uhuru ambapo sarafu mpya ya shillingi 20 ilitolewa ikiwa na sura ifuatayo.
.................Inaendelea.
 
So far away

Member
Joined
Jan 7, 2017
Messages
59
Points
150

So far away

Member
Joined Jan 7, 2017
59 150
 1. Shillingi 20.

  Hiyo ndiyo iliyokuwa sarafu ya mwisho kutolewa wakati wa utawala wa Nyerere. Rais Mwinyi alipochukua madaraka mwaka 1985, aliendelea na sarafu zenye picha ya Nyerere hadi mwaka 1986 zilipotolewa sarafu zenye picha ya Mwinyi. Sarafu za senti tano,
  kumi, na ishirini hazikutolewa tena. Sarafu zilizotolewa wakati huo zilikuwa za senti 50, Shilingi 1, shilingi tano na shilingi kumi ambayo ilikuwa na sura ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Sarafu hizo ni hizi hapa:

  senti hamsini  Shilingi moja  Shilingi tano

  Shilingi 10  Kadri thamani ya shilingi ilivyoendelea kudorora, ilibdi kutengeneza sarafu nyingine ambapo sarafu ya shilingi 20 ilitolewa mwaka 1990 ikiwa na sura ya Mwinyi kama ifuatavyo.

  Shilingi 20  Mwaka huo huo sarafu nyingine ya shilingi 5 ilitolewa kwa kumbukumbu ya jengo jipya la benki kuu. Kwa bahati mbaya sikufanikiwa kupata picha yake. Mwishoni mwa utawala wa mwinyi, thamani ya shilingi ilikuwa chini kiasi kuwa sarafu ya Baba wa Taifa yenye thamani ya shilingu kumi ilikuwa inakimbilia kuishiwa nguvu yake. Hivyo sarafu mpya yenye sura wa baba wa taifa ikatengezwa ikiwa na thamani ya shillingi 100.

  Shilingi 100

  Rais Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995, akapiga marufuku matumizi ya sura za raisi aliyeko madarakani kwenye sarafu: alipendelea sura za waasisi wa taifa tu na picha alama za asili za nchi ndizo zitumike. Hata hivyo hakutaka kuondoa kabisa sura ya rais Mwinyi kwenye sarafu, hivyo ikatengezwa sarafu mpya ya shilingi 50 iliyokuwa na sura ya Mwinyi kama ionekanavyo hapo chini iliyotolewa mwaka 1996.

  Shilingi 50

  Wakati huo huo sarafu tatu zilitolewa kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 35 ya uhuru pamoja ni michezo ya 26 ya olimpiki iliyofanyika Atlanta Marekani mwaka huo. Sarafu hizi zilionyesha wachezaji wa kutupa tufe, riadha, na karate kama ifuatavyo.

  tufe

  riadha  karate

  Mwaka 1997 kulitolewa sarafu mbili mpya: moja ilikuwa na thamani ya shillingi 500 ikiwa inakumbukia miaka 75 tangu malkia Elizabeth mama wa malkia Elizabeth II alipotembelea nchi yetu mwaka 1923. Sarafu ya pili ilikuwa na thamani ya shillingi 200 ikiwa inatukuza mbuga za wanyama pori wa Afrika. Sarafu hizo zilikuwa na sura zifuatazo

  Shilingi 200
  Shilingi 500

  Mwaka 1998, ilitolewa sarafu nyingine ya kudumu ya shilingi 200 kuchukua nafasi ya sarafu zote za kumbukumbu zilizokuwa na thamani hiyo. Sarafu hiyo ilikuwa na picha Karume na inaonekana kama ifuatavyo:

  Shilingi 200

  Mwaka huo huo, ilitolewa sarafu nyingine ya thamani ya shilingi mia tano kutukuza mbuga za Serengeti. Sarafu hiyo ilikuwa na sura ifuatayo.

  Shilingi 500  ........................Inaendelea

 2. Kuanzia mwaka 1998, sarafu yetu ilikuwa imara tena na haijatolewa sarafu nyingine mpya kwa karibu miaka tisa sasa. Mpaka sasa sarafu kubwa zinazotumika ni zile za shillingi 50, 100 na 200 zionekazo hapa chini:

  Shilingi 50

  Shilingi 100

  Shilingi 200

  Hata hivyo, sarafu zote zilizowahi kutolewa na benki kuu ya Tanzania bado ni halali ingawa ama hazipatikani tena kwenye mzunguko au zimashekuwa na thamani ndogo kiasi kuwa zinahitajika nyingi sana ili kufanya manunuzi ya aina yoyote. Katika historia ya benki kuu, hakuna sarafu yake iliyowahi kufutwa.

  Usisahau kusoma Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania
 
Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Messages
9,693
Points
2,000

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2011
9,693 2,000
 1. Nimekuwa natafiti pole pole kutafuta picha za pesa tulizowahi kutumia hapa kwetu, nikaona nizitundike hapa kukumbushana tulikotoka. Kuna sarafu ambazo nimeshindwa kupata picha zake, lakini hata hivyo nadhani nimefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 kukusanya ukweli kuhusu sarafu yetu. Najua kuwa hadithi hii ni ndefu sana, hata hivyo kama unataka kujua historia ya sarafu yetu jipe dakika kumi hivi kuisoma yote hapa; ni burudani ya aina yake.

  Kabla ya mwaka 1884, nchi yetu ilikuwa inatumia sarafu moja ya Riyal iliyokuwa imetolewa na Sultan wa Zanzibar chini ya Sultani wa Oman. Sarafu za Riyal zilikuwa kama ifuatavyo

  Riyal

  Baada ya 1884, Zanzibar ilitumia sarafu za aina tatu kwa mpigo. Sarafu ya kwanza ilijulikana kama Maria Theresa Thaler iliyotolewa Italy, ilikuwa na sura ifuatayo.

  Maria Theresa Saler

  Sarafu ya pili ilikuwa ni rupia ya kihindi pamoja na visehemu vyake ambavyo vilikuwa vingi kidogo. Sehemu kubwa za rupia zilikuwa ni Anna, pice , robo rupia na nusu rupia:

  1 Anna

  1/4 rupee  1/2 rupee

  1 rupee  Pesa hizi zilikuwa ngumu sana hasa kwa vile Anna ilikuwa na vipande vingine kama 1/12 ya Anna, 1/6 ya Anna, 1/4 ya Anna na kadhalika. Sikuweka picha za vipande hivi ingawa ninavyo.

  Sarafu ya tatu ilikuwa inajulikana kama Zanzibari Rupee ambao kimsingi ilikuwa sawa na rupee ya kiingereza iliyokuwa ikutumika Kenya na Uganda. Sikupata picha yake.

 2. senti 20

  senti 50

  Shilingi 1

  Sarafu hizi zinaendelea kutumika hadi leo ingawa thamani ya shilingi imeshuka kiasi kuwa zinaonekana hazina thamani yoyote. Ilipofika mwaka 1971 wakati wa sherehe za miaka kumi ya uhuru, sarafu mpya ya shilingi tano iliyokuwa na pembe kumi na mbili ilitolewa. Wakati huo exchange rate ya dola kwa shilingi ilikuwa ni shilingi tano kwa dola moja ya kimarekani. Kwa hiyo sarafu hii ya shilingi tano ilijuikana pia kama "dola" au "DALA" ingawa kwenye mikoa ya ziwa ilijulikana zaidi kama "Scania." Nadhani mnakumbukua chanzo cha neno "dala dala" ni kutokana na nauli ya mabasi hayo wakati huo kuwa shilingi tano. Sarafu hii ya miaka kumi ya uhuru haikudumu sana na mwaka 1972 ikabadilishwa sura na kuwa na pembe kumi kama ifuatavyo.

  Shilingi 5

  Kuna taarifa kuwa mwaka 1974 sarafu mpya za shilingi 25 na shilingi 1000 zilitolewa ingawa benki kuu haikutunza picha zake. Ingawa sikuweza kupata sura ya sarafu ya shillingi 1000, nimefanikiwa kupata picha ya sarafu ya shillingi 25 ambayo ilikuwa na sura ifuatayo:

  shilingi 25

  Mara baada ya kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977, thamani ya pesa ilianza kupunguka pole pole kiasi kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na sarafu kati ya senti ishirini na senti tano. Hivyo sarafu ya senti kumi iliingizwa kwenye mzunguko; sarafu hii ilikuwa kama ifuatavyo.

  senti 10

  Kufuatia mkutano wa FAO uliofanyika Arusha mwezi September mwaka 1978, sarafu chache za shillingi 5 zilitolewa kukumbukia mkutano huo; sarafu hizo zikuwa na sura ifuatayo

  Shillingi 5

  Baada ya hapo, hakukuwa na sarafu mpya hadi mwaka 1982 wakati wa sherehe za miaka 20ya uhuru ambapo sarafu mpya ya shillingi 20 ilitolewa ikiwa na sura ifuatayo.
.................Inaendelea.
Kumbe hata zamani kulikuwa na wapmbav
 
pocoloco

New Member
Joined
Jun 7, 2015
Messages
3
Points
45

pocoloco

New Member
Joined Jun 7, 2015
3 45
Ni historia nzuri sana inasisimua ila mi ninasikitakita kuona thamani ya sarafu yetu ilivyoporomoka leo dola moja ya Marekani ni imependa thamani mara 440 zaidi ya ilivyokua miaka 45 iliyokwisha inasikitisha sana
 
Forum statistics

Threads 1,380,714
Members 525,856
Posts 33,777,576
Top