Amba Samedi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2024
- 205
- 336
Kuna historia ndani yako inayoshuhudia kuwa hata katika giza zito, nuru iliwahi kuchomoza. Pengine sasa umechoka, Mwili umelemewa, moyo umevunjika, na ndoto zako zinaonekana kwa mbali kwenye upeo wa macho yako.
Lakini historia yako haijaisha bado. Historia yako inajua kusimama tena, kusamehe tena, kuamini tena, na kupigana tena.
Usikate tamaa. Kumbuka ulipotoka. Kumbuka jinsi Mungu alivyokuinua pale ambapo wote walidhani umeanguka. Kumbuka yale machozi yaliyogeuka kuwa ushuhuda. Historia yako ina nguvu. Historia yako ni ushahidi wa rehema ya Mungu isiyoisha.
Leo, vuta pumzi. Simama tena. Tembea kwa imani, hata kama huoni mwisho wa njia. Kwa sababu historia yako bado inaendelea, na mwandishi wake ni Mungu ambaye hajawahi kushindwa.
Historia yako ni ushahidi kwamba bado kuna zaidi huko mbele na yajayo yanafurahisha.
Pr. Makore hapa
Wimbo Ulio Bora Media